Hivi hii imekaaje wadau?

Lituye

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
1,862
5,680
Bunge hivi karibuni limefanya marekebisho ya sheria mbali mbali. Moja ya sheria hiyo ambayo ningependa kuijadili ni hii ambayo inakataza mtumishi wa serikali au familia yake, au taasisi yoyote ambayo ana maslahi nayo kuingia mkataba wa kibiashara na serikali au kuomba tenda yoyote.

Lakini cha ajabu ktk Siasa tunaona hali tofauti kabisa katika uteuzi wa viongozi wa serikali hiyo hiyo. Wapo viongozi wanateuliwa wakiwa ni ndugu au rafiki wa wanao wateua au marafiki wa watoto wao.

Je, hii sheria ina mantiki yoyote katika ujenzi wa wa taifa hili kiuchumi na kijamiii? Au itungwe sheria kuzuia viongozi wa kisasa kuteuana kirafiki?

Karibu kwa mjadala wenye tija.
 
Back
Top Bottom