Hivi, Zanzibar ingekuwaje bila ya Muungano? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi, Zanzibar ingekuwaje bila ya Muungano?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ngalikihinja, Sep 9, 2009.

 1. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #1
  Sep 9, 2009
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,435
  Likes Received: 3,782
  Trophy Points: 280
  Hivi, Zanzibar ingekuwaje bila ya Muungano? Wangetajirika au wangekuwa maskini zaidi?
   
 2. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #2
  Sep 9, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  wewe unadhani vipi?
   
 3. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #3
  Sep 9, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,593
  Likes Received: 18,589
  Trophy Points: 280
  Soma kijarida cha Siasa ndani ya Mwananchi la Jumatano ya leo, ukurasa wa 5 kwenye hoja kutoka Zanzibar ya Mwandishi wa BBC Swahili, Mwanasheria na Mwanaharakati, Ally Saleh anayeuliza swali hilo hilo.

  Kwa maoni yangu, Zanzibar ingekuwa mbali sana nje ya muungano, ukiondoa Afrika Kusini, Zanzibar ndio nchi ya kwanza kuwa na Televisheni ya Rangi Kusini mwa Jangwa la Sahara mwaka 1972.Ukitembelea Bait Al Ajab ukayashuhudia yaliyokuwako humo ikizingatiwa ni Zanzibar ya kale, utakubaliana na mimi saa hizi, hakuna nchi yoyote Afrika ingeifikia Zanzibar kwa utalii, miundo mbinu na biashara kama bandari huru.Yaani kwa lugha nyingine, Dubai ingekuwa cha mtoto.

  Ukitafuta historia ya visiwa vyote vya bahari ya hindi, Zanzibar ndio ilikuwa kitovu cha kila kitu, Reunion na Seycheles vimeibuka juzi juzi tuu, yaani Zanzibar ingekuwa mbali sana , yaani wee acha tuu.Huwezi kuizungumzia Zanzibar ingekuwa wapi bila kuuzungumza muungano.

  Ukibahatisha kusoma andiko la Prof Isaa Gullamhussein Shivji " The Legal Basis of Union Between Tanganyika na Zanzibar" alilolitoa mwaka 1994 anaeleza bayana kuhusu misingi ya sheria iliyounda Muungano, amini usiamini hata hicho kinachoitwa 'Hati za Muungano' sio legal documents, sio mkataba wa kisheria ni makubaliano tuu kati ya Nyerere na Karume kwa lengo la kuokoa jahazi la kuyalinda mapinduzi, Karume alikuwa radhi muungano hata uwe wa nchi moja na hata bila maandishi lakini kwa msingi mmoja tuu, "Wewe rais, mimi makamo".

  Karume akifufuka leo na kukuta rais wa Zanzibar si lolote si chochote, hili tuu pekeyake ni kuvunja yale makubaliano ya msingi na angeuvunjilia mbali muungano instantly. Naomba msinione kama mpinga muungano, bali ni mpenda haki tuu itendeke na kuweka mambo wazi tuu ni kuwa hakujakuweko mkataba wa muungano, Karume aliisubmit dola ya Zanzibar kwa Tanganyika, Tanganyika ikajibadili jina kuitwa Tanzania, ikayameza mamlaka yote ya kidola ya Zanzibar katika kitu kiitwacho mambo ya Muungano, huku yale ya Tanganyika nje ya Muungano yakiendelea kuwa ya Tanzania hivyo aliyejisubmit ni Dola ya Zanzibar kumezwa na Tanganika ilijibadili jina kuitwa Tanzania.

  Lugha nyepesi Dola ya Tanganyika ipo kwa jina jipya la Tanzania, Serikali ya Tanganyika ipo kwa jina la Serikali ya Muungano. Serikali ya Zanzibar ipo kwa jina la serikali tuu kama jina tuu na sio dola. Jina halali la Serikali ya Zanzibar lilitakiwa liwe Mamlaka ya Zanzibar, maana Zanzibar sio nchi, ni sehemu tuu ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania yenye mamlaka ya kujitawala kwa mambo yake ya ndani.

