Hizi Cheki hizi zina matatizo gani.. miye sitaki..

Ni yeye (WAMA) ndiye anatoa cheque....amewapiga 'changa la macho' hao wanaajiita 'Salma Kikwete Saccos'! All in all hii nchi ina vituko vingi sana....watu tunaowapa dhamana mara nyingi hawapo makini kabisa!

Kama baba kila siku anadanganywa unatarajia mama aweje?
 
Sikutegeme sana kama uwezo wa JK unaweza kutofautiana na uwezo wa mkewe, kiakili, umakini na kuweza kuchambua mbivu na mbichi. Full of reckless leaders. Hii inaonyesha ni jinsi gani nchi inavyopumilia mashine, hii ni indicator kuwa umakini katika nchi umepungua kama sio kuondoka kabisa. Sio JK peke yake hili ni tatizo la nchi nzima kama kiongozi wa nchi yupo hivi hii inasadifu hali halisi ya nchi katika umakini!
 
Du, hawa ni wale ambao enzi zao za shule hisabati waliiona kama 'kikwazo' badala ya kuiona kama 'msaidizi'. Inatupasa kama taifa, na katika kila familia tuinue mapenzi kwa somo hili mashuleni. Sio vibaya kila mzazi, hata aliye mchovu kabisa, akamfundisha mwanaye kile alichoambulia enzi zake za shule.
 
Mbona hata Mwanakijiji kakosea. Hizi haziitwi cheki, zinaitwa hundi. Na hizi ni mfano tu wa hundi.


Mkuu mfano wa hundi lazima uwe sawa na hundi yenyewe..............

Huwezi kuonesha mtaani unalipa Laki Tatu halafu baadae ukalipa Billioni Tatu then unasema ile ilikuwa mfano wa hundi tu.....Hapana,hii haikubaliki
 
Ufisadi mtupu iweje ajiandikie cheque yae mwenyewe???? nae ni wale Gamba wa CCM tu. jamani halafu huyu si alikuwa mwalimu?
 
mkuu..... WAMA ndiyo wanamlipa Mama Salma Kikwete .... kwa hiyo mama anajitapeli mwenyewe kwani WAMA ni yake na Mama Salma Kikwete SACCOS ni yake ..... huyu ni mtu mmoja na pia hayupo makini

Alas! kumbe zinatoka mfuko wa shoto zinahamishiwa mfuko wa 'kulia'!
 
Tehe tehe teheee! Haya ma-saccos, foundation, NGO za wake wa wakubwa zinawasaidiaje wale akina mama wa vijijni! Hivi presidaa atakayefuata naye mke wake inabidi aanzishe kiji-saccos, foundation au NGO yake. Je hii do demokrasi mpya au ndo uwajibikaji mpya wa ki-tz.
Katika katiba tunahitaji kuweka mipaka ya hawa warembo wa ikulu. Ebu fikiria akiingia atakaye kuwa na warembo wanne wa halali, kwa wastani tutegemee ofisi za namna hii zisizopungua nane ikiwa kila mmoja atakuwa na NGO itakayokuwa na Saccos.
 
Mh WildC, nadhani Joseph akiitwa Yusuf inaleta maana kuliko kosa la kumwita Joseph kama Mary! maoni tu.
Nimelitafuta hili neno "cheki" kwenye kamusi yetu halimo. Ni tofauti kidogo na huo mfano wako. Tusonge mbele na mada yetu. Kosa kama lile sio Salma wala JK peke yao wanaweza wasiligundue. Vifijo, nderemo na shamrashamra zinazokuwa pale hazimpi nafasi mgeni rasmi kuliona hilo. Na wala halina madhara pande zote.
 
Hao walioandika hawakuona?na mama Salma mwenyewe hakuikagua au ana macho lkn haoni?
 
Ndivyo walivyo. Wanashindana vituko

Mwisho wa siku kinachoumia ni Tanzania na walalahoi wake maskini. Ni jambo liliowazi wazi kwamba wake/waume zetu kuna part kubwa sana wanaplay kwenye perfomance zetu maishani mpaka kwenye kazi. Ndio maana walisema when you see a strong man then there is a strong woman behind au what you do off the job determines what you do on the job. Sasa ukiwa bogus then ukawa unaspend time na bogus obviously utaperform poorly.
 
Nimelitafuta hili neno "cheki" kwenye kamusi yetu halimo. Ni tofauti kidogo na huo mfano wako. Tusonge mbele na mada yetu. Kosa kama lile sio Salma wala JK peke yao wanaweza wasiligundue. Vifijo, nderemo na shamrashamra zinazokuwa pale hazimpi nafasi mgeni rasmi kuliona hilo. Na wala halina madhara pande zote.

kumbuka .... yawezakuwa kwamba signatory wa WAMA ni Mama Salma na vile vile Signaory wa Mama Salma SACCOS pia ni mama Salama Kikwete ... a dummy cheque is always drafted from the leaf of a real cheque ......

mama salama amechemka
 
Huyu mama inawezekana naye akawa ni moja ya chanzo cha mme wake kushindwa kufanya kazi,
hana muda wa kusimamia mambo ya familia, najua wanakatoto kadogo nyumbani, ni nani anapitia
hata madaftari yake nyumbani kama dad na mom wote ni wazurulaji kutafuta publicity, ndo matokeo
yake hako katoto nako katakuja kuwa kakilaza.

Nani anaandaa chakula cha rais wetu, sio mkewe?

Pia kwa nafasi ya mme wake, lazima atakuwa na wageni wengi sana nyumbani, nani anawakaribisha
na kuwakarimu wageni hawa, au ndio maana ikulu sasa zinaenda kila aina ya takataka kuanzia
matapeli, machangudoa, majizi, vibaka, mafisadi waganga, wachawi na wanamazingaombwe,
sababu nyumba haina msimamizi.

Alafu angetakiwa ajue kwamba dawa za mvuto za mume wake zimeishiwa nguvu kwa kiwango
kikubwa sana kama sio kwishne kabisa ndo maana jamii inaziona kasoro zake hata zike ndooogo sana,
familia yake imekuwa ni target ya kila aina ya mapingamizi, kwa nini asijifiche nyumbani kuhepuka
haya yote lakini,

na kama anajichosha namna hii mzee anapumzika vipi jioni kama sio kumtia majaribuni ******
 
Cha kushangaza zaidi wao walioko karibu na hata huyo mama Salma mwenyewe na hata huyo aliyeishika hiyo cheki na hata huo umati wa watu waliopo hapo wanajifanya hawaoni makosa wakati mimi msomaji nayaona kwa hali nyingine tunaweza kusema ni makusudi au wanajua wanachofanya au aliyeandika hiyo cheki hakwenda shule hata mtoto wa darasa la 7 sidhani kama anaweza kufanya makosa ya kijinga namna hiyo, halafu cheque hiyo hiyo yenye makosa wanai-display public kabisa bila kuhisi tatizo lolote watu wakisema ni wizi wanaanza kulalama
 
WAMA- Salma Kikwete
SALMA KIKWETE SACCOS - Salma Kikwete

Yaani hela inatoka point A kurudi point A
 
kumbuka .... yawezakuwa kwamba signatory wa WAMA ni Mama Salma na vile vile Signaory wa Mama Salma SACCOS pia ni mama Salama Kikwete ... a dummy cheque is always drafted from the leaf of a real cheque ......

mama salama amechemka
Si unaona hata wewe umekosea! Umeandika "Signaory" badala ya signatory.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom