Hivi unajua unaweza kutumia akili kidogo tu ukapata pesa nyingi?

Wale wanaobeza business models alizoleta Controla mlipaswa mlete na masuluhisho ya mambo yale mnayoona kuwa yatafanya biashara hizo zisitekelezeke.

Controla ametoa tu "...a tip of the iceberg" mambo mèngine yatampasa mtu husika atafiti zaidi namna ya ku-monetize hizo business models na kuziba loopholes.

Business models zote zina changamoto...zilitatuliwa na wahusika kadri zilivyojitokeza. Ukidai kuwa business model fulani haiwezekaniki kwa vile utapigwa na wateja au employees...then tafuta namna ya kuzuia huo upigaji...na business isonge mbele.
 
Kuna biashara moja
zile biashara za kukodisha CD uswahilini watu wanadharau ila zinatoa sana hela,biashara flan ya kilofa ila mpunga unaingia mno
Ni kweli ni nzuri ila hapa mtu aliye ajiriwa hawezi fanya hiyo biashara ya CD

kufatilia CD flani imetoka au haijatoka,kufatilia miendelezo ya CD yani ni ngumu

CD ni biashara inayomuhitaji muhusika BOSS full time awepo kazini ajue wateja wanataka nn

Kwa waajiriwa haiwafai hiii ila ni safi sanaa.
 
Ni kweli ni nzuri ila hapa mtu aliye ajiriwa hawezi fanya hiyo biashara ya CD

kufatilia CD flani imetoka au haijatoka,kufatilia miendelezo ya CD yani ni ngumu

CD ni biashara inayomuhitaji muhusika BOSS full time awepo kazini ajue wateja wanataka nn

Kwa waajiriwa haiwafai hiii ila ni safi sanaa.
Kwa waajiriwa ni kweli kuna ugumu mwingi sana,ila kwa vijana wasio na ajira hiyo kaz inawafaa
 
DocJayGroup, DocJayGroup kama mtu anakodishiwa TATA yenye thaman zaidi ya m80 kwa rejesho la 200k tena route za mipakani sembuse kifaa cha million 1 ndio unashangaa ..

Bajaji yenye thaman ya million 7 je ? Vip kuhusu boda boda yenye thamani ya 2m kwa rejesho la 10k .kwa mtazamo wako basi kusinge kuwa na biashara ya kukodisha vitu tena hivyo ambavyo ni rahisi kuhamishika.

Kuhusu kukodisha speakers ni biashara inayoingiza faida kubwa especialy vijijini maana huku harusi, sherehe disco vumbi zote tunawategemea wanaokodisha hivyo vifaa labda experience yako ktk biashara imeishia mjini .

Zaidi ya asilimia 50 ya wafanyabiasha wa pale ilala boma sokoni meza wanazotumia kufanya biashara hukodisha kwa watu 1000 per day. Na unakuta kunajamaa anameza zaidi ya 5

Jamaa yangu amekodisha kibanda kidogo cha chuma pale mwenge 3000 per day anauza vocha mpesa tigo pesa kwa mfanya biashara anaejielewa hawezi kimbia na kifaa akaiacha biashara yake.

Mimi kwa uelewa wangu hayo uliyoandika ni risks ambazo zinaweza kuikumba biashara yoyote wizi ni tatizo hata bank inayolindwa na askari inafika mahala wanaporwa sembuse wewe sijui mwenye duka linalolindwa na mzee mwenye miaka 70

Kuhusu mtoa mada CONTROLA nimpongeze tu kwa kutoa elimu nzuri na maelezo yaliyo nyooka, kwa mtu mwenye kuchukua maamuzi nadhan raman jamaa kasha ichora imebaki kufanya upembuzi yakinifu nijinsi gani uta manege risk ya ulichoamua kukifanya

Akili za kuambiwa changanya na zakwako aliwahi kusema j k kikwete

Sent using Jamii Forums mobile app
 
jooohs,
Hiyo mifano ya magari ya tshs 80 million kama Tata au Canter au coaster nilishasem sio mizuri kwa sababu kuna tofauti sana kati ya vyombo vya transport na vifaa katika hii list. Mimi mwenyewe niliwaambia nina kampuni ya tours na tunatumia landcruisers za 50 million tshs na kuendelea ambazo kampuni inakodisha kwa kampuni nyingine au nawapatia driver guides ambao wanazungusha wageni mbuga za wanyama.

Lakini kumbuka kampuni inafanya vetting ya uhakika sana kabla ya kumpatia mtu land cruiser. Mtu anafuatiliwa historia yake makazi yake, je ana historia ya udokozi na wizi au ni mwaminifu?, wazazi wake wako wapi? wanafanya nini?, ana familia manake mke na watoto?, je amejiaminisha na magari ya wengine tayari kabla ya magari yangu. Nk. Hiyo ndio process pia inatumika kumpa mtu bajaji, magari ya mizigo etc. Usipofanya hivyo eti ukampatia tu kila anayekuja kutaka gari lako unafikiria itakuwaje kwa Tz yetu?

Pia kwa kampuni yangu, gari hailali kabisa nje kama wageni wameshamaliza kazi. Gari ikiwa na wageni, inajulikana kabisa inalala wapi. Pia cruisers zote zina GPS tracking devices mbili ambazo madereva hawajui imewekwa wapi kwa gari. Kwa hio naomba muangalie tofauti ya process ya kukodisha magari kama Tata uliyoyataja na vyombo hivyo kama welders nk. Hivyo vyombo mfano mjini, utakodisha kwa waswahili wengi sana na utawajuaje? Na ukisema kitu cha milioni moja, milioni moja kuipoteza ni sawa? Kwani sio hela?

Nakubaliana nawe kuhusu kijijini. Kijijini kila mtu anamjua kila mtu. Hapo lazima biashara iwe nzuri. Na kufuatilia historia ya mtu kwa kijijini ni rahisi sababu watu sio wengi na wenye udanganyifu na uswahili, udokozi/ wizi wanafahamika kabisa ni wakina nani. Kwa hio mtu kama huyo akija au rafiki yake, au ndugu yake, unampiga chini tu akitaka kukodi equipment.

Hapa tunaongelea mijini sababu asilimia yetu kubwa ni mijini. Mimi ndio swali langu hilo. Majiji kukodisha hivyo vifaa hakika utalizwa tu. Naomba labda mtu aje na wazo lingine, lakini la kwako ndugu yangu bado halijatatua hii changamoto kabisa.

Risks zipo kila biashara, na kama nilivyosema ni muhimu kuzifahamu na kutafuta namna ya kuzikabili. Wizi upo kila sehemu, na ndio maana nimekutajia jinsi watu tunavyoukabili kwa kuwapatia watu magari ya thamani kubwa wayaendeshe. Pia kwa watu wenye maduka nk, wanaweka hatua muhimu kuzuia hilo. Lakini hizo idea za controla kwa mijini ni ngumu sana. Na sio sawa kuwaambia watu watafanikiwa kwa akili ndogo.

Hakuna biashara inayotumia akili ndogo. Mimi sikuwa na lengo baya tokea awali, nilitaka tubadilishane mawazo tu, ila controla akaanza kunishambulia na kujisifia sana wakati mimi najua kabisa wala hafanyi biashara yeyote. Ni mwandishi mzuri sana lakini. Ila sasa kuandika mada inayotoka kichwani, na kuandika mada mbayo mtu una experience nayo ni vitu viwili tofauti kabisa. Na jinsi mdada/ mmama alivyonishambulia, inaonyesha hana ujuzi kabisa wa biashara.
 
Back
Top Bottom