  Namalizia kwa kuzungumzia kidogo katiba. Kilichofanyika kwenye Muungano, ndicho kilichofanyika kwenye uundaji wa katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ambayo ni katiba iliyoundwa kibabe na kwa hadaa bila kufuata misingi ya uundaji wa katiba, yaani "Constitutional without Constititionalism" ambapo katiba huundwa na constituent assembly, Tanzania haukuwahi kufanyika bali mwaka 1977, bunge la chama kimoja lilijigeuza constituent assembly na kuipitisha hiyo katiba kwa dakika 15! Mandate ambayo ni kubwa kuliko uwezo wa bunge letu.

  Haya naona niachie hapa nisije nikatonyesha na makovu ya vidonda vya zamani, ila naamini siku moja haki itatendeka.
   
 4. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #4
  Sep 9, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,056
  Likes Received: 24,060
  Trophy Points: 280
  Mi nadhani kusingekuwa na Zanzibar. Kungekuwa kuna Unguja ya ASP na Aman Karume na Pemba ya CUF na Seif Shariff Hamad. Usisahau kusingekuwa na CCM kule.
   
 5. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #5
  Sep 9, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  CUF imeanza mwaka gani na ASP imeanza lini?
   
 6. S

  Son of Alaska JF-Expert Member

  #6
  Sep 9, 2009
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 2,813
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 0
  BILA muungano ni obvious kwamba UNGUJA kungekuwa na SHARIA kwa kwenda mbele
   
 7. K

  Kekuye Senior Member

  #7
  Sep 9, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 116
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unguja ingekuwa 'sovereign state' na vivyo hivyo Pemba na kila moja ina uwakilishi Umoja wa Mataifa.
   
 8. w

  wasp JF-Expert Member

  #8
  Sep 9, 2009
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 206
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Zanzibar imekuwepo kabla ya muungano na itaendelea kuwepo hata kama muungano ukivunjika.
   
 9. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #9
  Sep 9, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,377
  Likes Received: 3,140
  Trophy Points: 280
  Kwanza utawala wa sheria usingekuwepo.kusingekuwepo muungano mpaka sasa tungekuwa tunajadili uunguja na upemba kabla ya kushughulikia maendeleo...kwa hiyo nchi ingekuwa omba omba huko oic....
   
 10. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #10
  Sep 9, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kungekuwa na Tanganyika na Zanzibar na mahusiano yao yangekuwa ya kiuendelevuu kibiashara na kiuchumiii..

  Umaskini ungepungua sanaa pemba.
   
 11. J

  Jews4ever Member

  #11
  Sep 9, 2009
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 74
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Waislamu wa Tanganyika wangehamia zenj
   
 12. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #12
  Sep 9, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  NAkubliana na watoa hoja waliotangulia kama kusingekua na muungano Zanzibar isingekuwepo kungelikua na Unguja na Pemba na vita ya wenyewe kwa wenyewe na moja ya kambi za Benladen mkondo ambao wangeliufuata si tofauti na Somalia kuhoji Muungano pamoja na mapungufu yake ni baadhi ya watu kutaka kujifariji wakati wanajua fika kua muungano umeisadia Zanzibar kwa iasi kikukubwa na Tanganyika imepoteza sana kwa kuulinda muungano kwa gharama yoyote.Hili lilitokea kwa Jamuhuri ya Kisoviet (Urusi) Hambapo Russia amabayo ilitumia pesa nyingi narasilimali zake kwa ajili ya jamuhuri nyinhine zilizokuzmo Katika jamuhuri ya Kisoviet.Baada ya kuvunjika kwa imaya hiyo asilimia 99 ya nchi hizo ni masikini na ombaomba na bado zinaitegemea Russia Ndugu zangu Wazenj huo ni mfano na kumbukeni wakati wote UTENGANO NI UDHAIFU!
   
 13. J

  JokaKuu Platinum Member

  #13
  Sep 9, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,805
  Likes Received: 5,098
  Trophy Points: 280
  ..ingekuwa kama Comoro, very unstable.
   
 14. E

  Ex-Fisadi Member

  #14
  Sep 9, 2009
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kusingekuwepo na zanzibar stable tunavyoiona sasa. Kungekuwepo na mapanga mbele kwa mbele au mapanga shaaa!!! Vile karume na wenzake walivyo wachinja waarabu na washirika wao,waarabu nao wangeisha lipiza kisasi!!! Genocide ya Rwanda ingeanzia zanzibar, na instability unayoiona Somalia ingekuwa imeanzia Zanzibar.Imagine wazanzibar, No wapemba wanaokwenda kutafuta ukimbizini Somalia!!!!!! ukiona hilo linatendeka ndipo unapopashwa kubaini Zanzibar ni kitu gani!!! Zanzibar ni bomu linalosubiri muungano uvunjike ili lilipuke. bila muungano zanzibar haitakuwepo
   
 15. Nkamangi

  Nkamangi JF-Expert Member

  #15
  Sep 9, 2009
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 642
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  uuwii!! ingebidi waarabu warudi kuokoa jahazi.
   
