Hofu hizi za wanawake!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,811
15,405
Kuna hofu nyingi kwa wanawake kudhani kwamba hawatapata wapenzi kwa sababu hawana matiti mazuri, hawana pua au midomo mizuri, hawana miili ya ‘Kizungu’, hawana mguu wa bia au hawana kiuno cha nyigu na makalio makubwa…….Ili mradi hofu, hofu, hofu……….

Hofu hizi hutokana na uongo ulio katika hatua hiyo ya kuelekea kujenga uhusiano. Ili kukabiliana na hili, ndio maana unakutana na wasichana wakiwa wanajinyima kula, wakiwa wanachubua ngozi zao, wakiwa wanafanya marekebisho ya sura (kwa wenye fedha) na mengine mengi.
Hii yote ni kutokana na kutojua tu. Ninavyofahamu ni kwamba, kinachoweza kumfanya mwanamke kuwa mzuri na kumvutia mwanaume yeyote ni tabasamu la kudumu. Tafiti nyingi zinaonyesha kwamba, kutabasamu humfanya mwanamke kuwavutia zaidi wanaume na hata wanawake wenzake. Kununa kumebainika kwamba hupunguza sana kiwango cha uzuri cha wanawake.
Badala ya kuhangaika kujinyima chakula, kujichubua, kujikandika vipodozi lukuki au kujiumiza kwa njia nyingine, njia rahisi ni kutabasamu tu, haigharimu, jaribu uone. Kumbuka hata hivyo kwamba, kutabasamu siyo kuchekacheka.
Hata kama umzuri vipi, mambo hayaishii hapo kwamba unakuwa tayari umejenga uhusiano, la hasha tabasamu na tabia pia vinachangia………………………
 
Hutegemeana na makuzi pamoja na hulka ya ndani ambayo kamwe haiwezi kulazimishwa, kutabasamu ni tabia hivyo likifanywa kwa unafiki bila kupenda il wengine waridhike unajikuta unaaribu zaidi..... hata hivyo ujenga upendo kwa wanaume..
 
Hakuna mwanamke mzuri wala mbaya. Inategemea na mahitaji ya mwanaume.
 
ndiyo maana biashara ya maduka ya vipodozi inalipa sana sasa hivi

dawa za kichina hata mlingotini nako wanaroga wapendwe
 
Duuu! Mimi nilikuwa naanza kinyume natafuta vilivyo ndani ya nguo
Ndio nije kuangalia vya nje.
Nawakilisha.
 
wengine ukitabasamu kila wakati tena kwa hawa viumbe wa jinsia tofauti na yetu hawakukosei neno binadamu mna wema!!!!!
 
Tabasamu zingine zinachekesha ati! Hujawahi kuona mtu anatabasamu halafu sura inakuwa kama anataka kupiga chafya?!
 
Kuna hofu nyingi kwa wanawake kudhani kwamba hawatapata wapenzi kwa sababu hawana matiti mazuri, hawana pua au midomo mizuri, hawana miili ya ‘Kizungu', hawana mguu wa bia au hawana kiuno cha nyigu na makalio makubwa…….Ili mradi hofu, hofu, hofu……….

Hofu hizi hutokana na uongo ulio katika hatua hiyo ya kuelekea kujenga uhusiano. Ili kukabiliana na hili, ndio maana unakutana na wasichana wakiwa wanajinyima kula, wakiwa wanachubua ngozi zao, wakiwa wanafanya marekebisho ya sura (kwa wenye fedha) na mengine mengi.
Hii yote ni kutokana na kutojua tu. Ninavyofahamu ni kwamba, kinachoweza kumfanya mwanamke kuwa mzuri na kumvutia mwanaume yeyote ni tabasamu la kudumu. Tafiti nyingi zinaonyesha kwamba, kutabasamu humfanya mwanamke kuwavutia zaidi wanaume na hata wanawake wenzake. Kununa kumebainika kwamba hupunguza sana kiwango cha uzuri cha wanawake.
Badala ya kuhangaika kujinyima chakula, kujichubua, kujikandika vipodozi lukuki au kujiumiza kwa njia nyingine, njia rahisi ni kutabasamu tu, haigharimu, jaribu uone. Kumbuka hata hivyo kwamba, kutabasamu siyo kuchekacheka.
Hata kama umzuri vipi, mambo hayaishii hapo kwamba unakuwa tayari umejenga uhusiano, la hasha tabasamu na tabia pia vinachangia………………………
Kaka Mtambuzi, sidhani kama nina la kuongezea hapa. Aksante sana. Ninajiamini na kujithaminisha kwa mpenzi wangu. Najua amenipenda mimi kama nilivyo, sihitaji kutamani maumbile ya mwanamke mwingine ili kumridhisha kwani angekuwa hajaridhika angekwenda kwa hao wenye maumbile hayo.
 
Na sisi ambao huwataka wapenzi wetu wanenepe?
Tunawapa hofu au tunafurahisha?kunenepa ni easy naona...
 
sijasema awe mnene but asifanye diet ya kujikondesha
ajiachie tu ,ajae jae hivi lol

Ohooo samahani sikuwa nimekupata vizuri nilidhani unataka kama ni mwembamba basi anenepe loh. But of coz kuna vitu ambavyo wanawake wengine hujisikia tu kuviweka sawa, mfano kiuno........Mimi ninenepe sina shida ilimradi tu 'kiwepo'. lol
 
ohooo samahani sikuwa nimekupata vizuri nilidhani unataka kama ni mwembamba basi anenepe loh. But of coz kuna vitu ambavyo wanawake wengine hujisikia tu kuviweka sawa, mfano kiuno........mimi ninenepe sina shida ilimradi tu 'kiwepo'. Lol

sijui kama nimekuelewa lol
 
Back
Top Bottom