Ingawa mmeo ni msiba na mbwaa usiwahukumu wanaume wote. Kama unayosema ni kweli basi mmeo ni mtu wa kuogopwa kuliko hata ukoma na ukimwi. Amelewa chupi kiasi cha kushindwa hata kujijua kama usemayo ni kweli. Kazi ni kwako kuchagua kusuka au kunyoa maana ameishatenda mengi yanayohitaji adhabu ambayo binadamu hawezi kuibuni. Kama unaona ana kuzuia kwenda kumtembelea kwanini usichukue watoto wake ukaenda kule kwa nguvu tena bila kumtaarifu ili ugundue kinachomfanya akuzuie. Uhitaji kuomba ruhusa kwenda kumuona mumeo wala watoto kwenda kumuona baba yao. Nadhani heshima na upole wako anavichukulia kama ujinga na woga kiasi cha kukuwekea masharti ya kipumbavu.Wewe naye ni mwili mmoja. Pia jitahidi uende mahakamani kutetea haki za watoto wako. Maana kama anazaa hovyo hovyo kama panya siku ya kufa utajikuta una utitiri wa watoto walio wake na wasio wake. Na kama utasema utumie kipimo cha DNA bado ni upotezaji pesa. Chukua hatua mapema. Kama utaona migongano haifai unaweza kuamua kuanza maisha yako na watoto wako na Mungu atakubarikini.
Huna mume hapo dada (pole kwa makavu ya uso, ndo dawa itakayokuponya).
1 huruhusiwi kumtembelea wewe wala watoto
2 haji tena kuwaona
3 hatoi matumizi.
Ni nini kinachowafanya muendelee kuwa mke na mume?
Hatua ya kwanza ya divorce process ni kuishirikisha familia, then viongozi wa dini. Waeleze wazazi, kuwa hamna ushirikiano wowote, sio wa kihali wala wa kimali. Na muongee kuhusu child support. Weka mguu chini haswa, atakuwa.kawekwa kwenye rambo huyo. Akisikia unataka kumuacha ataanza kukimbizana na wewe utashangaa.
Kujibu swali lako, sio wanaume wote wako hivyo. Huyo wako tu mwenye kichwa kama doughnut tu.
Ukweli ni kuwa hapo huna mume.Ni jambo lisilopendeza kukuambia muachane lakini jikague unaweza kupata maradhi ya hisia!
"
Angalia faida na hasara za kuishi kwa aina hiyo.Jitahidi kutafuta suluhu kwa nguvu.
"
Waeleze wazazi na wengine walio karibu na ndoa yenu ili mpate ufumbuzi.
"
Ni lazima aitwe aeleze sababu.Akikataa huyo hana maana na hataki suluhu.
"
Hapo unaweza kuamua vinginevyo!
KHEE!
mamii cha kufia nini?
cha kufia nini mpenzi wangu!
hebu endelea na maisha yako kwanza bora kama mpo miji tofauti na anavokukataza usiende anakuepusha na mengi sana mpenzi wangu!AKUWACHE UPUMUWEE!
mume wa aina hii hapaswi kujumuisha wanaume wote kuwa wanafanana!
kimsingi baki mwenyewe lea watoto wako,wawili tuuu na una kazi!FUNGA MKANDA JIKAZE NYANYUKA PIGANIA FUTURE YA WANAO!
mume mjaa laana hvo si mume ati!
Asante sana. Sijawahi kushitaki upande wowote ingawa mwenye macho haambiwi tazama. Wanajionea wenyewe