 16. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #16
  Sep 9, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  ^^ umefulia..
   
 17. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #17
  Sep 9, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Tatizo sio Zanzibar ,mi huwaga najiuliza Tanganyika ingelikuwaje kama si huu Muungano ambao wanaung'ang'ania ,utafikiri hapa tulipo wanataka kuzama na kuogelea awajui.

  maana ukiipima Zanzibar tokea na kabla ya Uhuru kulikuwa na amendeleo yanayoonekana ,historia inatwambia ni nchi ya mwanzo kuwa na umeme unaochukua radius ya 5Km hata uingereza walikuwa hawaipati Zanzibar ,pia tarehe zinatuambia Zanzibar ilikuwa inategemewa katika kutoa misaada kuziokoa nchi flani flani za Wazungu ikiwemo Denmark na baadhi ya Scandnavian wakati huo.Zanzibar ni nchi ya mwanzo kuwa na Tv ya rangi hapa Afrika kama haitoshi gari ya mwanzo kunguruma kule Kuwait inasemekana ilitoka Zanzibar na wameiweka kwenye museum yao.
  Halafu tunaposema Zanzibar jaribuni kutafuta mipaka yake kwenye 1880 ,baba yenu wa Taifa hata hajajulikana kama atazaliwa na wengi wa wazee wenu walikuwa bado wapo kwenye misitu ya Congo na Zaire wakitembea na mishale migongoni wakiwinda ngulewe nchanga yaani hata hawajaiona wala hawajui bahari ni kitu gani.Leo hii mmejua kuvaa suruali na tai mnainyanyasa Zanzibar.
  Ila mimi siwashangai maana mnatoka mbali sana na mmefika mjini.
   
 18. Monsignor

  Monsignor JF-Expert Member

  #18
  Sep 9, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 523
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  CUF, ASP yote ni majina tu. Kwani CCM imeanza mwaka gani? Suala hapa siyo jina la chama bali ni mtizamo. Kwani CUF wakiamua kujiita ASP sasa hivi mlengo wao utabadilika?

  May be. But you cannot bet on that.

  Nyerere aliona mbali japo jina hilo linawatia kichefuchefu watu wengine. Bila muungano hakuna cha sisi Wazanzibari bali wao wazanzibara kisha sisi wapemba wao waunguja. Hamtakaa salama

  Umaskini Pemba umepunguzwa na fursa walizopata Wapemba bara

  Hawawezi kuelewa hilo. Umimi umetawala nyoyo zao.

  That is ununderstatement. Comoro wanagombea madaraka hawa watakuwa kama Somalia chuki bin chuki. wewe mwarabu, wewe mtumwa, wewe chogo almuradi kila aina ya uchochezi.

  Well put Ex-Fisadi.
  Naaamini umefika wakati kiongozi mmoja ajipe ujasiri asema let them go. Wao wenyewe hawezi kujitoa kwa sababu wanajua fika kabisa kuwa they have a lot to loose. Viongozi wao ndio hawana msaada. Jana Waziri kongozi kafuturisha nyumbani kwake O'bay. Kweli huyu atadai kuwa muungano hauna faida? NI kiongozi gani Mtanganyika ana nyumba Zanzibar?
  wazanzibari wakati ndo huu, haki haitolewi bali hutwaliwa. Bila kuvunja muungano mtaendelea kulalama mpaka kiama huku maisha yakiendelea.
   
 19. O

  Omumura JF-Expert Member

  #19
  Sep 10, 2009
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Yote hayo ya nini, muungano uvunjike ili kila mtu apewe haki yake stahiki. kwa mtazamo wangu, huu muungano daima umeendelea kuwa chanzo cha kutoaminiana baina ya pande zote mbili,matokeo yake shutuma haziishi kutoka kote kote.Bora uvunjike ili ukweli udhihiri,kama wengine watapata karafuu then wengine wapate madini maisha yasonge mbele as usual!!!
   
 20. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #20
  Sep 10, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  There is an easy way to find out...
   
Loading...