CCNP Engineer
JF-Expert Member
- Apr 13, 2017
- 463
- 1,299
Nimemaliza chuo mwaka juzi UDSM. Naishi hapa hapa Dar kwasababu nature ya field yangu kampuni nyingi ziko hapa mjini. Sina hata zaidi ya miaka miwili kitaa, ndio kwanza najipanga na life. Nimepanga chumba kimoja mtaani, hata kiwanja sina.
Kwa kifupi ni kuwa bado sijaseto vizuri na life langu binafsi. Kuna sehemu nimejishikiza wakati natafuta sehemu ya kudumu yenye masilahi. Cha ajabu ni kuwa tangu nimalize chuo na kujishikiza hapa nilipo, ndugu zangu wananiomba sana hela. Wananiomba mno, shangazi, shemeji, baba yangu mdogo, dada zangu.
Hapo sijagusia watu ambao ni compulsory kama mama yangu (huyu ni wajibu wangu)
Hapo sijagusia kuhusu mchumba wangu, mahitaji yake, na mpango wetu wa kufunga ndoa, majukumu ya familia.
Uwezo wa kumsaidia ndugu 10,000 au 30,000 ninao. Tatizo unakuta wote wanaomba kwa mpigo, kila mtu na shida yake. Shangazi leo kanipigia simu anaumwa, hana hela.
Baba yangu mdogo kanitumia sms kuwa nimmrushie 10,000 hana hela ya kula usiku huu nyumbani kwake.
Shemeji yangu kaniomba nimpe 50,000 amtumie mama yake mzazi kalazwa hospitali. Babu yangu (ana watoto na wajukuu wengi) kanitumia sms kuwa kaibiwa hela zote alipokua mwanza airport hivo hana hela ya matumizi. Mama yangu kanipigia simu anahitaji 25,000 ya kununulia cable ya TV.
Umeona hapo? Umsaidie nani umwache nani?
Hii imekaaje wadau, kiuchumi sipo vizuri lakini ndugu wanaiomba sana msaada wa pesa. Na ukiwaambia huna hela wanaona unawanyima tuu hela unapeleka wapi wakati uko bachelor, huna mke, huna mtoto.
Hawajui kuwa namie nina mipango yangu kimaisha. Najichanga nipate kiwanja, kujenga, hela ya kodi, mahari ya mchumba wangu. Hivi huu ndio utu uzima, ukoo wangu ni masikini sana ama mie naonekana spesho sana? Niwe nawajibuje ili waridhike wasije kunisusia kwenye matatizo yangu na harusi yangu mwakani?
Mdogo wenu CCNP