Hivi vyeti vya walimu wa private schools kutakiwa halmashauri imekaaje

Nadhani wanataka kubaini wageni wanaofanya kazi bila vibali, maana ni wengi sana kwenye private sector
 
Upande wa science na mathematics, private wanachukua watu waliopiga A, B form six.
Na ndio maana wanawachukua wenyee degree ya uandisi na sio wenye degree ya Elimu.
Hapo vichwa vingi vitakatwa.
 
Uzuri ni kuwa kule top 10 wanaingia haohao mnaowasema wanafundishwa na walimu ambao hawana vigezo, na kule mkiani wanakaa ambao wanafundishwa na walimu mnaowaita wenye vigezo
Kw hiyo unataka kusemaje poyoyo wewe.serikali isiwasimamie huko kw sbbu ni shule binfsi.???!!
 
Juzi jamaa yangu ambaye mwalimu Wa English medium amesema jumatatu wapeleke vyeti original vya sekondari,degree na diploma kwani vinahitajika serikalini

Mwenye kujua dhumuni la agizo hili atujuze.

Asante!

Serikali ipo kwa ajili ya wananchi wake na ustawi wao. Taasisi zinazoanzishwa nchini zinaanzishwa kwa kufuata sheria zinazoruhusu uanzishwaji wake. Hakuna taasisi inayoanzishwa iwe juu ya sheria.

Kama sheria na taratibu zinataka kazi fulani mfano udaktari ufanywe na wenye taaluma hiyo, basis serikali ina wajibu kusimamia sheria hiyo.

Au muuzaji wa madawa nchini, yawe ya kilimo au mifugo, lazima awe na taaluma inayohitajika pasipo kujali umiliki wa drug stores.

Vivyo hivyo katika ualimu. Ualimu ni taaluma, hivyo wenye taaluma husika tu ndio wanaostahili kuwa walimu. Serikali ina wajibu wa kusimamia utekelezaji huu wa sheria pasipo kujali umiliki wa shule kwani shule binafsi zimesajiliwa kwa mujibu wa sheria na zinawajibika kutiina kufuata sheria na kanuni za usajili wao.

Huo ni utendaji tu wa kawaida wa serikali kama inavyotakiwa, usimamiaji sheria na kanuni.
 
Upande wa science na mathematics, private wanachukua watu waliopiga A, B form six.
Na ndio maana wanawachukua wenyee degree ya uandisi na sio wenye degree ya Elimu.
Hapo vichwa vingi vitakatwa.

Elimu ni taaluma. Kuna kufaulu mitihani na kuna kuelimika. Kufaulu mitihani sio lazima kuwe kuelimika.

Umeshawahi kujiuliza wale wanaopiga one Kali za kusimamiwa na kupewa malezi ya jicho kwa jicho wakiwa A level huwa wanakuwaje vyuo vikuu na katika maisha ya uwajibikaji duniani?

Tafakari!
 
Swala la uhakiki wa vyeti halina u privatell wala gvt maana kinachoangaliwa ni uhalali wa vyeti katika kutoa huduma nyeti kama elimu na Afya na nyinginezo.
Mbona kina bashite hawahakikiwi? Mbona Phd hazihakikiwi? Mimi ya kwangu ni ya maganda ya karanga lakini nashangaa wanatusahau. Mbona kwenye uhakiki wa silaha Phd walikwenda na bunduki zao 2 kiunoni??!
 
Unaongea kitu gani wewe...hata hufahamiki na hii verbal diarrhea yako
Sisi tuna muelewa hata ukikataa kuelewa ukweli utabaki hivyo huwezi kumpeleka mwanao kwenye shule ya masifuri na kulipa hela yako hizi shule zina jichuja zenyewe nguvu zielekezwe huku kwenye masifuri yapungue
 
Labda hapa wengi hamjui kama lengo ni kupata watu wanje mmesahau ma boss wako radhi wawafiche. Maana kuna company moja najua kabisa foreigners hawsaini daftar.

Kwahyo hata wakisema wapeleke vyeti watapeleka wale raia, maana sometimes ni relief kwa ma boss kwasababu wengine hata hela ya mifuko ya jamii na kodi hawapelekewi na wamerizika
 
Juzi jamaa yangu ambaye mwalimu Wa English medium amesema jumatatu wapeleke vyeti original vya sekondari,degree na diploma kwani vinahitajika serikalini

Mwenye kujua dhumuni la agizo hili atujuze.

Asante!
Huelewi kitu gani? Kuna taaluma ambazo zimewekewa viwango na wakati mwingine hata usajili. Ualimu, Udaktari, injinia, famasia, nk. Huwezi kujidai uko private wakati una vyeti fake.
 
Labda hapa wengi hamjui kama lengo ni kupata watu wanje mmesahau ma boss wako radhi wawafiche. Maana kuna company moja najua kabisa foreigners hawsaini daftar.

Kwahyo hata wakisema wapeleke vyeti watapeleka wale raia, maana sometimes ni relief kwa ma boss kwasababu wengine hata hela ya mifuko ya jamii na kodi hawapelekewi na wamerizika
Tafadhari! Usiseme kampuni fulani, tutajie jina ili JF ifanya kazi yake. Nchini kwaohawatutaki kwa nini hapa tuwafiche?
 
Dah, hapo jamaa yangu njaa iaterejea. Nilisoma na jamaa o level, ana uwezo mzuri sana wa Pcm, SHIDA alidisco udsm miaka ileee, kajikita private school km mwl mahili wa masomo hayo ya sayansi. Kwa hili SHIDA niona ileee yaja. Ila yupo vizuri balaa
 
Kw hiyo unataka kusemaje poyoyo wewe.serikali isiwasimamie huko kw sbbu ni shule binfsi.???!!
Kwa hiyo we unaona vizuri sana serikali kuwabana private huku shule za serikali zinaendelea kufanya vibaya, kwahiyo huo usinamizi ni kwa private pekee? Hapa hapakufai we endelea tu kumsaidia dadako kukatakata nyanya
 
Juzi jamaa yangu ambaye mwalimu Wa English medium amesema jumatatu wapeleke vyeti original vya sekondari,degree na diploma kwani vinahitajika serikalini

Mwenye kujua dhumuni la agizo hili atujuze.

Asante!
Mkuu ungejua kuwa hata private activities bado ziko chini ya uangalizi wa Serikali usingeuliza swali lako. Ndio maana hata ukianzisha Pharmacy au Bucha ya nyama wanakuja kukagua.
 
Kwa hiyo we unaona vizuri sana serikali kuwabana private huku shule za serikali zinaendelea kufanya vibaya, kwahiyo huo usinamizi ni kwa private pekee? Hapa hapakufai we endelea tu kumsaidia dadako kukatakata nyanya
Haha hahaaa.wewe ni mmoja kati ya hao wanaotakiwa kukaguliwa?!@
 
Inaweza kuwa wanadhibiti shule siziwekeze kwenye walimu wasio na sifa. Kwa upande mwingine wanaisaidia Loan board kupata pesa yao.
 
Back
Top Bottom