Hizi ishu za Mungu/Dini ni very complicated

Hizi ishu za Mungu/Dini ni very complicated

Unajua mkuu unaweza ukaona wewe una point za msingi sana na mimi ukaniona situmii akili zangu sawa sawa ila huwa napenda kusema siku zote hii ni mitazamo tu ndio maana tunaona atheists kama wewe ambao wamekuja kuwa waumini wa dini na wanaamini Mungu wakati mwanzo walikuwa wanasema Mungu hakuna kwa sababu hakuna uthibitisho.
Ni kweli mkuu tunatofautiana kimtizamo. Baadhi ya atheists kuamini kuwa Mungu yupo ni sawa na muamini yeyote kuwa atheist hii haihalalishi uwepo au kutokuwepo kwa jambo. Mbona waamini wengi tu wamekuwa atheists baada ya kushtuka kuwa wanaabudu story zilizotungwa na binadamu wenzao?.

Mkuu watunzi wa vitabu vyenu vitakatifu washakufa ndio maana hakuna aya mpya zinazoshuka kutoka mbinguni ili kuendana na karne ya sasa.
 
Jibu langu ni Nadharia sio complete facts

Smallest block ya viumbe hai ni protein na baadhi ya Elements, na hizi zilitokea kwenye maeneo ya Dunia ambapo Geo biology activities zilikuwa active, sehemu nyingine kwenye Solar system yetu kuna hizo ni kwenye mwezi wa Saturn unaitwa Europa huwa kuna miamba inatoa mvuke au aina ya Kimiminika, but hadi sasa wachunguzi hawajaweza kuthibisha kama kuna any micro biology au any cellular life na itafananaje na hapa Duniani.

How life happens on Earth, Maji katika Kimiminika yalifikaje Duniani hakuna anayejua wala jibu sahihi, but yapo na tuna endelea kuenjoy
Hii Paragraph ya mwisho ndio ufafanuzi mzuri.

Hakuna anayejua na hakuna uthibitisho wowote ule wa kisayansi au kidini wa kuonyesha namna gani ulimwengu ulianza.

Ni nadharia na speculations tu ndivyo vilivyopo.
 
Ni kweli mkuu tunatofautiana kimtizamo. Baadhi ya atheists kuamini kuwa Mungu yupo ni sawa na muamini yeyote kuwa atheist hii haihalalishi uwepo au kutokuwepo kwa jambo. Mbona waamini wengi tu wamekuwa atheists baada ya kushtuka kuwa wanaabudu story zilizotungwa na binadamu wenzao?.

Mkuu watunzi wa vitabu vyenu vitakatifu washakufa ndio maana hakuna aya mpya zinazoshuka kutoka mbinguni ili kuendana na karne ya sasa.
Umesema vizuri kuwa tunatofautiana mitazamo kwa maana huo msimamo wako kuwa hakuna Mungu ni mtazamo tu ambao wengine walifikia kuachana nao na kuwa waamini Mungu.
 
Na hata huyo binadamu mwenyewe akitengeneza kitu chochote iwe mashine au chochote kile hakiwezi kua 100% perfect yaani coefficient of machine haiwezi kua 100% hata itoke kiwandani muda huu na chochote kile kingine mpaka vyakula, lazima kitakua na kasoro fulani
Huyo binadamu si muweza wa yote, si mjuzi wa yote kiasi kwamba akitengeneza chochote kikawa na kasoro alaumiwe.

Unapokuwa na Mungu mwenye sifa ya uwezo wote ujuzi wote na upendo wote halafu ukawa na ulimwengu wenye kuruhusu mabaya hapo unakuwa umejipinga.

"Mungu hayupo,
Nasema Mungu hayupo,
Kama Mungu huyo yupo kweli kwanini hajawahi kujionesha zaidi ya wahubiri kuhimiza imani tu na kujifanya kumuongelea kama wawakilishi wake!?
 
Hii Paragraph ya mwisho ndio ufafanuzi mzuri.

Hakuna anayejua na hakuna uthibitisho wowote ule wa kisayansi au kidini wa kuonyesha namna gani ulimwengu ulianza.

Ni nadharia na speculations tu ndivyo vilivyopo.
Kweli Kbsa hakuna uthibitisho
 
[emoji16][emoji16][emoji16]siwezi nikajifanya sielewi ,na hapa ndo chimbuko LA maswali hayo kwenye post , pia labda inawezekana mpaka Sasa kizazi cha Leo hatujajua Mungu anafikiwaje,japo binafsi naamini Mungu yupo ila usije sema nithibitishe ,siwezi kuthibitisha ila naamini Mungu yupo

Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
labda hata jina sio lake ndio maana hata tukimuita hajagi. huyo aliimba huu ulimwengu akaniumba namimi na kilakitu labda haitwi mungu maana siamini kilakitu
 
Halafu jingine, amenyamaza kimya kama vile hayupo.
Wananzengo wanatumia huo mwanya kuwapiga hela wanaomtafuta.
akamtoa mtoto wake wapekee kamafidia kwetu tukakombolewa toka kwenye zambi.! sasa najiulizaga sisi tulikua tunadaiwa nanani hadi yesu atolewe fidia kutulipia.? kingine kama alikufa kwaajili sisi tusamehewe zambi zetu mbon zambi bado zinaendelea haziishi.? au ata mtuma tena.?
 
