Hivi unajua unaweza kutumia akili kidogo tu ukapata pesa nyingi?

Nilitamani kukuandikia insha ndefu sana maana unaonekana bado sana ktk Biashara,Ila nataka kukwambia kitu kimoja cha muhimu sana katika ujasiriamali/biashara kwa ujumla

Tuna cheza na Hatari ila Mjasiriamali/Mfanyabiashara alie kwiva hujua namna ya kudeal na hizo HATARI.Hata forex ina kitu inaitwa STOP LOSS unaijua kazi yake hiyo kitu? huku kwenye biashara tuna STOP HASARA

Unataka kujua STOP HASARA inavyofanya kazi? Penda kujifunza halafu ingia Field halafu nimalizie kitu kimoja,Siandikagi vitu ambavyo nasikia sikia kwa watu au kwenye vipindi vya radio,ukiona nimeandika kitu ujue nimeshakifanya

kama sijakifanya huwa nafungaga bakuli langu,ndio mana sinaga thread bandika bandua na si kwamba kila ninavyoandika ninachofanya kinafanikiwa kuna vinavyo feli sana tu ila kamwe hutoniona nikileta Ushuhuda wa kufeli kwangu humu JF ila ktk

Ninavyovileta humu na kuviandikia Kama mtu akivifata Probability ya Kufanikiwa ni 81%,ukiona kina ugumu au hakiwezekani Fahamu tu kuwa Haukujipanga.

Mechi yyte ili utoe matokeo mazuri yakupasa umjue Mpinzani wako kajiandaaje,ana silaha gani kisha ndio uingie vitani,ukienda kichwa kichwa bila kujiandaa utarudi mikono kichwani.

kwenye biashara unatakiwa uwe na vitu vifuatavyo Taarifa sahihi,Mtaji,uzoefu,uthubutu. DocJayGroup
 
CONTROLA,
Umeandika post ndefu sana lakini Haujajibu Maswali Yangu Kabisa. Mtu anaweza kuwa na mtaji, na anaweza kuwa na uthubutu, lakini watu hapa nimeona wengi hawana uzoefu. Na ndio maana wanakubaliana tu na mawazo yako bila kuyafikiria kwa undani zaidi.

Uzoefu ndio huo mtu atakodisha vitu sijui majenereta na welder za mamilioni, halafu zitaibiwa. Atapata uzoefu na hassra kubwa hapo hapo.

Naomba unipatie jibu kuhusu mbinu. Tupatie mbinu 3 kwamba wewe unahakikisha vipi hivyo vitu vya mamilioni watu wakikodi wanavirudisha? Mfano ungeweza sema mtu akikodi mimi nampatia kijana wangu anaenda naye ili kusimamia hivyo vitu. Je huyo kijana anafanya kazi full time na unamlipa shs ngapi? Jenereta itasimamiwa vipi? Welda sawa, anaweza kuwa ni mchomeleaji. PA system anaweza kuwa fundi mitambo. Je vibanda portable unahakikisha vipi haviibiwi? Na kama ni vijana, unawalipaje ili wasiingiwe na tamaa wao wenyewe wakakuibia?

Umetoa mawazo, na unasema una uzoefu, basi naomba sasa utoe mawazo zaidi ya namna mtu atakavyoweza kufanikiwa dhidi ya vikwazo hivyo nilivyovitaja.
Hapa hatugombani, bali tunaelimishana.
 
CONTROLA,
Eti biashara mimi bado sana? Usinifurahishe. Nina lodge ya wageni. Nina kampuni ya utalii. Na studio ya media production. Na nina mpango wa kuanzisha kampuni ya ujenzi/ construction. Kwa hio usiseme eti sina uzoefu. Nimefanya business tokea 2003. Nimefanikiwa sehemu na sehemu, pia nimefeli sehemu na sehemu. Kufeli au kushindwa ndio kunakupa mafunzo na uzoefu.
 
CONTROLA,
Jambo muhimu sana kuhakikisha mtu unafanikiwa kwenye biashara yeyote ni kufanya risk analysis (udadisi wa vikwazo) kabla ya kuanza biashara, na kuweka mikakati na mipango mapema ya kukabiliana na vikwazo hivyo. Mtu usiruhusu vikwazo vikafanya usijaribu biashara, lakini ni muhimu kuweka mikakati mapema kuhakiki mtu hauangushwi na vikwazo hivyo.

Kwa Tz, kikwazo kikubwa katika uwekezaji ni wizi, udanganyifu, usanii nk. Hio itakuwa ni changamoto zaidi kwa mawazo uliyoyatoa ya kukodisha vitu vya thamani kwa watu mbalimbali.. watu ambao hawana uchungu na vitu hivyo sababu hawakuvilipia mamilioni kuvinunua.

