Hivi Wazungu wana makabila?

Ni swali zuri sana kwani hata mimi sina huo,sie wengine hatujawahi hata kupanda ndege
 
Padri mcharo,niah said. mataifa yanayounganisha united kingdom ni madogo kuliko mkoa wa mbeya kabla haujazaa songwe au arusha kabla haijazaa manyara kwa hiyo muelewe kuwa hizo ni kabila japo zina stutus ya taifa.


Nimeishi Amsterdam (Uholanzi) miaka 7 wakati nachukua degree yangu ya Theology.
Nimepata Upadri nikaenda kuishi Cyprus miezi 3, Catalonia mwezi mmoja, Turin Italy mwaka mzima..
Sijawahi kusikia wala kuona makabila Ulaya...
Ukinipa mfano halisi nakunya hapa mbele ya duka, sokoni Kariakoo
 
data asante kunisaidia. Makabila yapo in form of dialects.


Mamdogo niah mbona unani aibisha hivi mchuchu...
Unasema amekusaidia wakati mshikaji amepigilia msumari na kupinga kuwa hakuna makabila Ulaya...
Ama hujui maana ya neno hamna. Hebu soma tena comment ya mchizi..


Anyway kurudi kwa topic..
Makabila hamna ulaya..
 
Hata tz miaka 300 ijayo hakutakuwa na kabila labda machache sana hususani maeneo ambayo hayafikiki. Cheki dsm jinsi wazaramo wanavopotea na kuwa watanzania wa dsm! Makabila ya mkoa wa pwani yatasambaratika karibu yote miaka 300 ijayo
 
Aiseeh Chief Engineer umeua hapo
 
Mwenye uelewa kutoka history anieleweshe kama wazungu wana makabila kama Tanzania tulivyo na makabila 120 or so! Na kama siyo, kwa nini hii imetokea Africa na siyo Ulaya/ Marekani/ Asia???


Wazungu walishafuta hayo mnayoyaita Makabila, ni lazima uelewe Kabila ni neno la dharau na maana yake ni mtu ambaye hajatastaarabika bado, yaani hajaweza kujenga Taifa, na ndiyo maana neno Kabila hutumika Afrika Kusini kwa Sahara, native Americans, aborigines hao ndiyo Wazungu hutumia neno Kabila lkn wengine wote walishafuta!
Isitoshe Tanzania haina Makabila 120 kama mnavyoanini na hayo yote unayoyaita Makabila Tanzania yalianzishwa na Wazungu/ Waarabu kabla ya Wageni kuja kwa mfano kulikuwa hakuna Wanyamwezi, Wahaya, Wagogo, Wachaga n.k. kama tuwajuavyo leo hii!

Hivyo neno Kabila ni neno la dharau kwa Mwafrika kama vile nigger tu!
 
Kabila ni kundi la watu lenye uhusiano wa damu au kwa kuoana.

Halafu unatakiwa utofautishe kati kati ya jimbo(state) na nchi(country). Kilichofanyika ujerman na italia ni muunganiko wa majimbo na si nchi.

Ili kujibu vizuri swali la mleta uzi tunatakiwa tutumie dhana/maana ya nchi ambayo ndani yake kuna makabila mengi ambayo yanaunganishwa na lugha moja ya nchi(taifa).
 
Padri mcharo,niah said. mataifa yanayounganisha united kingdom ni madogo kuliko mkoa wa mbeya kabla haujazaa songwe au arusha kabla haijazaa manyara kwa hiyo muelewe kuwa hizo ni kabila japo zina stutus ya taifa.
Wewe UK ni kubwa kuliko ulivyohadithiwa
 
Sasa kama hawana makabila ni kwa nini wana msamiati wa tribe.... Ifike mahali wazungu waache kujipendekeza..
Labda waliuunda huu msamiati kwa ajili yetu sisi wenye hayo makabila,
By the way kama wana makabila je wana kilugha cha hayo makabila tofauti na Lugha yao ya Taifa?
 
Hata tz miaka 300 ijayo hakutakuwa na kabila labda machache sana hususani maeneo ambayo hayafikiki. Cheki dsm jinsi wazaramo wanavopotea na kuwa watanzania wa dsm! Makabila ya mkoa wa pwani yatasambaratika karibu yote miaka 300 ijayo
Mkuu fanya simpo math tu,
wanaochangia uzi huu, wangapi wanaweza onge lugha ya mabila yao vizuri, je watoto wao itakuwaje, watoto wa watoto wao.............
Kwanya siku hizi kila mtu anataka apeleke mtoto wake english midium sijui international, na sio kijijini kujifunya kilugha.......
Effect ya hii ishaonekana miaka michache tu ya utaifa wetu (50+years)
Sasa next 120 years itakuwaje.... Tz yote itakuwa ni mjini........ Hakuna makabila ya kuongea labda kama historia tu kuwa kulikuwa kuna wanyakyUsa........
 
Mimi ni mkatoliki ninayeijuwa vizuri system ya kanisa,

Kwanza kwenye mfumo wa kanisa katoliki maelezo uliyoyatowa hapo utachekwa huwezi kwenda kuinjilisha huko

Kwanza ulipata upadrisho lini? Na uko chini ya jimbo gani? Na je unahudumu shirika gani?
 
Mwenye uelewa kutoka history anieleweshe kama wazungu wana makabila kama Tanzania tulivyo na makabila 120 or so! Na kama siyo, kwa nini hii imetokea Africa na siyo Ulaya/ Marekani/ Asia???
Kuna watu wanaitwa wakalunya na wabastia huko Spain. Hao ni zaidivya Wajaluo na Wakikuyu
 
Niah, asante kwa jbu lako. Ebu angalia link hii. Nimejaribu kutafuta jibu, sijui kama liko sahihi
whatever happened to european tribes?
 

Kwanini watu wa Caralunya ni tofauti na wa Madrid au Bilbao?
 
Padri kama unasema kweli , basi uko sahihi. Soma link hii utupe mwanga zaidi.
whatever happened to european tribes?
 
Kuna Uzi uliuleta hapa kuwa una miaka 26!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…