Hata sasa mie nikiuliza Rais Samia huwa analalia shuka rangi gani laweza kuwa swali gumu pia?
wako watu wanajua. walau naweza kukwambia kamuulize fulani atakua anamajibu.! mfano naweza kubwambia bodyguard wake au mume wake. au mjukuu wake. ila hayo maswali kuhusu Imani sina hata wakumuuliza nikiuliza naambiwa nakosea sana nakufuru.!
 
kufa ni njia ya kumfikia mungu, hakuna njia nyingine ya short cut, ko ata wewe mungu anakulinda mpaka siku yako ikifika anakuchukua tu ata kama upo kitandani na anakuchukua kwa Nia njema tu! Lingine ukiwa mtenda maovu lazima uchukie kifo ila jaribu kuwa mwema kwa nguvu zako zote wiki Moja tu uone kama utaogopa kifo!
tukifa tunaenda kwa mungu.?
 
Mungu hakumwumba mwanadamu kuwa dhaifu isipokuwa wanadamu tunaozaliwa leo tunazaliwa katika dunia ambayo imeshaathirika na matokeo ya uasi.

Mfano; Biblia inasema baada ya Mungu kuumba kila kitu akatazama na kuona kila kitu kuwa ni chema sana. Mwanzo 1:31.

Hata kuna wakati Mungu aliwahi kumwita Ayubu kuwa ni mtu mkamilifu. Kwa hiyo kusema kwamba wanadamu wote ni dhaifu au hakuna mkamilifu sio sawa labda kama unajilinganisha na Malaika ambao waliumbwa tofauti na wanadamu

Ayubu 1:8
Kisha Bwana akamwuliza Shetani, Je! Umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mwelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu.

Mungu hakumwumba mwanadamu kuwa roboti bali alimwumba awe mtu mwenye maamuzi. Kwa sababu Mungu alitaka kuwe na mahusiano ya upendo kati yake na mwanadamu aliyemwumba ndo maana ilibidi kumpa uhuru kamili wa kuamua kumpenda Mungu au kutompenda.

Mungu asingeweza kujisikia kupendwa na mwanadamu ambaye hana utashi wake binafsi yani kama tungeumbwa as programmed creatures. Ukweli ya kwamba tuna uwezo wa kuamua kumtii au kutomtii Mungu ni udhihirisho tosha kuwa Mungu alituachia uhuru mkubwa ili Upendo utakaooneshwa kutoka kwetu Kwenda kwake uwe Upendo halisi.

Mungu hachoki. Isaya 40:28 “Je! Wewe hukujua? Hukusikia? Yeye Mungu wa milele, Bwana, Muumba miisho ya dunia, hazimii, wala hachoki; akili zake hazichunguziki.”

Biblia inaposema Mungu alistarehe siku ya saba haina maana kuwa alichoka, ni lugha ya picha kuonesha kazi maalum ya Uumbaji aliikamilisha na aliacha kufanya uumbaji, lakini sio kwamba alikuwa amechoka na wala sio kwamba aliacha kufanya kazi kabisa.

Mwanzo 2:2
"Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya."

Mwanzo 2:3
"Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya."

Yohana 5:17
"Akawajibu, Baba yangu anatenda kazi hata sasa, nami ninatenda kazi."

Sina majibu ya kila swali ulilouliza lakini nadhani nitakuwa nimesaidia kupunguza mzigo wa maswali yako
sasa me napenda je kitu sikioni hata kukishika.? namaanije hayo maandishi kwenye kitabu hata alie andikwa simjui sijui alikua anania gani.? kutupa uhuru ndo Kutuachia maandishi tu ndo tuamini na kumpende kweli.?
 
wako watu wanajua. walau naweza kukwambia kamuulize fulani atakua anamajibu.! mfano naweza kubwambia bodyguard wake au mume wake. au mjukuu wake. ila hayo maswali kuhusu Imani sina hata wakumuuliza nikiuliza naambiwa nakosea sana nakufuru.!
Vizuri kumbe unajua swali hilo kuhusu shuka la Samia kuna watu maalumu wa kuulizwa na si yeyote tu atakuwa na hilo jibu, sasa na hayo maswali kuhusu Mungu pia utizame ni yupi sahihi atakuwa na jibu ya hayo maswali.
 
hakuna binadamu anaweza kujibu hayo maswali kuhusu mungu. kwamfano nikamuulize nani naweza kupata majibu.?
 
Hizi mada za dini na Mungu Mara nyingi zipo complicated Sana ila hatuna budi kuishi humo humo tu.
 
hakuna binadamu anaweza kujibu hayo maswali kuhusu mungu. kwamfano nikamuulize nani naweza kupata majibu.?
Sasa ukijua hilo ndio usianze kusema kuwa hujibiwi maswali yako na kuelekeza lawama kwa watu huku ukijua hawawezi kuwa na hayo majibu ya maswali yako.
 
Sasa ukijua hilo ndio usianze kusema kuwa hujibiwi maswali yako na kuelekeza lawama kwa watu huku ukijua hawawezi kuwa na hayo majibu ya maswali yako.
asa nitaamini vp habari ambazo napewa na watu ambao nawao hawazijui vizuri.?
 
Back
Top Bottom