Hivi unajua unaweza kutumia akili kidogo tu ukapata pesa nyingi?



Sent using Jamii Forums mobile app
 
DocJayGroup, Nilichogundua ni kuwa wewe una wivu mbaya sana na pia ni mchoyo wa maendelelo. Na pia moyo wako hupendi kuona watu wengine wakifanikiwa.

Mleta mada yeye kajaribu kushirikisha watu wengine mawazo mbalimbali ya kijasiriamali ila wewe unaanza kumponda na kumdharau, huku ukianza kujisifia, badala ya na wewe kuongezea uzoefu wako na mawazo katika biashara alizozitaja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilianza kwa uzuri kabisa. Mleta mada ndio kaanza dharau. Fuatilia mada tokea mwanzo utaona. Hakuna mtu anapenda mafanikio ya wengine kama mimi. Shida watu wanapenda kuambiwa maneno matamu tu. Mfano, kuambiwa utafanikiwa kwa kutumia akili kidogo sana. Kwenye biashara hakuna kutumia akili kidogo. Kama ingekuwa rahisi, kungekuwa na Reginald Mengi kibao Tz.

Mimi sijakuzuia, nilishasema uko huru kufuata maelezo ya mtoaji mada. Naomba tafadhali maneno yangu yote usiyazingatie kabisa. Ni dunia huru.

Lengo langu lilikuwa jema kabisa nilitaka kujenga mada vizuri zaidi ili iweze kusaidia watu kwa undani zaidi. Kwa kuwapatia watu njia za kufanikiwa wakishaanza biashara na kumudu vikwazo. Watu wajifunze kuchukua critics vizuri. Ila mtoa mada akaanza kinishambulia tu wakati mimi malengo yangu yalikuwa mazuri. Na ndio ikawa ugomvi ambao binafsi siupendi kabisa.
 
Hili mashine inafanya kazi gani boss

Sent using Jamii Forums mobile app
Unaziona hizi paving Blocks hapa chini mkuu



si unaziona zilivyo pendeza vizuri,sasa kabla ya kuwekwa hizo paving nyumba yeyote ile lazima hiyo mashine ipite kushindilia Udongo,ikiwashwa inatengeneza vibration inayosababisha udongo kushindilika vizuri,na baadae ndio hizi paving zinakujaja kuwekwa Juu.

Hiyo ni kazi 1 ya hiyo mashine japo zipo nyingi ila ktk hizo nyingi wateja wengi utaowapata ni wale wataokuja kutaka wakaitumie site ili badae waweke paving.

Ina hela sana hii mashine ni pesa hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…