Hivi weupe ndio urembo au?

Waarabu na mhindi wenyewe wanajichubua tu. Tena mwarabu ukimwambia u look like white anafurahi sana.

Ni kweli....nilionaga documentary moja hivi kwenye BBC wakionyesha waarab na wahindi wanavyojichubua kutaka kufanana na wazungu.
 
Ndiyo, kwenye jamii nyingi, hususan za watu weusi [walio na asili ya Afrika] rangi nyeupe ya ngozi huhusishwa na urembo.

Naamini ni ukweli ambao watu wengi hatuupendi, lakini ndo hivyo tena. Ukweli mara nyingi huwa ni mchungu na tulio wengi huwa tunajitahidi kuukataa waziwazi.

Hapo juu umezungumzia watu kujichubua ili kujibadili rangi ya ngozi na wawe weupe zaidi. Vipi kuhusu nywele bandia zilizonyooka? Ina maana nywele asilia za kipilipili ni mbaya, siyo?

Na vipi kuhusu majina ya kigeni siku hizi?

Unakuta mtu anaitwa Anthony Francis wakati baba ni Mgogo na mama ni Mnyiramba!

Au Maxwell John wakati baba ni Mmakonde na mama ni Mzaramo!

Hiyo mifano inanileta kwenye hoja ya kuhusisha Uafrika na uduni na Uzungu na ubora.

Hata watu wenye tabia za kishenzi huwa tunawaita 'waswahili'. Halafu tabia flani flani zinazoonekana au kudhaniwa kuwa ni za kistaarabu ndo zinaonekana ni za 'kizungu'.

Ni ndivyo tulivyo tu.
Hata hivyo uafrika una UDUNI na UDHAIFU mkubwa kulinganisha na uzungu.

Sisi tupo tupo tu, na uduni, ujinga na udhaifu wetu ulianza kuanzia kwa mababu zetu

Ninathubutu kusema walikuwa hovyo na goi goi kabisa.

Jamii kuwa dominated na jamii nyingine kiutamaduni, kiuchumi na kiteknolojia ni ushahidi kuwa jamii hiyo ni Dhaifu na ya hovyo.

Sisi watu weusi hatuna ubabe wowote kwa watu weupe hasa wazungu.

Hata kama inauma ndivyo ilivyo.

Wabillah Tawfiq.
 
Chungu lakin dahawa
 
Kwetu usukumani weupe kwa mwanamke ni dili hata dau linapanda.

Sent from my TECNO-W3LTE using JamiiForums mobile app
 
Ni kweli....nilionaga documentary moja hivi kwenye BBC wakionyesha waarab na wahindi wanavyojichubua kutaka kufanana na wazungu.

Acha tu wazungu wenyewe nikiwa angalia huo weupe wao naona ni kama wako na abnormalities sijui watu wanaupendea nini huo weupe. Kwanza wanazeeka haraka sana
 
Acha tu wazungu wenyewe nikiwa angalia huo weupe wao naona ni kama wako na abnormalities sijui watu wanaupendea nini huo weupe. Kwanza wanazeeka haraka sana

Wenzako wasijua hivyo wanaulilia huo weupe, mpaka kufanya madada zetu kujichubua na kuota ndevu za kujitakia.
 
Siku hizi kuna hadi Herbal lightening cream,yaani wamejua serikali inapinga kwasababu ya madhara ya kiafya sasa wanakuwekea picha au hata kutumia papai na parachichi na ndani kuna hydroquinone inayokuchubua.
Tatizo letu ni kulazimisha vitu jamani,mwanaume kama anavutiwa na weupe muachie huyo mwanaume weupe waliozaliwa hivyo,gharama ya kujichubua na matokeo ya hizo kemikali hakuna mwanaume mwenye thamani hiyo. Si hawa wa sayari hii.Kesho hushindwi kumkuta na baamedi mweusi.

brain is the beautiful part of the body.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom