Viongozi wetu wanapenda kujionyesha na sifa zaidi kuliko uhalisia! Matatizo mengi sana MKJJ ukiachia mbali utata wa tarakim na maneno yaliyo katika hiyo cheki kuna mambo makuu najiuliza hapa-
Hivi kama ikiwa Mke wa Rais na wasaidiza wake wote wanaweza kuwa hawana umakini kiasi hicho je umakini upo wapi katika nchni yetu? lakini kingine ambacho kinanisumbua sana juu ya haya mambo pale ambapo fedha za serikali zinatumika bila tija, hakika nakwambia unaweza kukuta serikali imegharimia hiyo safari ya huyo mama kwa zaidi ya millioni tano jumla yote mpaka posho za mashushu kwa ajili ya kufanya huo upupu! hapa tija ipo wapi? Kwani kama angechagia hiyo fedha 380,000 au 380,000,000 bila kufanyika maandalizi makubwa yenye gharama zaidi ya huo mchango kuna ubaya gani na hapa ndipo kwenye tatizo katika bongo za viongozi wetu na wake zao.
Hakuna anaye fanya analysis ya faida ya haya mambo, lakini naamini hata ziara nyingi za viongozi wetu nje ya Ikulu kwenda mikoni na nje ya nchni ni mzigo wa ajabu pengine gharama za safari ni mara mbili ya kinachokwenda kufanywa. Kingine hii inaonyesha hana cha kufanya sijui kwani hasirudi kufundisha? labda ingemjengea heshima mara dufu! Inawezeka bado anakula msharaha wa uwalimu ingawa aingii darasa si ajabu kwa Tanzania.