Hivi, Zanzibar ingekuwaje bila ya Muungano?

Yote hayo ya nini, muungano uvunjike ili kila mtu apewe haki yake stahiki. kwa mtazamo wangu, huu muungano daima umeendelea kuwa chanzo cha kutoaminiana baina ya pande zote mbili,matokeo yake shutuma haziishi kutoka kote kote.Bora uvunjike ili ukweli udhihiri,kama wengine watapata karafuu then wengine wapate madini maisha yasonge mbele as usual!!!
Waziri Kiongozi wa Zanzibar afuturisha nyumbani kwake Oysterbay dar es salaam,Marais wastaafu wa Zanzibar wanaishi Dar es salaam,hii imekaaje???Na wavunje muungano tuone nani atalia sana.
........ndio hio.
 
Maelezo ya Pasco yanavutia kuyasoma...lakini naomba kutofautiana nae katika hoja kwamba Zanzibar ingekuwa mbali sana na kilichoizuia Zanzibar kupaa ni huo Mwuungano. Andiko la Prof. Shivji juu ya uhalali wa Mwuungano umelichambua kwa mawazo yako ya kufikirika bila kuhuisha hali halisi ya wakati le na mahitaji yaliyokuwepo wakati wa Mwuungano na uwazi uliachwa baada ya Muasisi mmoja wa Mwungano kuuwawa!

Kwa sababu demokrasi inakuwa na kusonga mbele toka mapungufu kibao ya Mwuungano hadi marejeo yanayoeleka kurekebisha mapungufu hayo kuelekea demokrasi ya kweli, natisha kusema kwamba UTASHI NDO ULIOZAA MWUUNGANO , na utashi ndo sheria yenyewe...defacto Legal status. Maelezo kibao tunayoweza kuyawaza na kuyawazua ni hoja za zuoni zinazotimiza hoja za malengo ya kitafiti na kubishaniwa/kujadiliwa.

Kwa Wakati moja au mwingine pande zote za Mwuungano zimefaidika na muudo uliopo. mapungufu ni mambo ya kujadiliwa ikiwa bado tuna dhamira ya kuudumisha!

Nyerere alipomtaka Karume awe kiongozi.. Karume alimjibu: " Mwalimu.. kuwa wewe Rais na mimi Makamu" Walio karibu na Karume walishawahi kuutamkia umma !

Tu Pasco umeshawahi pia kuchambua kauli za Karume juu ya uchaguzi wa Rais wa Zanzibar????Aliwahi kusema... :Uchaguzi wa nini.. Mimi Si ndio Rais?" Kilitonya chanzo kimoja. Nadhani hoja na ...."Ninge.... Inge???? Pengine...? ni mawazo hasi ambayo yanapaswa kuwekwa kapuni na kuganga haya yaliyopo!!!!

MUNGU IBARIKI TANZANIA... BAWIKI WATANZANIA WOTE NA WAOKOE KATIKA MAANGAMIZO YA MAFISADI NA WASIOITAKIA MEMA...
 
hawa wangekuwa wanakula kashata tuu na kahawa hawataki makuu wavivu kama nini,ila nafikiri wangekuwa better kuliko sasa!
 
Naomba msinione kama mpinga muungano, bali ni mpenda haki tuu itendeke na kuweka mambo wazi tuu ni kuwa hakujakuweko mkataba wa muungano, Karume aliisubmit dola ya Zanzibar kwa Tanganyika, Tanganyika ikajibadili jina kuitwa Tanzania, ikayameza mamlaka yote ya kidola ya Zanzibar katika kitu kiitwacho mambo ya Muungano, huku yale ya Tanganyika nje ya Muungano yakiendelea kuwa ya Tanzania hivyo aliyejisubmit ni Dola ya Zanzibar kumezwa na Tanganika ilijibadili jina kuitwa Tanzania.

Lugha nyepesi Dola ya Tanganyika ipo kwa jina jipya la Tanzania, Serikali ya Tanganyika ipo kwa jina la Serikali ya Muungano. Serikali ya Zanzibar ipo kwa jina la serikali tuu kama jina tuu na sio dola. Jina halali la Serikali ya Zanzibar lilitakiwa liwe Mamlaka ya Zanzibar, maana Zanzibar sio nchi, ni sehemu tuu ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania yenye mamlaka ya kujitawala kwa mambo yake ya ndani.

Namalizia kwa kuzungumzia kidogo katiba. Kilichofanyika kwenye Muungano, ndicho kilichofanyika kwenye uundaji wa katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ambayo ni katiba iliyoundwa kibabe na kwa hadaa bila kufuata misingi ya uundaji wa katiba, yaani "Constitutional without Constititionalism" ambapo katiba huundwa na constituent assembly, Tanzania haukuwahi kufanyika bali mwaka 1977, bunge la chama kimoja lilijigeuza constituent assembly na kuipitisha hiyo katiba kwa dakika 15! Mandate ambayo ni kubwa kuliko uwezo wa bunge letu.

Haya naona niachie hapa nisije nikatonyesha na makovu ya vidonda vya zamani, ila naamini siku moja haki itatendeka.
Maneno sawia kabisa Ally Saleh Alberto. Watanganika wametudumaza sana kimaendeleo.

Ila mimi naona bila Muungano Zanzibar ka maana ya Unguja na Pemba ingekuwa mbali sana. Ila huku Tanganyika ingekuwa vita kali sana ya UDINI. Mimi naona Wakatoliki wangejitwalia Tanganyika na kusababisha vita baina ya madhehebu na madhehebu au hata dini kwa dini kwa jinsi mbegu hizi za chuki za kidini zilivoshamiri.
 
kwa ufupi Zanzibar ingegawanyika mara mbili yaani ile ya maalim Seif na ya Karume.

Na Tanganyika ingekugawika mara tano yaani ile ya Pengo(Katoliki), Ile ya Malasusa(KKKT), Ile ya Dr Mokiwa (Anglican), Ile Ya mufti Simba (Bakwata) na ile ya Sh Kundecha (Shura ya maimamu) kila mmoja angeikata Tanganyika pande lake
 
Maelezo ya Pasco yanavutia kuyasoma...lakini naomba kutofautiana nae katika hoja kwamba Zanzibar ingekuwa mbali sana na kilichoizuia Zanzibar kupaa ni huo Mwuungano. Andiko la Prof. Shivji juu ya uhalali wa Mwuungano umelichambua kwa mawazo yako ya kufikirika bila kuhuisha hali halisi ya wakati le na mahitaji yaliyokuwepo wakati wa Mwuungano na uwazi uliachwa baada ya Muasisi mmoja wa Mwungano kuuwawa!

Kwa sababu demokrasi inakuwa na kusonga mbele toka mapungufu kibao ya Mwuungano hadi marejeo yanayoeleka kurekebisha mapungufu hayo kuelekea demokrasi ya kweli, natisha kusema kwamba UTASHI NDO ULIOZAA MWUUNGANO , na utashi ndo sheria yenyewe...defacto Legal status. Maelezo kibao tunayoweza kuyawaza na kuyawazua ni hoja za zuoni zinazotimiza hoja za malengo ya kitafiti na kubishaniwa/kujadiliwa.

Kwa Wakati moja au mwingine pande zote za Mwuungano zimefaidika na muudo uliopo. mapungufu ni mambo ya kujadiliwa ikiwa bado tuna dhamira ya kuudumisha!

Nyerere alipomtaka Karume awe kiongozi.. Karume alimjibu: " Mwalimu.. kuwa wewe Rais na mimi Makamu" Walio karibu na Karume walishawahi kuutamkia umma !

Tu Pasco umeshawahi pia kuchambua kauli za Karume juu ya uchaguzi wa Rais wa Zanzibar????Aliwahi kusema... :Uchaguzi wa nini.. Mimi Si ndio Rais?" Kilitonya chanzo kimoja. Nadhani hoja na ...."Ninge.... Inge???? Pengine...? ni mawazo hasi ambayo yanapaswa kuwekwa kapuni na kuganga haya yaliyopo!!!!

