hivi viboko mashuleni vinatusaidia kweli?

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,658
20,889
Najiuliza hili swali, mbona shule za international na maacademy hakuna viboko, au shule za wahindi na watu wanafaulu. hivi hakuna njia nyingine ya kuwaadabisha vijana wetu? mi naona viboko ni adhabu inayowafaa wanyama sio watu!
 
Nashauri viboko viendelee ili kuwaadabisha watoto watukutu kama Lulu!!
 
Viboko havisaidii, vinawafanya watoto wasipende shule. Vinawajenga wanafunzi kuwa na nidhamu ya uoga.
 
Viboko havisaidii, vinawafanya watoto wasipende shule. Vinawajenga wanafunzi kuwa na nidhamu ya uoga.
sure kabisa mtoto anajifunza ili awajibike lazima pawepo na adhabu vingenevyo hakuna kuwajibika
 
Ujinga wa mtoto /kijana umefungwa kwenye akili yake unaondolewa kwa viboko.
inamaana watoto wa shule za international au za kihindi au ulaya ni wajinga kwa sababu viboko havijaondoa ujinga wao?
 
hata Biblia inaruhusu viboko
sina shida ya mzazi kumchapa mtoto wake sababu tafiti zinasema ili adhabu iwe effective inategemea na anaye itoa, lakini kwa waalimu naona tunaharibu watoto. just imagine mwalimu katoka kukuchapa alafu anakufundisha muda huohuo au unategemea mtoto akamuombe msaada wa kimasomo! mwalimu ni rafiki lakini huku afrika especially TZ ni adui.
 
inamaana watoto wa shule za international au za kihindi au ulaya ni wajinga kwa sababu viboko havijaondoa ujinga wao?

Hakuna popote duniani kwenye nidhamu sahihi isiyotunzwa na ukali wa adhabu, hata mtoa mada hii angekuwa muuaji kama siyo ukali wa adhabu ya kuua ambayo ni kunyongwa. Ulaya hakuna nidhamu kabisa kama mtu unafikiri vizuri, mfano vijana wengi mmeharibika ukiwemo wewe ambaye unanakiri tu na kutoa mada, hivi sisi tuliochapwa viboko umeona nani anavaa surali mbele ya mama yake hali chupi yake ikionekana? hayo ni matokeo ya uhuru usiokuwa na mipaka na zaidi ya yote ni matokeo ya kuamini kuwa kila kitu cha ulaya ni kitu kizuri kwa mwafrika. Na kwa taarifa yako 95% ya wote walisoma International ni wavivu na wazembe popote walipo kwa kuwa shule hizo zina wafundisha watu mfumo wa maisha ya ulaya badala ya mfumo halisi wa maisha ya Tanzania.

Angalia mbona mmepiga kelele Cameroon alipokuja na hoja ya kuturudisha SODOMA NA GOMORA? Ikiwa kila kitokacho ulaya ni kizuri hapo je? Fikirini kwanza kabla ya kucopy na kupaste kwenye bongo zenu.JESHI LINA NIDHAMU KWA SABABU YA UKALI WA ADHABU BILA HIVYO PASINGETOSHA Utakuta mtu ana miaka 30 jeshini anaingia kijana ana miaka 25 lakini mwenye elimu na cheo ni lazima pasipo hiari wala mjadala apokee amri kutoka kwa huyu mjukuu na aitekeleze akibisha cha moto atakiona upo hapo mdogo wangu nimekuita mdogo wangu kutokana na mleta hoja anaonekana ni mwathirika wa kupenda vya ulaya.
 
Back
Top Bottom