Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,921
- 30,266
HOFU HII INASABABISHWA NA NINI KWANINI HAIKUWAPO WAKATI WA KUPIGANIA UHURU WA TANGANYIKA?
KUSUPA HAPENDEZEWI NA KUSEMA KUWA CHIEF MKWAWA ALIKUWA MUISLAM ANASEMA:
‘’MOHAMED SAID USICHEZE NA HISTORIA YA WAHEHE, WAPO WANAOIJUA VILIVYO!
ETI MKWAWA AJIITE ABDALLAH? HIVI KWELI WEWE UNAMJUA MKWAVINYIKA?
Mohamed Said naandika haya baada ya kuisoma post yako kuhusu Abdallah Mkwawa, nami nina machache ya kukwambia;
1. Tumekunyamazia unapotoa maandishi yako juu ya historia ya TANU na mwelekeo wako wa kutaka kuwaaminisha (wanaokuamini) kwamba TANU kilikuwa chama cha Waislamu, kilianzishwa na Waislamu, kiliiamarishwa na Waislamu…’’
Jibu langu kwake Bwana Kusupa:
''Ndugu yangu Kusupa umehamaki sana.
Najua kwa nini umehamaki na kwa mbali katikati ya mistari unajaribu kunitisha.
Hayo yote niliyoandika nimeyapata Mkwawa Museum Kalenga.
Si kama mie naandika bila ushahidi.
Yuko mtaalamu wa historia ya Mkwawa hapo makumbusho unaweza ukamuuliza.
Nilimuuliza kuhusu Mkwawa kuwa Muislam.
Akaniambia ni kweli.
Nikamuuliza aliupataje?
Akamtaja Abushiri bin Salim Suriyama kutoka Pangani.
Nikamuuliza jina lake la Kiislam.
Akaniambia ni Abdul.
Nikamsahihisha nikamwambia ni Abdallah.
Sithubutu hata kidogo kucheza na historia ya Wahehe wala na ya yeyote awaye yule.
Ikiwa kuandika yale yaliyoandikwa Mkwawa Museum ni "kucheza," basi wanaochezea historia hiyo si mie bali ni wenyewe wenye dhamana ya kuhifadhi historia hii.
Angalia hapo chini imeandikwa Abushiri asili yake ni Tanga.
Ukweli ni kuwa Abushiri ni Mzanzibari na ndiye aliyemfunza Mkwawa kuandika na kusoma kwa hati za Kiarabu.
Barua hii aliyoandika Mtwa Abdallah Mkwawa kwa mkono wake ipo Mkwawa Museum.
Hapo chini inaonyeshwa barua aliyoandikwa na Mtwa Abdallah Mkwawa.
Ndugu zangu haya ndiyo niiyoyakuta Mkwawa Museum Kalenga nikayaandika na haya ndugu zangu ndiyo yaliyomghadhibisha
Bwana Kusupa na kunionya mimi nisicheze na historia ya Wahehe kama ilivyo huko juu.
Huu uoga wa majina ya Kiislam nini maana yake?
Huyo hapo juu chini jina wanalolipenda wanahistoria wetu ni Songea Mbano ingawa ukweli jina lake ni Abdulrauf Songea Mbano.
Ukieleza kuwa hilo jina mnalomwita la Songea Mbano mnalikatiza jina lake ni Abdulrauf Songea Mbano kuna watu wanaghadhibika hawalitaki jina hilo.
Halikadhalika Mkomanile jina lake ni Khadija Mkomanile lakini jina la Khadija hawalipendi.
Kote katika historia ya Vita Vya Maji Maji mashujaa hawa hawatambulishwi kwa majina yao kamili ya Kiislam.
Hii nini maana yake?