Hizi taarifa za ndege kushindwa kutua Dodoma kutokana na Taa inalenga kuieleza nini Dunia? Hakuna tender inatengenezewa mazingira?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
877
4,106
Ndege inapoondoka Dar es Salaam inajulikana for sure itatua Dodoma muda gani na miundombinu ya uwanja inajulikana.

Lakini Kwa tuliosoma Cuba tunaposikia ndege ya Yanga yashindwa kutua, ndege ya kiongozi mkubwa yashindwa kutua lakini ndege zenye abiria wasio na attention Kwa jamii hazikwami kushuka tunajiuliza maswali mengi. Baadhi ya maswali

1. Je, hakuna MTU anataka kuhujumu juhudi za Mhe. Rais baada ya kuonekana ikulu imekamilika Kwa asilimia Mia moja? Ionekane Dodoma hakuna kiwanja cha kuaminika cha kutua ili wakubwa waendelee kuishi Dar?

2. Au labda yupo kiumbe anawaza kuwatangazia wageni kwamba Dodoma siyo sehemu salama? Kwa lengo gani?

3. Au labda yupo MTU amenusa tender yakutengeneza uwanja wa Dodoma so anaanza kuwatisha viongozi ili file la tenda lipitishwe. Tukumbuke Mkakati WA serikali siyo kukarabati uwanja uliopo Bali kujenga uwanja wa msalato.

4. Waziri mwenye dhamana amekosa nguvu yakusimamia sekta anatakiwa aondolewe ofisini? Kwamba anahijumiwa?

5. Au labda uzembe tu kama ulivyo uzembe WA Watanzania waliozoea kutumbuliwa?

Uwanja hauna Taa na unawasha ndege kwenda kutua ukijua wazi uwez kutua? Tunacheza na uhai.
 
Uwanja hauna Taa na unawasha ndege kwenda kutua ukijua wazi uwez kutua? Tunacheza na uhai
Kwa kweli hapa tunachezewa shere.

Yaani ni kama walikuwa wanasafiri kwa kubahatisha vile, yaani kama hawaujui uwanja upoje. Sasa hilo la kuweka Taa uwanjani si linaweza kuingia kama maboresho tu ya uwanja. Uwanja si tayari una bajeti ya matengenezo, inatumika kutengeneza nini??

Wasitupotezee muda kuweka habari za taharuki. Meneja wa uwanja ana fungu la matengenezo, atumie pesa hiyo kuweka hizo taa.
 
Eti kukwamisha juhudi, Yani mlishakua kama wajinga furani, Kila kitu ni kukwamisha juhudi,
 
Dodoma wengi hawapapendi sema wamelazimishwa tu na uharaka wa kuhamia haupo ni makosa aliyafanya JPM. Angalia balozi zote ziko Dar na sijui kama wanahamia Dodoma! Shule nzuri, hospitali nzuri, hali ya hewa safi ni Dar! Ndo ukweli!
 
Ndege inapoondoka Dsm inajulikana for sure itatua Dodoma muda gani na miundombinu ya uwanja inajulikana.

Lakini Kwa tuliosoma Cuba tunaposikia ndege ya Yanga yashindwa kutua, ndege ya kiongozi mkubwa yashindwa kutua lakini ndege zenye abiria wasio na attention Kwa jamii hazikwami kushuka tunajiuliza maswali mengi. Baadhi ya maswali

1. Je, hakuna MTU anataka kuhujumu juhudi za Mhe. Rais baada ya kuonekana ikulu imekamilika Kwa asilimia Mia moja? Ionekane Dodoma hakuna kiwanja cha kuaminika cha kutua ili wakubwa waendelee kuishi Dar?

2. Au labda yupo kiumbe anawaza kuwatangazia wageni kwamba Dodoma siyo sehemu salama? Kwa lengo gani?

3. Au labda yupo MTU amenusa tender yakutengeneza uwanja wa Dodoma so anaanza kuwatisha viongozi ili file la tenda lipitishwe. Tukumbuke Mkakati WA serikali siyo kukarabati uwanja uliopo Bali kujenga uwanja wa msalato.

4. Waziri mwenye dhamana amekosa nguvu yakusimamia sekta anatakiwa aondolewe ofisini? Kwamba anahijumiwa?

5. Au labda uzembe Tu kama ulivyo uzembe WA Watanzania waliozoea kutumbuliwa?

Uwanja hauna Taa na unawasha ndege kwenda kutua ukijua wazi uwez kutua? Tunacheza na uhai.
Tunashinikiza turuhusiwe kununua taa zingine.
 
Makamu wa Rais alishindwa kutua akitoka Burundi juzi ikabidi aje DSM na asubuhi arudi Dodoma kumuwakilisha mh Rais Samia Kwenye Ibada ya kumsimika Askofu wa KKKT
 
Hakuna kujifunza kutokana na ile ajali ilyotokea Bukoba na kusababisha mauti

CCM wanajua kuiba tu hawana huruma na Nchi

Tujiapize kuwa 2025 cha moto wakione.
 
Hakuna kujifunza kutokana na ile ajali ilyotokea Bukoba na kusababisha mauti

CCM wanajua kuiba tu hawana huruma na Nchi

Tujiapize kuwa 2025 cha moto wakione.
Baada ya 2025 akili zako halisi zitakapokurudia ndio utajua CCM ni dubwasha lenye mipango ya kutawala daima. Muda huu nakupa nafasi ya kujipa matumaini hewa lakini 2025 na kuendelea ndio ukweli utaanza kuwaingia.

Kimsingia huwa natazama mambo kwa jicho la tatu na hapa ndipo kwenye ukweli mchungu. Ni miaka 30 ambao ni umri wa vyama vya siasa vilivyopo lakini cha kushangaza CHADEMA hakina ofisi na hili la kutokuwa ofisi ndio linawatesa na kuamini kukimbizana barabarani ndio siasa, wajenge ofisi waone kama watakimbizana barabarani.

Hicho Cha kutokezo ni kidokezo tu lakini kwa ufahamu na akili za kawaida ni kweli CHADEMA itaweza kuijenga Tanzania ikiwa wanashindwa kupajenga kwao?
 
Baada ya 2025 akili zako halisi zitakapokurudia ndio utajua CCM ni dubwasha lenye mipango ya kutawala daima. Muda huu nakupa nafasi ya kujipa matumaini hewa lakini 2025 na kuendelea ndio ukweli utaanza kuwaingia.
Kama Uchaguzi utakuwa HURU na wa HAKI ayeyaa!!! ayeyaa!!

Naisevu hii meseji.
 
Mimi ndio nitakuwa mtu wa mwisho kuamini CCM imeshindwa na CHADEMA
Mimi hii Tanzania naizunguka sana watu wameuchoka CCM ngoja tuone Kinana atakuja na mbinu gani zaidi ya kutumia Dola ili kubakia madarakani.
 
Back
Top Bottom