ymollel
JF-Expert Member
- Aug 23, 2012
- 3,095
- 2,294
tatizo sio chip ya MTK, inawezekana simu ikawa na chip hizo zingine na ikawa hovyo pia. Zipo simu nzuri za MTK na zipo za hovyo vile vile kama ulivyosema tatizo ni umasikini inamaanisha MTK za bei chee ni mbovu. ukinunua simu kama Tecno S1 au Y2 utajuta bora kununua kitochi. Lakini kuna simu za mtk Kama nokia 5.1 na Motorola e4 sio simu za kubeza.
Heshima kwenu wakuu.Nisipoteze muda napenda kuleta mrejesho kuhusu hizi simu zinazouzwa Kwa bei ya promosheni ni kisanga baada ya simu yangu kuleta shida ya display nikairudisha kwao Tigoshop wakagoma kunibadilishia ingawa ilikuwa ndani ya warrant nikasema fresh tatizo umaskini. Yote kwa yote kwa sasa mara ionyeshe majina mara yasionekane nikaamua kumpa wife aiburuze maana yeye haangalii ubora wa simu shikamoo mchina.