MUNGU IBARIKI TANZANIA... BAWIKI WATANZANIA WOTE NA WAOKOE KATIKA MAANGAMIZO YA MAFISADI NA WASIOITAKIA MEMA...

Hicho kitabu ukikisoma between the lines kinasema Muungano ni halali! Maelezo mengi yametolewa juu ya Muungano na kama kuna mwenye akili ya kuelewa ameshaelewa! Tofauti ndogo zilizopo ZOTE zinazungumzika. Tatizo lililopo sasa hivi ni baadhi ya wanasiasa kutaka ku-take advantage ndani ya kasoro chache zilizopo! Kenya walichekelea kuvunja iliyokuwa EAC mwaka 1977 lakini sasa hivi wako desperate kutaka tena kuwe na EAC (a political federation). Kwa hiyo tusivurugwe na wanasiasa wachovu ambao wana maslahi binafsi na baadaye tukaanza tena kutaka kuungana huku mambo yakiwa yameharibika irreparably!
 
Na Tanganyika ingekugawika mara tano yaani ile ya Pengo(Katoliki), Ile ya Malasusa(KKKT), Ile ya Dr Mokiwa (Anglican), Ile Ya mufti Simba (Bakwata) na ile ya Sh Kundecha (Shura ya maimamu) kila mmoja angeikata Tanganyika pande lake

kuu umemaliza kila kitu hapo.

Hongera kwa uchambuzi
 
Hoja za namna hii ni za uchochezi na zinahatarisha muungano wetu. Swali hilo ni sawa na mtu kujiuliza "Hivi mimi ningezaliwa Ulaya ningekuwaje?
Tutafute hoja zingine za msingi.
 
Lugha nyepesi Dola ya Tanganyika ipo kwa jina jipya la Tanzania, Serikali ya Tanganyika ipo kwa jina la Serikali ya Muungano. Serikali ya Zanzibar ipo kwa jina la serikali tuu kama jina tuu na sio dola. Jina halali la Serikali ya Zanzibar lilitakiwa liwe Mamlaka ya Zanzibar, maana Zanzibar sio nchi, ni sehemu tuu ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania yenye mamlaka ya kujitawala kwa mambo yake ya ndani.

Namalizia kwa kuzungumzia kidogo katiba. Kilichofanyika kwenye Muungano, ndicho kilichofanyika kwenye uundaji wa katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ambayo ni katiba iliyoundwa kibabe na kwa hadaa bila kufuata misingi ya uundaji wa katiba, yaani "Constitutional without Constititionalism" ambapo katiba huundwa na constituent assembly, Tanzania haukuwahi kufanyika bali mwaka 1977, bunge la chama kimoja lilijigeuza constituent assembly na kuipitisha hiyo katiba kwa dakika 15! Mandate ambayo ni kubwa kuliko uwezo wa bunge letu.

Haya naona niachie hapa nisije nikatonyesha na makovu ya vidonda vya zamani, ila naamini siku moja haki itatendeka.
Yaani siku zote nakufagilia kwa Elimu yako lkn leo zaidi,sijui nikupe cheo gani mkuu.. Big 5
 
CUF, ASP yote ni majina tu. Kwani CCM imeanza mwaka gani? Suala hapa siyo jina la chama bali ni mtizamo. Kwani CUF wakiamua kujiita ASP sasa hivi mlengo wao utabadilika?

May be. But you cannot bet on that.

Nyerere aliona mbali japo jina hilo linawatia kichefuchefu watu wengine. Bila muungano hakuna cha sisi Wazanzibari bali wao wazanzibara kisha sisi wapemba wao waunguja. Hamtakaa salama

Umaskini Pemba umepunguzwa na fursa walizopata Wapemba bara

Hawawezi kuelewa hilo. Umimi umetawala nyoyo zao.

That is ununderstatement. Comoro wanagombea madaraka hawa watakuwa kama Somalia chuki bin chuki. wewe mwarabu, wewe mtumwa, wewe chogo almuradi kila aina ya uchochezi.

Well put Ex-Fisadi.
Naaamini umefika wakati kiongozi mmoja ajipe ujasiri asema let them go. Wao wenyewe hawezi kujitoa kwa sababu wanajua fika kabisa kuwa they have a lot to loose. Viongozi wao ndio hawana msaada. Jana Waziri kongozi kafuturisha nyumbani kwake O'bay. Kweli huyu atadai kuwa muungano hauna faida? NI kiongozi gani Mtanganyika ana nyumba Zanzibar?
wazanzibari wakati ndo huu, haki haitolewi bali hutwaliwa. Bila kuvunja muungano mtaendelea kulalama mpaka kiama huku maisha yakiendelea.
GREAT THINKERS NDO HII.
Kwa mara ya kwanza namuona mwana JF humu kafulia.. loh! hata aibu huna.
 
Wanajamvi kama Zanzibar insingekuwa ndani ya muungano leo tungekuwa na wakimbizi kibao kutoka nchi za Pemba na Unguja.Nchi za Burundi na Rwanda zingekuwa ndani ya muungano kamwe tusingeshuhudia mauaji makubwa na wakimbizi kibao.Zanzibar hawawezi kujitoa ndani ya muungano hata kwa dakika moja wanajua ndani ya muungano wanauhakika na ulinzi na usalama.

Hivi wale wapemba waliojazana Dar wataenda wapi kama muungano ukivunjika,marais wote wastaafu wamekimbilia huku bara maana wanajua Zanzibar hakuna ardhi ya kutosha ,tena uchumi wao unategemea zaidi karafuu ambayo haina bei kwenye soko la dunia.

Natamani atokee kiongozi mmoja huku bara akaauvunjilia mbali muungano tuone sinema ya bure,yaani siku ya kwanza tu maalimu sefu na Dr Karume watakimbilia Dar kuomba hifadhi.Tanzania bara imetumia gharama kubwa sana kuwalea na kuwalinda wazanzibar chakushangaza bado wanachonga utadhani Zanzibar wanauchumi unaopaa kumbe umaskini umewavuruga mpaka uvunguni.
 
Tatizo sio Zanzibar ,mi huwaga najiuliza Tanganyika ingelikuwaje kama si huu Muungano ambao wanaung'ang'ania ,utafikiri hapa tulipo wanataka kuzama na kuogelea awajui.

maana ukiipima Zanzibar tokea na kabla ya Uhuru kulikuwa na amendeleo yanayoonekana ,historia inatwambia ni nchi ya mwanzo kuwa na umeme unaochukua radius ya 5Km hata uingereza walikuwa hawaipati Zanzibar ,pia tarehe zinatuambia Zanzibar ilikuwa inategemewa katika kutoa misaada kuziokoa nchi flani flani za Wazungu ikiwemo Denmark na baadhi ya Scandnavian wakati huo.Zanzibar ni nchi ya mwanzo kuwa na Tv ya rangi hapa Afrika kama haitoshi gari ya mwanzo kunguruma kule Kuwait inasemekana ilitoka Zanzibar na wameiweka kwenye museum yao.
Halafu tunaposema Zanzibar jaribuni kutafuta mipaka yake kwenye 1880 ,baba yenu wa Taifa hata hajajulikana kama atazaliwa na wengi wa wazee wenu walikuwa bado wapo kwenye misitu ya Congo na Zaire wakitembea na mishale migongoni wakiwinda ngulewe nchanga yaani hata hawajaiona wala hawajui bahari ni kitu gani.Leo hii mmejua kuvaa suruali na tai mnainyanyasa Zanzibar.
Ila mimi siwashangai maana mnatoka mbali sana na mmefika mjini.

Inawezekana ukawa sahihi lakini kumbuka "Kuwa wa kwanza si tatizo, ishu ni kuendelea kubaki wa kwanza"
 
..huku bara wengi tumeoleana ktk dini hizi mbili.

..familia na koo nyingi sana zimegawanyika baina ya dini mbili kubwa.

..udini uliletwa na mwanasiasa mmoja ambaye alikuwa hana njia ya kujihakikishia usalama wa kisiasa kwa kutumia kabila, badala yake akaona atumie Dini.
 
Maneno sawia kabisa Ally Saleh Alberto. Watanganika wametudumaza sana kimaendeleo.

Ila mimi naona bila Muungano Zanzibar ka maana ya Unguja na Pemba ingekuwa mbali sana. Ila huku Tanganyika ingekuwa vita kali sana ya UDINI. Mimi naona Wakatoliki wangejitwalia Tanganyika na kusababisha vita baina ya madhehebu na madhehebu au hata dini kwa dini kwa jinsi mbegu hizi za chuki za kidini zilivoshamiri.

Hivi waislamu kweli wasingejitwalia Zanzibar? Kumbuka yule jamaa aliyewekwa ndani na polisi kwa vile tu amekula hadharani wakati wa mwezi mtukufu wa ramadhani.
 
Hoja za namna hii ni za uchochezi na zinahatarisha muungano wetu. Swali hilo ni sawa na mtu kujiuliza "Hivi mimi ningezaliwa Ulaya ningekuwaje?
Tutafute hoja zingine za msingi.
Unaweza ukawa uko sahihi, lakini siku zote ukiogopa kujadili kitu kwa vile tu kinakusumbua kwa namna moja au nyingine, hayo mashaka yako utakuja kuyaweka kwenye matetndo na ikawa tooooo late. Is better you discuss so as you get to know all the merits and demerits..
 
Hoja za namna hii ni za uchochezi na zinahatarisha muungano wetu. Swali hilo ni sawa na mtu kujiuliza "Hivi mimi ningezaliwa Ulaya ningekuwaje?
Tutafute hoja zingine za msingi.
Ndugu Rumenyela atuwezi kuishi kama wanyama ,majadiliano ndio yanayotupelekea kuona nini ,wapi kumekosewa na nini kifanywage ili kuendeleza kile tunachokiona kina manufaa na sisi na kusimamisha kile kisicho na manufaa.

Wanasema majadiliano si vita ,ila huweza kuwa makali na yenye majigambo kwa kila upande na mijicho watu kutoleana ,ila wale wenye roho nyepesi kama wewe wanaweza kushikwa na woga na kushindwa kutegua bomu.

Aafu watu kama nyinyi mkiwekwa kwenye ghala la silaha mnaweza kusababisha milipuko kwa kutetemeka mikono mnapohandle mabomu,kuwa mvumilivu,kuwa m'bunifu na kuwa shujaa katika kuendeleza na kujenga hoja ,usiwe mwepesi goigoi na mwoga na haraka kutafuta mafichi kwani mficha uchi hazai labda akibakwa na ndio hapa tulipo WaTanganyika tumewabaka lazima watapata mimba tu.
 
Hoja za namna hii ni za uchochezi na zinahatarisha muungano wetu. Swali hilo ni sawa na mtu kujiuliza "Hivi mimi ningezaliwa Ulaya ningekuwaje?
"Mficha maradhi kifo humuumbua"

Ukweli ni kuwa kuna mambo tukiyanyamazia ilhali kuna watu wana info zaidi tutajikuta tunajisemea 'heri tungeyaongelea mapema'.

Just think of it!
 
maneno sawia kabisa ally saleh alberto. Watanganika wametudumaza sana kimaendeleo.

Ila mimi naona bila muungano zanzibar ka maana ya unguja na pemba ingekuwa mbali sana. Ila huku tanganyika ingekuwa vita kali sana ya udini. Mimi naona wakatoliki wangejitwalia tanganyika na kusababisha vita baina ya madhehebu na madhehebu au hata dini kwa dini kwa jinsi mbegu hizi za chuki za kidini zilivoshamiri.

kama kungekuwepo na vita za kidini, zanzibar wasaidia vipi??? Kwa kweli hakuna cha maana wanachokifanya ndani ya muungano zaidi ya sisi kujipendekeza ili tuonekana na jumuiya za kimataifa kuwa tunajali undugu na tulisaidia sana mataifa ya kimagharibi kuenea kwa ukomunisti.
 
Kikwete katika ilani ya uchaguzi mwaka 2010 ukitoa ahadi ya kuvunja muungano kura yangu unayo na watanzania kibao watakupigia kura lakini kwa masharti ya kuwatimua wapemba wote walioko huku Tanzania bara.
 
Back
Top Bottom