Hivi Wenzangu huwa mnakula vyakula Gani?

Hivi Wenzangu huwa mnakula vyakula Gani?

We Jamaa; ina maana hauyajui hata yale matunda pori? Matunda ya Aina aina yapo ni mengi mno huko maporini ushindwe wewe mwenyewe. Huko mjini mmekomalia eti maembe, mananasi, machungwa na machenza ambayo hustawishwa katika mashamba tena kwa kutumia viuatilifu (dawa za kuua wadudu).
Matunda pori hayaguswi na kemikali yoyote ile e.g. Ubuyu; Ukwaju, Furu, Majumbau, Mabungobungo, n.k. ukiyala hayo unakula kitu OG.
Arf huwez amin mm sipo mjini naishi maporin huku kwenda mjini tu natumia Tsh 15k
 
Maharage waweza yabadilisha na dengu,choroko,kunde,njugu mawe mbona mboga nyingi sana,Kuna kisamvu hapo,mboga nyanya,mboga mayai...kifupi wewe mvivu tuu wa kufikiri vyakula ila vipo vingi sana
 
Kilicho kuchosha wewe ni repetition siyo chakula chenyewe, jaribu kubadilisha style ya upishi.

Ongeza variety ya vyakula vya wanga, mboga na legumes kama dengu, choroko, mbaazi na kunde.
 
Mkuu hivyo vyakula umevitaja ulaya bei ghali sana ispokuwa viazi ulaya. Dagaa kilo tu ni laki na nusu hadi laki mbili na ni snacks za mbwa. Samaki, unga, viaz vitamu na mboga za majani bei yake imechangamka.
Sasa mim bei ya ulaya inanihusu nn Mkuu šŸ˜‚

Kwanza Sina Mpango wa kwenda huko ulaya nabaki zangu kukomaa hapa hapa mpijimagoe
 
Umeoa mkuu? Ngoja waje waliooa wakupe uzoefu wa kula mboga moja miaka kwa miaka. Hao ndio wanafaa kukushauri.

Mimi kama Mwaisa nilitaka kukushauri ule Kitimoto. Haijawahi kuboa
Kitimoto utamla kila siku, hakinai?

Mi nilichoamini hakikinaishi haraka ni samaki aina ya sato ama perege, waweza kula mfulilizo kama kitoweo mwezi mzima na usikinaishwe.
 
Arf huwez amin mm sipo mjini naishi maporin huku kwenda mjini tu natumia Tsh 15k
Basi bro. kula vile vitu vya asili na utashangaa hutokaa usikie vinakuchosha i.e Vinakukifu. e.g. Kula karanga, kunde, dengu (isiyokobolewa), maboga ya kuchemsha na tui la nazi, mtama mweupe (tena usiukoboe), Ugali wa dona, Chai ya mchaichai(Lemon grass) yenye limao na tangawizi, magimbi yakuchemshwa, delega, mnafu n.k. n.k. Habari ya Bp; Diabetes utasikia kwa wenzio.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom