Ukiona dalili hizi, mwenzako ana mchepuko

Job Richard

JF-Expert Member
Feb 8, 2013
3,865
2,176
KILA mmoja atakubaliana na mimi kwamba mahusiano baina ya wapendanao kwa kawaida yanakusudia kuwa ya upendo, maelewano, kuaminiana na urafiki wa hali ya juu ingawa hali halisi siyo hiyo katika uhusiano wa wengi. Wengi wetu wameumizwa kwa mapenzi hasa kutokana na tatizo la uaminifu katika mahusiano yao.

Zifuatazo ni dalili zitakazokusaidia kuwa macho mara utakapoona mazingira ya kufanana nazo yanatokea katika uhusiano wenu.

KUPENDA KUTEMBEA NA MIPIRA YA KINGA
Ukiona mpenzi wako ana tabia ya kubeba kondomu kwenye pochi yake au mfukoni kwa kisingizio kuwa anajali, elewa kwamba yuko katika mahusiano na mtu mwingine.

UTATANISHI KATIKA MATUMIZI YA SIMU
Ukiona simu zinamiminika mpaka usiku wa manane naye anapokea kwa siri. Yamkini pia alikuwa yuko huru hata simu yake inapolia waweza ukaichukua na kumpatia lakini ghafla anakuwa na hofu kubwa na kuificha simu yake, au anakwenda na simu hadi bafuni isije ikasikika juwa kuna jambo.

Wengine wanaondoa milio katika simu zao wakati haikuwa kawaida yao, kuweka nenosiri (password) ngumu hadi mwenyewe anashindwa kuikumbuka, wako ambao simu zao zikipigwa hawawezi kupokea na kuongea kwa uhuru kama kawaida, ataondoka na kujitenga pembeni akijifanya anaongea kiuaminifu kabisa.

HARUFU MPYA KWAKO

Kwa kuwa wapendanao huwa wamezoeana, mara nyingi hata aina ya manukato mmoja anayotumia yanakuwa yanajulikana kwa mwenzake, sasa fikiri unamkuta mpenzi wako ana harufu ya tofauti kabisa na uliyoizoea, umeisikia harufu hiyo akiwa amerudi toka kazini wakati asubuhi alipoondoka alikuwa na harufu ile uliyoizoea, elewa kwamba kuna jambo!

MABADILIKO FARAGHANI
Jambo hili linaweza kujidhihirisha katika picha mbili tofauti. Kwa kawaida wapenzi huwa na mazoea fulani katika tendo la ndoa, kwa muda waliokaa pamoja kila mmoja humfahamu mwenzake kwa kiasi fulani. Inawezekana likawa jambo la kushangaza pale ambapo ghafla unamuona mpenzi wako anapoteza kabisa hamu ya tendo la ndoa, au hata mnapokuwa katika tendo hilo humuoni akifurahia bali anakuwa kama anayelazimishwa au kutohamasishwa na chochote, hapo elewa kwamba huyo ana mchepuko.

KUJIPENDA KUPITA KIASI
Yawezekana mpenzi wako alikuwa amezoea kuvaa kawaida, hapa simaanishi kutopendeza na wewe ulikuwa umemzoea katika hali fulani ya mavazi au mitindo mara ghafla anabadilika na kuwa mtanashati zaidi ana badilisha mavazi, anapenda mavazi ya gharama, labda alikuwa hatumii manukato lakini ghafla anaanza kupenda manukato, anajijali zaidi ya kawaida yake kiasi ambacho hukumzoea na kutoka mara kwa mara. Katika hali hii jaribu kuwa macho zaidi kufahamu nini kilicho sababisha mabadiliko hayo.

KUCHELEWA KURUDI KAZINI
Sio kwamba kila mtu anapochelewa kurudi kazini basi anakuwa sio mwaminifu, lakini zaidi ya asilimia 75 (kutoka kwenye tafiti) ya ambao wamekuwa na mahusiano nje wamekuwa wakitoa visingizio vinavyohusiana na kazi, vikao, mikutano na safari za kikazi, yamkini wewe ni shahidi wa hili.

MARAFIKI WAKE KUKUKWEPA
Inabidi ujiulize sana pale inapotokea ghafla wale marafiki wa mpenzi wako uliowazoea, uliokuwa unawapigia simu wakati wowote leo wanakukwepa na hata simu hawapokei na mara nyingine wakipokea hawakupi taarifa yakueleweka au wanakudanganya. Hii yote inawezekana wanamlinda rafiki yao, au wanakosa cha kujibu maana wanajua uhalisia wa kinachoendelea.

MAELEZO YA KUTATANISHA
Unaweza kukuta katika mapenzi yenu mpenzi wako anaanza kuwa na sentensi ngumu na zisizo kuwa na msingi kwa mfano anasema “kwa jinsi hii sidhani kama tutafika” “mimi siamini kama mapenzi yatadumu” “yani ndio maana watu wanashindwa kukaa na mpenzi mmoja” na mara nyingine anaweza kukuuliza baadhi ya maswali moja kwa moja ili kukuona utajibuje. Sentensi hizi zina chanzo moyoni, kuwa macho.

KUFICHA FEDHA
Hii utaiona ghafla mpenzi wako anaanza kuwa na siri kuhusu fedha zake au matumizi yake, na wala hapendi kuulizwaulizwa kuhusu suala hilo. Tabia hii ikidhihirika katika mapenzi yenu usichelewe kuchunguza maana kwa kukaa kimya unaweza kujikuta umechelewa, yaani mwenzio tayari ana mtu mwingine.
 
TZ ya vi-wonder......

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Kwenye kupoteza hamu ya tendo sababu sio tu mchepuko
Mtu anaweza akawa na stress au depression,kwa wanawake post partum period pia inaweza kuondoa hamu ya tendo kabisa,sasa badala uwe faraja na umsaidie unaongeza tatizo kwa kuhisi anachepuka!
 
Usisahau na Kununa nuna hovyo, tena bila sababu ya msingi...
Ila vina muda basi, wataachana tu.....

tena dawa ya mpenzi mwenye mchepuko ni kumuacha kama alivyo, punguza shobo kwake, akinuna wewe tabasamu, usimjali.....hii itapelekea zile tabia zake mbaya azionyeshe huko mchepukoni Ili wakinaiane mapema.
 
Back
Top Bottom