BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,376
- 8,118
Simu ni Kifaa muhimu cha mawasiliano kwa binadamu yeyote lakini haitakiwi kuwa sehemu ya mwili wako kiasi cha kukufanya uwe kama mtumwa kifaa hicho.
Wataalaamu wa Saikolojia wanasema, ukitaka kubaini kama umepata Uraibu (Addiction) ya matumizi ya Simu, anza kuangalia ni kwa muda gani unaweza kukaa bila kushika Simu yako hasa muda ambao uko peke yako bila shughuli nyingine.
Inashauriwa ukibaini umepata Uraibu wa Simu, anza taratibu kwa kujizuia kwa kupunguza matumizi yake ambapo unaweza kuweka muda maalumu 'Time Limit' kwenye 'App' unazozipenda zaidi mfano, Instagram, Twitter, TikTok n.k. ziwe zinajifunga kila baada ya dakika kadhaa.
Vipi Mdau, umeweka Tiki kwenye dalili ngapi hapo?