Hivi Wazungu wana makabila?

Sema zamani inawezekana zamani na wenyewe walikuwa na makabila ila kwa sasa hamna kama huku Tanzania kiswahili kinavyoharibu au kuhua lugha za asili,,,, watu wengi kwa sasa kwa mfano Tanzania wanazaliwa hawajui lugha zao za asili
 
Nadhani uko sahihi. Nimejaribu kusoma hii link. Ni kama ulivyoongea.
whatever happened to european tribes?
 
Yalikuwepo ila kwa sababu ya muingiliano sana wanaonekana kitu kimoja, mfano Tanzania watoto wanaozaliwa wanakielewa zaidi Kiswahili kuliko lugha za asili, baba msukuma kamwoa mchaga sasa hapo mtoto ataishia kuzungumza Kiswahili, sasa wenzetu hizo muingiliano ina miaka hata maelfu
 
Labda kwa zamani ila wenzetu wameacha tamaduni ya majina ya ukoo africa ukimwambia mtu full name yako bila mwakifamba shayo bado ujamaliza kuna kipindi cv kuna mpk kabila mzungu izo waliweza mapema tuitane na vyetu vyetu viwe na majina peter frank basi lkn utasikia mtu ajalizika we peter frank wa wap
 

Ubeligiji kuna flemish and walloon. Hii ni kulingana na lugha wanayo ongea. Flemish - dutch speeking and walloon - french speeking.
 
Ukiwa London utasikia accent yao ni tofauti na mtu wa York. Mtu wa Liverpool akiongea tofauti na mtu wa Birmingham. Kuna accent nyingine kama za New Castle unaweza ukatoka kapa.
Kama makabila yao unayajua tunaomba uyataje sio kutupa maelenzo ya rafudhi zao kwamfano hapa tanzania tuna wakara wako kisiwa cha ukerewe wanyambo wako karangwe wapare Wapo Kilimanjaro nk
 
mmmh!!!! "Mungu ibariki Tanzania na watu wake"
 
hahahaha!!!!!!!! hi ni Tanzania.
 
Makabila wanayo ila wao walijitaidi kwa watu wa jamii moja kuunda taifa mfano taifa mfano uholanzi, sweden na ureno japo kuna mataifa mengine yenyewe yaliundwa kwa ndoa za watoto wa kifalme na kuwa na taifa moja kama spain ilivyo ni muunganiko wa wajamii( kabila) ya kubwa wa spain , basque, catalonia, na kila sehemu wana lugha yao na tamaduni zao japo lugha kuu ni ki spanish vivyo hivyo kwa switzerland muunganiko wa jamii za kifaransa , kiitalia, kigerman , ki roman ambao n sawa na makabila tu kwa kwao kwaio kila canton (state)(mkoa) wana lugha yao na tamaduni zao.
 
Hawana Makabila, ukiangalia nchi zao zimeundwa kutokana na ufalme wa eneo husika.

Mfano Belgium, France, UK, Holland, Spain n.k pia ukiangalia nchi zao nyingi ni ndogo kuliko mikoa ya Tanzania. Mfano San Marino in Km2 61, Lienchtenstein ina km2 160, Malta ila Km2 316. Dodoma pekee in km2 2,576.

Ina maana kama wazungu wasingeigawa kwa namna walivyoigawa, Mikoa mingi Tanzania ingekuwa nchi.
 
Reactions: JMF
Hakuna nchi ambayo haina au haikua na makabila.tatizo ni kwamba wenzetu historia yao inaanza karne nyingi zlizopita wakat uku kwetu ni juzi tu miaka ya karibuni.Na ata sisi miaka 500 ijayo aya makabila ya leo yatakua yamefutika yote kitakachobaki ni lugha ya kiswaili kama lugha rasmi na wakati huo inawezekana hii mikoa ikawa ni mikoa yenye serikali zinazojitegemea na kutengeneza nchi moja yenye majimbo kamili yanayounganishwa na lugha 1 ya kiswaili.aya makabila mengi unayoyaona leo tanzania ni watu waliotoka uko nchi zingine wakaamia hapa wakatengeneza lugha na wengine walikuja na baadhi ya maneno na wakazaana wao kwa wao had kabila likakomaa kwenye eneo walikofikia lakin kwasababu sasa kuna mwingiliano mkubwa na makabila mengine nakukua kwa lugha ya kiswail ni hakika uko badae nasisi huu msamiati wa makabila utakua haupo.
 
Reactions: JMF
Huyu jamaa anayejiita padri ni mpumbavu kupindukia yaan anaweza kuwa mpumbavu namba moja humu JF
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…