Hivi ya BALALI yameishia wapi??

Mzee wa Gumzo

Senior Member
Apr 21, 2008
197
5
Kila uchwao maswali mengi hujipanga kichwani mwangu mzee wa gumzo lakini huwa sipati majibu.

Jamani naomba tusaidiane hili la balali,si mnamkumbuka yule gavana wa benki kuu ya tanzania aliyepewa nafasi hiyo akitokea (kuazimwa)IFM?.

Baada ya kuibuka kwa sakata la EPA na rais kumvua ugavana tulitarajia kuona kasi,hari na nguvu mpya katika kumkamata balali na kumfikisha mbele ya pilato kama shahidi wa kwanza na muhimu katika uporaji wa mabilioni ya wadanganyika.

Lakini mpaka leo kimyaaaa!.Hatusikii chochote kuhusu mtu huyu.tuliambiwa alikuwa marekani anatibiwa lakini mpaka leo?

Hivi kwa ishu nyeti kama hii mpaka leo balali anavinjari tu mitaani?Tunahitaji nini kumkamata? au tunaogopa nini?au niseme watawala wetu wangwaya nini kumleta balali mbele ya mkono wa sheria???

Mimi wala sielewi,labda nyiye wadanganyika wenzangu mnajua zaidi yangu!haki ya nani hii nchi!
Uwanja wenu waungwana
 
Kila uchwao maswali mengi hujipanga kichwani mwangu mzee wa gumzo lakini huwa sipati majibu.


Mzee wa gumzo,

Utajiuruza sana na hutopata jibu, nasema hivyo kwa sababu moja kubwa. Hujui kuwa sisi akina sisiemu tulichukua pesa nyingi kutoka BOTI kwa ajiri ya kampeni za uchanguzi, na siri hizi zote Balala anazifahamu. Kwa hiyo inabidi mtu huyu sisi sisiemu tumlinde sana pamoja na kuwa amechota mabilioni ya vijisenti vya wananchi
 
Back
Top Bottom