Infropreneur
JF-Expert Member
- Aug 15, 2022
- 14,178
- 30,662
Nakazia.Upo sahihi Mungu na Shetani wanategemeana kama Simba na Yanga
Mungu na shetani wote ni character wa kutungwa. Fictional characters, hawajawai kuwepo
Nakazia.Upo sahihi Mungu na Shetani wanategemeana kama Simba na Yanga
Mungu na shetani wote ni character wa kutungwa. Fictional characters, hawajawai kuwepo
Kama Mungu huyo aliumba kila kitu kwa ukamilifu.Nadhani Haya mambo yanahitaji level flani ya mambo ya kiimani zaidi
MUNGU aliumba kwa ukamilifu, lakini Kuna mifumo/systems alitengeneza ili vyote vikafanyike kwa hiyo. Bila uhuru upendo ni batili, vyote vifanyikavyo sio kwa kupenda/kutokupenda bali kwa kufuata na kuheshimu mifumo aliyoiweka humo. Ni ngumu kuelezea jambo zito linalohitaji sio tu ufahamu wa kawaida bali zaidi ya hapo.
Long story short: Mungu ni Dhahiri na vyote vifanyikavyo ni thabiti kwa kufuwata sheria na mifumo iliyoandaliwa.
Dunia yenye uasi iliwezaje kuwepo kwa Mungu mwenye kujua yote tangu mwanzo na hata milele?Mungu hakumwumba mwanadamu kuwa dhaifu isipokuwa wanadamu tunaozaliwa leo tunazaliwa katika dunia ambayo imeshaathirika na matokeo ya uasi.
Mfano; Biblia inasema baada ya Mungu kuumba kila kitu akatazama na kuona kila kitu kuwa ni chema sana. Mwanzo 1:31.
Hata kuna wakati Mungu aliwahi kumwita Ayubu kuwa ni mtu mkamilifu. Kwa hiyo kusema kwamba wanadamu wote ni dhaifu au hakuna mkamilifu sio sawa labda kama unajilinganisha na Malaika ambao waliumbwa tofauti na wanadamu
Ayubu 1:8
Kisha Bwana akamwuliza Shetani, Je! Umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mwelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu.
Mungu hakumwumba mwanadamu kuwa roboti bali alimwumba awe mtu mwenye maamuzi. Kwa sababu Mungu alitaka kuwe na mahusiano ya upendo kati yake na mwanadamu aliyemwumba ndo maana ilibidi kumpa uhuru kamili wa kuamua kumpenda Mungu au kutompenda.
Mungu asingeweza kujisikia kupendwa na mwanadamu ambaye hana utashi wake binafsi yani kama tungeumbwa as programmed creatures. Ukweli ya kwamba tuna uwezo wa kuamua kumtii au kutomtii Mungu ni udhihirisho tosha kuwa Mungu alituachia uhuru mkubwa ili Upendo utakaooneshwa kutoka kwetu Kwenda kwake uwe Upendo halisi.
Mungu hachoki. Isaya 40:28 “Je! Wewe hukujua? Hukusikia? Yeye Mungu wa milele, Bwana, Muumba miisho ya dunia, hazimii, wala hachoki; akili zake hazichunguziki.”
Biblia inaposema Mungu alistarehe siku ya saba haina maana kuwa alichoka, ni lugha ya picha kuonesha kazi maalum ya Uumbaji aliikamilisha na aliacha kufanya uumbaji, lakini sio kwamba alikuwa amechoka na wala sio kwamba aliacha kufanya kazi kabisa.
Mwanzo 2:2
"Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya."
Mwanzo 2:3
"Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya."
Yohana 5:17
"Akawajibu, Baba yangu anatenda kazi hata sasa, nami ninatenda kazi."
Sina majibu ya kila swali ulilouliza lakini nadhani nitakuwa nimesaidia kupunguza mzigo wa maswali yako
Lakini hapo hapo uwezekano wa Mungu kuwazuia hao wanadamu wasimuue yesu!Waliomuua ni wanaadamu
Aliruhusu kwa sababu ilikuwa ni sadaka ya kuwakomboa wengineLakini hapo hapo uwezekano wa Mungu kuwazuia hao wanadamu wasimuue yesu!
Ulisema kitu kimoja hakiwezi kuwa na maelezo tofauti, nimetoa mfano wa Rais Samia kuonyesha kuwa kunaweza kuwa na maelezo tofauti ila anayekusudiwa ni mmoja ndio maana hata kama hayo maelezo yanaji contradict bado hatuwezi kuhitimisha kwa kusema Rais Samia hayupo.Mungu hawezi kua sawa na Samia. Samia kila mtu atamuongelea jinsi anavyomjua, anavyofaidika na yeye na mambo kama hayo. Pia mtu anaemjua Samia utotoni atamuongelea tofauti na Samia na mtu mwigine aliemjua ukubwani, mume wake atamuongelea tofauti na watoto wake, ndugu zake wa damu watamuongelea tofauti na rafiki zake.
Tunapozungumzia Mungu tunaongelea kitu tofauti, hatutegemei kiwe na maelezo tofauti ya kubadilika badilika kulingana na wakati . Umesahau Biblia inasema Mungu ni yule yule jana , leo na hata milele? Mungu ni yule yule asie badilika? Soma biblia.
Sasa kama Mungu ni yule yule jana , leo na hata milele, hawezi kua na maelezo tofauti tofauti, atakua ni yule yule siku zote.
Kwa msingi huo Mungu anaetajwa kwenye dini hayupo.
Kama anaona watu hawajui wanampata vipi kwanini ajifiche? Kwaninis asijidhirishe basi hata kwa njia yoyote ile ili watu wamuamini? Basi alete hao manabii wake kama wale tuliosimuliwa na vitabu?Mim nachoweza kusema hatujui njia ya kumfikia Mungu ili ajibu maombi yetu manake mambo yanavyoenda ni vice versa kbsa Yani Kuna wakati kama maombi hayajibiwi japo majaribu ni sehem ya maisha yetu
Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
Wacha upuuzi wewe itakuwa hujui hata historia za dini, kabla ya kuundwa hizi takataka ziitwazo dini watu waliishi kwa amani bila mitengano ya kijinga, vita vya kijinga kisa utofauti wa imani, alafu hizi dini ndizo zimeleta machafuko na tabia za kishenzi.Dini hazina magumu ila ni binaadamu ndio anajichanganya mwenyewe na kuvuruga.
Dini ni kumfanya binaadamu aishi na wenzake kwa wema na amani na kutii amri za Mungu ambazo wote tunakubaliana nazo.
Huitaji kuwa na dini ili ufanye mema na kuwa na imani.Dini hazina magumu ila ni binaadamu ndio anajichanganya mwenyewe na kuvuruga.
Dini ni kumfanya binaadamu aishi na wenzake kwa wema na amani na kutii amri za Mungu ambazo wote tunakubaliana nazo.
Naunga mkono hoja, ila sina imani saana na dini. Nachojua hata babu zangu waliabudu hata kabla ya kuletewa imani za kigeni.. maana walijua ipo nguvu kuliko was, almost jamii zote duniani ziliabudu kwa namna tofauti tofauti..[emoji16][emoji16][emoji16]siwezi nikajifanya sielewi ,na hapa ndo chimbuko LA maswali hayo kwenye post , pia labda inawezekana mpaka Sasa kizazi cha Leo hatujajua Mungu anafikiwaje,japo binafsi naamini Mungu yupo ila usije sema nithibitishe ,siwezi kuthibitisha ila naamini Mungu yupo
Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
Labda pengine tunamtafuta mahali asipokuwepo, ama tumemuacha mbali sana! Maana kuna mafundisho ukiyasikiliza, mpaka umpate ni zaidi ya ngamia kupenya kwenye tundu la sindano... anyway sitaki kukufuru, moto sio mzuri.Halafu jingine, amenyamaza kimya kama vile hayupo.
Wananzengo wanatumia huo mwanya kuwapiga hela wanaomtafuta.
Kuna pahala nimewahi sikia kuwa 'yupo mkuu wa anga, kazi yake ni kuzuia maombi kwenda juu.. kuvuka hapa si kazi ndogo, binafsi sielewi kwanini awe na nguvu hivi..Mim nachoweza kusema hatujui njia ya kumfikia Mungu ili ajibu maombi yetu manake mambo yanavyoenda ni vice versa kbsa Yani Kuna wakati kama maombi hayajibiwi japo majaribu ni sehem ya maisha yetu
Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
Mkuu sijui kama unaelewa, nimekwambia kitu kimoja hakiwezi kua na maelezo tofauti halafu bado kikawa kitu kile kile.Ulisema kitu kimoja hakiwezi kuwa na maelezo tofauti, nimetoa mfano wa Rais Samia kuonyesha kuwa kunaweza kuwa na maelezo tofauti ila anayekusudiwa ni mmoja ndio maana hata kama hayo maelezo yanaji contradict bado hatuwezi kuhitimisha kwa kusema Rais Samia hayupo.
Kwa hiyo uwezo wa mwanadamu ni sawa na Mungu?Na hata huyo binadamu mwenyewe akitengeneza kitu chochote iwe mashine au chochote kile hakiwezi kua 100% perfect yaani coefficient of machine haiwezi kua 100% hata itoke kiwandani muda huu na chochote kile kingine mpaka vyakula, lazima kitakua na kasoro fulani
Unasomaga been biblia kweli wewe?!Waliomuua ni wanaadamu