Dada;
Watakuambia mengi ila nataka ujitulize uhakikishe kuwa ndoto zako hukujia siku gani, umekula nini, na kwenye shughuli zako kulikuwaje?
Maswali haya huweza kukuelekeza chanzo cha ndoto na mwisho maana yake. Mara nyingi huwa unapenda saana kula chips, na hizi huleteleza ndoto, au ugali wa kabichi na viazi kwa mbali. Ukiota ndoto siku ulizotumia vitu hivyo zipuuzie tu.
Kama hukutumia vitu hivyo na kwenye shughuli kulikua sio heka heka, zitafakari ndoto hizo. Nazo ni kuwa:
Una idea nzuri saana kichwani, lakini mvivu kuitendea kazi. Siku ukiitendea kazi, utapata mafanikio makuu. Lakini, umekuwa ukijiona ka usiyefaa kulifanya uwazalo. Amka, tendea kazi wazo lako kwani ni njia ya kutokea.
Kama uliwahi kumwelezea mtu flani wazo, akalifanyia kazi uliona alichofanya. Badala ya kujua kuwa weye ndiye chanzo cha mafanikio hayo, ukaona ni mwingine. Ukabaki jiuliza, mbona sifikii??
Acha kujidharau kwani una uwezo mkuubwa sana na nyota yako inakuhimiza kuamka na kufanya.
Maana ya pili:
Je, kwa nini wazazi wako hawako pamoja?? Weye kwa nini unatamani kwenda kwa babako zaidi? Angalia, kilichomfanya babako asiishi na mamako kwani kimeondoka?? Atakuzimia nyota yako soon.