Hizi Cheki hizi zina matatizo gani.. miye sitaki..

Kweli umakini umekosekana katika kuandika hizo tarakimu kwa kuondoa 0 mwishoni. Hayo yote ni 9 lakini 10 inakuwaje pesa ya foundation iandikiwe kwa mtu binafsi? Na hawa ndio viongozi wetu tunaowategemea wakemee hali hii. Where is the accountability?

Nadhani Mwanakijiji hapendi aina hizi za cheque zinazokuwa personalised. Really unacceptable!
 

carelessness.jpg
 
Swali la kizushi samahani sana wakuu!

Salma R. Kikwete; R stands for what?
 
Huyu mama ni kihere here sana na anapenda sifa sifa tu....haina logic kuaandaa sherehe yote hiyo kwa ajili ya kukabidhi check ya sh laki tatu na elfu themanini, angeweza kukabidhi kimya kimya tu
 
ndo maana kiungamishi wao (R. one) anatumia camry kupigia misele, km wangekuwa makini wangeweza kumnunulia chalii walau hata ka'RAV 4.
 
hii nayo kali!

Sasa nijiulize tatizo liko kwa nani? ni wanaokabishi au wasadizi wa mama, au ni mama mwenyewe hakukagua kuwa anakabidhi nini?
hii ni aibu nyingine tena.
 
Kwanza Tarakimu zimekosewa, 3,800,00 sio milioni tatu na laki nane (3, 800,000). Tukipanga tarakimu zao sawa sawa inakuwa hivi 380,000.

Pili, inalipwa kwa Salma Kikwete Saccos, kama hiyo saccos ni ya Salma ni sawa, lakini angalia kulia chini ya tarakimu kuna maneno Wanawake na maendeleo foundation! sijui hii ni mpya kwasababu haimaanishi WAMA.

Picha ninayoipata kuna Salma Kikwete saccos, Wanawake na maendeleo foundation, nimeshindwa kuelewa analipa nani na analipwa nani.Salma kikwete saccos inalipwa na wanawake na maendeleo foundation!!! mh imenikanganya nakiri.

Nadhani ipo haja ya katiba mpya itakayoandikwa ianishe wigo wa madaraka ya wake wa viongozi wakuu.
Hawa wapambe wa mke wa rais ikiwa ni pamoja na wana usalama wanahakiki kazi zao kweli, hii si kumdhalilisha mke wa mkuu hata kama naye alipaswa kusoma anachotoa au kupokea. Mh!
 
1.jpg


Hii ndo kibongo bongo mke wa muheshimiwa nae hayupo makini.

Kwa maneno ni shilingi milioni tatu na laki nane kule pembeni wamempiga changa la macho imeandikwa 3.800,00/= vitu vya kushangaza kama hivi utaviona bongo tu.
Kikosi cha intelenjisia na protocali sijui kimemdanganya mke wa rais?
Kwa hisani ya MJENGWA - Picha, Habari & Matangazo
 
Mbona hata Mwanakijiji kakosea. Hizi haziitwi cheki, zinaitwa hundi. Na hizi ni mfano tu wa hundi.
 
Ni yeye (WAMA) ndiye anatoa cheque....amewapiga 'changa la macho' hao wanaajiita 'Salma Kikwete Saccos'! All in all hii nchi ina vituko vingi sana....watu tunaowapa dhamana mara nyingi hawapo makini kabisa!
 
Ni yeye (WAMA) ndiye anatoa cheque....amewapiga 'changa la macho' hao wanaajiita 'Salma Kikwete Saccos'! All in all hii nchi ina vituko vingi sana....watu tunaowapa dhamana mara nyingi hawapo makini kabisa!

mkuu..... WAMA ndiyo wanamlipa Mama Salma Kikwete .... kwa hiyo mama anajitapeli mwenyewe kwani WAMA ni yake na Mama Salma Kikwete SACCOS ni yake ..... huyu ni mtu mmoja na pia hayupo makini
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom