Hivi, wadau hii imekaaje?

doppla2

JF-Expert Member
Jun 16, 2014
1,314
1,366
Ama kweli maisha ni kuchagua
Kuna jambo nimeliona chini ya jua, kwangu naliita ni ubatili na kujilisha upepo

Unakuta mmezaliwa sita ndani ya familia
Wote mmelelewa malezi sawa katika mazingira sawa. Cha ajabu mmoja ndo anatokoea kuwa mwajibikaji

Anapenda kujituma, Mwenye bidii na
Anajitoa Sana kwa mambo ya wenzake

Ila wengine, wao ni much knower....
Wabinafsi , wapenda bata

Sasa Kama mjuavyo kwenye issue za familia majukumu ndo wimbo wa familia

Kwa mtego him, yule ambaye ana sifa ya uwajibikaji anajikuta zigo limemuangukia.

Masikni ya Mungu, anajitahidi kwa mengi ila progress yake binafsi haionekani coz kingi amewekeza kwa familia na ndgu zake

Ila wale wala bata coz ni wabinafsi chochote wanachofanya ni kwa maslahi yao binafisi, so in reality huonekana wana vitu tangible.

Mwisho wa siku uonekana wajanja na full dharau hata kwa ndgu yao mwajibikaji


So wadau kwenye maisha haya ipi ni philosophy nzuri kuamua kuiishi

Ujifanye mwajibikaji... Uambulie kutupiwa majukumu na lawama au uwe kauzu upambane na hali yako tu ???
 
Hahaaaa, siku hizi watu tunabana maisha tunawakaribia wazungu. Balancing equation / fifty fifty otherwise utumbuaji unaoendelea utakuta fixed asset = 0
 
pambana na hali kwanza, hali yako ikikaa sawa.. basi utaanza kuwajibika na kwa ndugu
 
Acha uzwazwa kijana!! Usikubali kuwa mshumaa unawaka wenzie wanapata nuru huku wewe unateketea
 
Ukitaka kusadia tumia akili usifanye majukumu ya mtu alie hai na yuko busy na bata

Saidia sana wale wasiojiweza na kweli wawe wanshida

Usisaidie kusomesha mtoto wa mtu alie hai na yuko busy na wanawake leo anaoa huyu kesho yule afu watoto wake asomeshi anasubiri mmsomeshe huyo mtoto apambane na mzazi wake

Kama ukitaka kufanya majumu ambayo sio yako kwa kiasi kikubwa unajitengenea umaskini WA real assets kabisa yaani
 
Back
Top Bottom