Hivi viwanja vya ndege vipi jamani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi viwanja vya ndege vipi jamani?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Mwanahisa, Jul 3, 2012.

 1. Mwanahisa

  Mwanahisa JF-Expert Member

  #1
  Jul 3, 2012
  Joined: Jun 29, 2012
  Messages: 1,397
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kwa wanauchumi, mnajua mchango wa usafiri wa Anga kwa uchumi wa nchi zetu,

  Chakustajabisha, Kiwanja cha JKNIA ndio kwanza kazi yakuvusha unga inashamiri ambayo haina tija kwa taifa.
  Mbona mambo ya msingi yasifanyike kama kuongeza miundombinu ya kisasa zaidi, ulinzi ikiwa kipaumbele?

  Huo wa KIA nao, ni kupakia wanyama wetu wa asili, wakati jirani hapo Kenya anajenga uwanja mpakani TAVETA ili watalii washukie hapo waende mlima KIlimanjaro, Kukwepa adha za umeme kukatika na jenereta kukosa mafuta.

  Huko jirani halali, Jomo Kenyatta IA wanaongeza terminal ya Greenfield, hapa nyumbani tunakazana na tender za kuchakachua nani apewe contract ya kupanua uwanja! na tuko kwenye jumuia ya Afrika mashariki kwa mwendo huu?
   
 2. k

  kijereshi JF-Expert Member

  #2
  Jul 6, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 257
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  It's so disheartening to the above said worse still viongozi wetu wanakazana kujenga another international airport B'moyo badala bila kuangalia umuhimu wa JKINA na jinsi ya kukiboresha kanda ya ziwa hawana airport ya kueleweka Mbeya nacho unaenda mwaka wa kumi songwe haijakamilika na sinahakika kama itakamilika hivi karibuni kwakifupi hatuna vipaumbele vinavyoeleweka viongozi wetu wake busy na kutorosha fedha ana kuzipeleka nje ya nchi
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Jul 6, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Mkubwa mleta mada, unachanganya mambo mawili:
  Kazi ya madawa ya kulevya inafanywa na watu wenye mkono uliofichama na si Mamlaka ya viwanja vya ndege, hali kadhalika ishu ya kusafirisha Twiga.
  Mamlaka isilaumiwe kwa mambo ambayo hayaihusu jamani. Viwanjani kuna watu wa idara ya Dawa za kulevya na wa Idara ya Veterinary, ambapo hao ni watu wa Wizara tofauti kabisa na Wizara ya Miundombinu, hivyo kuilaumu Mamlaka ya Viwanja ni makosa Live.
   
 4. Tripo9

  Tripo9 JF-Expert Member

  #4
  Jul 6, 2012
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 2,168
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Nimekua mfuatiliaji wa kimyakimya wa nyuzi mbalimali. Nimegundua mkuu PK ishu zozote zinazoibuliwa kuhusu viwaja vya ndege unazizima na kuwaonesha watoa mada hawana hoja. Hii ina impact kwenye threads zao kwa kua unakua kama ushafunga mjadala na hakuna cha kujadili.
  Usiwe kama msemaji wa uozo utokea ktk viwanja vyetu hivi vya ndege. Nini maana ya team work sasa kama watu wahusikao na kuibua madawa ya kulevya hawa work hand in hand na watu wa airport authority.
  Kwa mimi mwananchi wa kawaida najua tu airport kuna uozo. I dont freaking know the tiny details of vitengo pale airport. So changamoto zinapotolewa wahusika wenyewe ndo wajipange na kuondoa uozo.

  Kama mkuu PK nitakua nimekukwaza uniwie radhi
   
 5. Mwanahisa

  Mwanahisa JF-Expert Member

  #5
  Jul 7, 2012
  Joined: Jun 29, 2012
  Messages: 1,397
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  PK ni kweli inaonekana kama lawama, ila ukweli ni hoja tu, sorry to say am decoding the right signals to a wrong channel.
   
Loading...