Mungu hakumwumba mwanadamu kuwa dhaifu isipokuwa wanadamu tunaozaliwa leo tunazaliwa katika dunia ambayo imeshaathirika na matokeo ya uasi.
Mfano; Biblia inasema baada ya Mungu kuumba kila kitu akatazama na kuona kila kitu kuwa ni chema sana. Mwanzo 1:31.
Hata kuna wakati Mungu aliwahi kumwita Ayubu kuwa ni mtu mkamilifu. Kwa hiyo kusema kwamba wanadamu wote ni dhaifu au hakuna mkamilifu sio sawa labda kama unajilinganisha na Malaika ambao waliumbwa tofauti na wanadamu
Ayubu 1:8
Kisha Bwana akamwuliza Shetani, Je! Umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mwelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu.
Mungu hakumwumba mwanadamu kuwa roboti bali alimwumba awe mtu mwenye maamuzi. Kwa sababu Mungu alitaka kuwe na mahusiano ya upendo kati yake na mwanadamu aliyemwumba ndo maana ilibidi kumpa uhuru kamili wa kuamua kumpenda Mungu au kutompenda.
Mungu asingeweza kujisikia kupendwa na mwanadamu ambaye hana utashi wake binafsi yani kama tungeumbwa as programmed creatures. Ukweli ya kwamba tuna uwezo wa kuamua kumtii au kutomtii Mungu ni udhihirisho tosha kuwa Mungu alituachia uhuru mkubwa ili Upendo utakaooneshwa kutoka kwetu Kwenda kwake uwe Upendo halisi.
Mungu hachoki. Isaya 40:28 “Je! Wewe hukujua? Hukusikia? Yeye Mungu wa milele, Bwana, Muumba miisho ya dunia, hazimii, wala hachoki; akili zake hazichunguziki.”
Biblia inaposema Mungu alistarehe siku ya saba haina maana kuwa alichoka, ni lugha ya picha kuonesha kazi maalum ya Uumbaji aliikamilisha na aliacha kufanya uumbaji, lakini sio kwamba alikuwa amechoka na wala sio kwamba aliacha kufanya kazi kabisa.
Mwanzo 2:2
"Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya."
Mwanzo 2:3
"Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya."
Yohana 5:17
"Akawajibu, Baba yangu anatenda kazi hata sasa, nami ninatenda kazi."
Sina majibu ya kila swali ulilouliza lakini nadhani nitakuwa nimesaidia kupunguza mzigo wa maswali yako