Hizi dola 1,000,000 ni za nani?

Hizi dola 1,000,000 ni za nani?

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,686
Polisi nchini Angola wanamtafuta mmiliki wa mkoba uliopatikana kwenye ndege ukiwa na dola milioni moja sawa na £650,000, ambao uliachwa kwenye ndege iliyokuwa ikisafiri hadi mjini Beijing, Uchina.

Rubani wa ndege hiyo alipata mkoba huo na kusalimisha pesa hizo kwa maafisa. Nchini Angola ni haramu kusafirisha kiasi hicho cha pesa kuvuka mipaka ya kimataifa.

Msemaji wa polisi Aristofanes dos Santos amesema kuwa uchunguzi sasa umeanzishwa kubaini asili ya pesa hizo ambazo zimetwaliwa na serikali.
Wachambuzi wanasema kuwa yeyote atakayedai kumiliki pesa hizo ataweza tu kurejesha asilimia 1.5% ya jumla ya pesa zote huku akikabiliwa na mashtaka ya kusafirisha pesa kinyume cha sheria.

Chanzo:
BBC
 
Kuna kiwango cha pesa ukiona tu masifuri yake moyo unalipuka
Imagine saa hii uko kitandani pekeyako unajifariji na JF halafu unaona post ya namna hii, unavuta picha ya $ 1,000,000/= yani dollar million moja zilivyojipanga vema na kubanana kwenye bridfcase...halafu unakumbuka shida zako.....!!!!
Dollar milioni moja jamaa kazikimbia....! Inauma sana...!!!
 
Polisi nchini Angola wanamtafuta mmiliki wa mkoba uliopatikana kwenye ndege ukiwa na dola milioni moja sawa na £650,000, ambao uliachwa kwenye ndege iliyokuwa ikisafiri hadi mjini Beijing, Uchina.
Rubani wa ndege hiyo alipata mkoba huo na kusalimisha pesa hizo kwa maafisa. Nchini Angola ni haramu kusafirisha kiasi hicho cha pesa kuvuka mipaka ya kimataifa.
Msemaji wa polisi Aristofanes dos Santos amesema kuwa uchunguzi sasa umeanzishwa kubaini asili ya pesa hizo ambazo zimetwaliwa na serikali.
Wachambuzi wanasema kuwa yeyote atakayedai kumiliki pesa hizo ataweza tu kurejesha asilimia 1.5% ya jumla ya pesa zote huku akikabiliwa na mashtaka ya kusafirisha pesa kinyume cha sheria.

Source: bbc

Ni za kwangu jamani.

Zilidondoka kwa bahati mbaya kwenye hiyo ndege.

Mimi sina noma, nirudishieni 10% tu na hizo nyingine zipelekeni kwa yatima wa Angola.

Tuwasiliane niwape akaunti yangu ya benki Bongo.
 
Kuna watu waaminifu duniani acha tu.
Unakabidhi kibunda cha $1M bila ukakasi wowote?
Mi nisingeweza.

Naona mlango wa mbinguni hutauona mkuu.

Hey, what the heck, ni afadhali uishi peponi hapa duniani. Pepo ya mbinguni is a toss up.
 
Ingekuwa Bongo 99.9 3/4 zisingerudishwa. Society yetu uhuni, wizi, uharamia, ukosefu wa uaminifu yaonekana ndio werevu na akili!
 
Huyo rubani atakua CCM tu, Ukawa hawawezi, rudisha hata senti...na kazi wanaacha...
 
Unapomwomba Mungu ujue hawezi kukujibu direct, lakini tukio kama hilo Mungu alijibu maombi ya Pilot ambaye hakutambua kuwa mwisho wa umaskini wake ilikuwa siku hiyo lakini hakujua.

Bahati haiji mara mbili.
 
Back
Top Bottom