Hivi wananchi weliowekeza kwenye Bureau de Change hatima iko he!!

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
10,319
2,000
Nawafikiria walioweka nyumba zao wakachukua mikopo Benki wakafungua Maduka ya kubadilisha Fedha za kigeni

Nadhani wataangaliwa wasiumie!!
Kwaresma njema

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi ni taratibu gani hasa za kisheria zilizokiukwa mpaka kufutiwa leseni na sio hata faini kama adhabu ya faini ipo kwenye sheria?
 
Isanga family

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
7,703
2,000
Washapoteza maana hela walizozikuta ziwe shilingi au dollar wamechukua walioumia ni wengi sana hapo,
 
OIL CHAFU

JF-Expert Member
Jun 8, 2012
984
1,000
Baada ya Bureau de change kuvamiwa na kuporwa hela zao nawaza Hivi kuna siku watakuja huku kwetu tuliolima nyanya na matikiti watuvamie wanyang'anye matikiti yetu
 
Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
10,319
2,000
Baada ya Bureau de change kuvamiwa na kuporwa hela zao nawaza Hivi kuna siku watakuja huku kwetu tuliolima nyanya na matikiti watuvamie wanyang'anye matikiti yetu
Ndio, kwani kwa sasa nasikia kuwa wafuga kuku wote wenye kuku katika batches zote wanaofikia 1000+ wajiandikishe! Kwa nini? Bado hawafahamu!
 
Pohamba

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
23,522
2,000
Kizazi Cha Kambarage kimerudi Mamlakani
Ambao hamkuwepo muone 'Nchi ya asali Na Maziwa' mliokuwa mnasimuliwa Kwenye vitabu vya ' TANU YAJENGA NCHI'

Baba Na Babu zetu ilifikia hatua wanaenda kutupa Fedha zao halali baharini wengine Kuzichoma Moto kwa Kuwa ukikutwa Na kiasi Fulani Cha Fedha Nyumbani kwako Ni Kama umekutwa Na Fuvu la Binadamu

Ukienda kuomba kubadili Fedha zako kupata Fedha Za Kigeni ilikuwa ngumu Kuliko kupata dhamana ya kesi ya Jinai

Wenye Biashara Za Maduka ya Kubadilishia Fedha wamfanyiwa ya Azimio la Arusha kuporwa mali zao mchana kweupe
 
bachelor sugu

JF-Expert Member
Jan 30, 2018
2,673

Umenikumbusha story ya mzee wangu aliyonisimulia kuwa alilazimika kwenda kutupa Mercury yake ziwani aliyoinunua Congo baada ya kukosa namna ya kuificha mpaka keaho ameishia kujuta tu na kulaani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom