Traxtion
JF-Expert Member
- Dec 10, 2021
- 5,945
- 11,912
Hizi IQ tests zimefanywa kwa upendeleo tu na kuziwekea nchi za kizungu namba kubwa kwenye IQ tests ili tuzidi kuwaona ni superior, hii ndio tabia za hawa watu weupe.
Vipimo vya IQ vilivuofanywa na Wechsler Adult Intelligence Scale (WAIS) na Stanford Binet Intelligence Scales vyote vimefanyika katika nchi za Magharibi huko na sisi hata hatukuhusika kwenye upimaji.
Kwa hiyo mtoto anayetoka kijiji cha Rukungiri, Uganda, ambaye anaweza kutambua mimea 50 tofauti kwa harufu, na anaweza kufuatilia mbuzi, ng'ombe, na kondoo usiku wa giza totoro pasipo umeme, na pia anasimulia hadithi kwa ufasaha katika lugha yake ya asili, wanamconsider ana akili pungufu kuliko mtoto wa Ulaya anayesolve Geometry kwenye karatasi huko Copenhagen, Denmark?
Nonsense!
Inaonekana hivi vipimo vyao vya IQ havipimi stadi za maisha, ubunifu, uelewa wa mambo, au hekima, ila vinapima uwezo wako wa kusolve mafumbo au maarifa yenye asili ya Kizungu, ila ukiwa na maarifa ya Kiafrika basi una IQ ndogo Huu ni upuuzi mtupu, ambao umevikwa joho la data na kulemewa na wakoloni wa kizungu tu.
Ni kama vile kipimajoto kilichotengenezwa wakati wa baridi kali kinachopima joto la jua la kitropiki.
Bara la Africa lote wameweka kuwa waty wake tuna IQ ndogo
Kila nchi ya Africa iko na below average IQ
Waafrika tusikubali kuamini kila upuuzi wa wazungu ambao wenyewe wanaita research.
Research kama hizi zinalenga kuwafanya Waafrika wajihisi inferior mbele ya wazungu na wamefanikiwa kiasi kwa baadhi ya watu. Ila mimi nawashauri kama mna watoto wenu msiwaaminishe kuwa wazungu wana akili kuliko sisi, mindset kama hizi ndio zinafanya tusiendelee
Ukiamini kuwa wewe ni mbumbumbu mwisho utakuwa mbumbumbu kweli