Hizi kero maofisini usiombe

unapanishwa cheo leokesho unakuta nazi na unga unga mlangoni lol
Duh! umenikumbusha tukio moja huko Kasulu, kuna jamaa alipata post ya juu maana elimu yake ilikuwa ya juu, basi wale wa chini yake walimfanyia vitimbi, waliotesha kichuguu ofisini kwake kabisaa! Jamaa aliacha kazi hapohapo akajitimua zake!
 
Mm nakerwa na hawa mabosi unahitaji huduma anakuja mtu anamwongelesha na anajua ww unamsubiri akitoka hapo bosi anasema siuhisiki na hili.
 
inakera zaidi kuna mjadala umekolea jukwaa la siasa (mfano ule wa juzi kujivua gamba kwa RA) mara ghafla anakuja kabacholi na kazi yake halafu kavuta kiti pembeni aone unavyomchorea ramani, itabidi u'minimise window ya JF, looh!
 
Kero yangu leo:
Nimenunua maandazi yangu mawili kabla sijaja ofisini ili niyanywe na chai.
Muda ulipofika nashangaa naletewa donut, kiazi kitamu na ndizi mbivu!
Yani mpaka nimeshindwa kula maandazi yangu....aaaargh!
 
Kero yangu leo:
Nimenunua maandazi yangu mawili kabla sijaja ofisini ili niyanywe na chai.
Muda ulipofika nashangaa naletewa donut, kiazi kitamu na ndizi mbivu!
Yani mpaka nimeshindwa kula maandazi yangu....aaaargh!

Duh! Hii kali mkuu!
 
Duh! umenikumbusha tukio moja huko Kasulu, kuna jamaa alipata post ya juu maana elimu yake ilikuwa ya juu, basi wale wa chini yake walimfanyia vitimbi, waliotesha kichuguu ofisini kwake kabisaa! Jamaa aliacha kazi hapohapo akajitimua zake!
Hawa ndio wanaorudisha maendeleo nyuma!
 
unakuta kuna mshkaji ofcn anakuzimikia,so kila saa anataka kuja mezani kwako! ananuka kikwapa ama mdomo,kumuambia huwezi na yy haji-express ili umtupe kule mkae mbali! taabu kweli!ama unakuta mna ofc useless kweli,disorganised!sasa ukikutana na client unaona aibu jinsi mnavyokuwa unproffessional!(ofc za gvt inahuu sana hii)
khaaa! Hakika híi ni kero kubwa kuliko.
 
Wahindi bana wanatuma sana watu, eti ukamtengenezee chai na anakwambia hivi; "Veve nitorogee(nikorogee) chai sasa wivi(hivi) bana" huku professional yako ni Accountant!
 
hizo zote sio kero

kero ni hizi..

1.ofisi inajua wewe ni addicts wa internet unakuta ki memo
kuanzia leo marufuku kuingia mitandao mingine isiyo ya kiofisi....

2.net kwako iko slow,unamuita administrator anakudengulia..
kisa anatembea na bosi wa head office

3.unaingia ofisini unakuta kuna ma trainee wanawake wapya
walivyovaa utasema wanatangaza biashara

4.unafika ofisini,unakuta kuna mabadiliko,
umekewa pc nyingine ya zamani na software za zamani...
unauliza unaambiwa ile nyingine inafanyiwa service
ikirudi wamefuta kila kitu...

5.kuna mgao wa umeme na ofisi haina bajeti ya genereta

6.kuna mgao wa umeme na genereta la ofisi lipo dirishani kwako

Hahahahaha...hapo kwenye red....ukitoka hapo jion ukiwa umelala unahisi kama genereta bado linanguruma
 
KUNA WALE AMBAO SHUGHURI YAO KUBWA NI KUANGALIA NANI HAKWENDA luch LEO.................... Aaaaaaaaaaafffuuuuuuuuuu wanakagua hayo huku wakijua muda huo ni tarehe kati ya 13 ta 21 ya mwezi.......... YAANI WANANIBOA ............we acha tu
 
Hii bomu boss, maana sijui ulikua umechacha au unasave mahela!! Bomba kweli!
 
Kubwa zaidi usiombe ukutane na mtu ambaye huwa hana lugha nzuri hata ukimpa utani mdogo wa kawaida anapayuka na atakwamba "Mse**e wewe!!" Hapo ni asubuhi unajikuta siku yako nzima imechafuka na ofisi unaiona chungu mno kisa mtu mmoja tu!
 
hEHEH...ya leo kali!
Naenda kupaki gari la mfanyakazi mwenzangu..nakuta kuna nafasi moja tu imebaki!
Nimeshaanza kufurahia vile najiandaa kuingia (ndo nimepiga indicator), naangalia nyuma namwona boss wangu nyuma naye anataka kuingia hapohapo..duh!
Na amekunja sura na yeye amepiga indicator vilevile..
Ingekuwa we ungefanyaje?
 
hEHEH...ya leo kali!Naenda kupaki gari la mfanyakazi mwenzangu..nakuta kuna nafasi moja tu imebaki!Nimeshaanza kufurahia vile najiandaa kuingia (ndo nimepiga indicator), naangalia nyuma namwona boss wangu nyuma naye anataka kuingia hapohapo..duh!Na amekunja sura na yeye amepiga indicator vilevile..Ingekuwa we ungefanyaje?
Naingia tu hivyo hivyo najifanya sijamwona! Kila mtu ana shida bana!
 
Naingia tu hivyo hivyo najifanya sijamwona! Kila mtu ana shida bana!


Haha..haya bwana! ilibidi nimwachie nikapaki nje!
ila ndo kero hizo..and naamini wewe mwenyewe ingekukuta hiyo usingefanya ivo ulivosema!
 
Back
Top Bottom