Wana JF ni muhimu tusiwaelimishe upande mzuri tu wa uwekezaji kama ulivyofanya, bali pia wajue changamoto na namna ya kuzikabili. Na kusema mtu anaweza kutumia akili kidogo akafanikiwa kama ulivyoandika ni udanganyifu mtupu. Biashara lazima mtu aweke akili zote kwake.
 
Mashine ya kuchomelea si lazima use fundi

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna mafundi wengi wanajua kuchomelea, na hawana mashine zao binafsi. Ukiwa na mashine ya kuchomelea ya kukodi, watakuja kukodi. Suala kama nilivyosema ni uaminifu na mafundi wenyewe ndio tunawajua uswahili kibao.

Una wazo katika hilo? Manake namna ya kukodisha kwa mafundi na kuhakikisha hawaharibu mashine wala hawaichakachui, wala hawaiibi? Welda nzuri itakayokidhi mahitaji ya mafundi, ni shs milioni moja na kuendelea. Si chini ya hapo.

Ukisema fundi wako aende nayo, je anaeenda kuisimamia tu au anaenda na yeye kuchomelea? Kama ni fundi ndio anakodisha, ujue atataka achomelee yeye mwenyewe.
 
DocJayGroup, NAKUBALI

KIUHALISIA HIZI IDEAS WATALIA WENGI SANA NA KUMTUKANA MLETA MADA KIMOYOMOYO-
PINDI WATAPOPATA MISHAHARA YAO YA JANUARY AU MIEZI MINGINE NA KUKIMBILIA MADUKANI KUNUNUA Welding machines, Maspika NA Kutengenezesha makabati WAKIAMINI WATAKODISHA TU NA KUPATA HELA KINDEZINDEZI!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hio sawa. Fanya kama mwandishi alivyoshauri ila jua kwa asilimia kubwa, kama hautapata suluhisho ya hizo challenges nimezisema hapo LAZIMA MTAJI WAKO UTAUPOTEZA NA PIA BISHARA ITAFELI Tu. Simaanishi kuwa negative. Huo ni uhalisia tu. Mimi na experience kubwa tu katika kufanya investment Tanzania. Kwa hio sio kwamba nasema tu. Naandika kutokana na ujuzi wangu.
SAFI KABISA,

MIMI NILIJARIBU KUMPIGIA FUNDI WELDING MMOJA KUMHOJI KUHUSU KUKODI MACHINE,

AKANIAMBIA YEYE ANAZO MACHINES TATU NA GRENDA MBILI,
ILA YAWEZA PITA MIEZI MINNE HAJAPATA MTU WA KUKODI_
SANASANA NI MAFUNDI WENZIYE ANAOJUANA NAO AMBAO NAO HUJA KUAZIMA KWA NADRA SANA IKITOKEA ZA KWAO ZIMEPATA HITILAFU-

NA PIA HAWAMLIPI KAMA ILIVYOANDIKWA HUMU ETI 30,000/= KWA MASAA SITA_
BALI WANAMPOZA TU KIUSHKAJI IKIZINGATIWA NAYE AKIKWAMA HUENDA KWA MAFUNDI WENZIYE.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Eti biashara mimi bado sana?? Usinifurahishe. Nina lodge ya wageni. Nina kampuni ya utalii. Na studio ya media production. Na nina mpango wa kuanzisha kampuni ya ujenzi/ construction. Kwa hio usiseme eti sina uzoefu. Nimefanya business tokea 2003. Nimefanikiwa sehemu na sehemu, pia nimefeli sehemu na sehemu. Kufeli au kushindwa ndio kunakupa mafunzo na uzoefu.
HII NCHI INAHITAJI WATU WASIOZUNGUKAZUNGUKA KAMA NYINYI-
YAANI STRAIGHTLY UMETAJA BIASHARA ZAKO TATU, MWAKA ULIOANZA BIASHARA NA BIASHARA YA NNE AMBAYO UNATAKA KUIANZISHA-

HAPA NDIPO PA KUPATA MWONGOZO FASTA HAPA MKUU!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tokea jf ianzishwe,mtu ambae ametoa madin ambayo ni tangible na ya ukwel ,wew umevunja rekod mzee,daaaaah

Nakutunuku cheo cha kanali,najua una madin meng ,ukinitumia piemu ya madin mengne itabid nikutunuku cheo cha generali
 
Mawazo mazuri sana.
Kuna kukodisha viti, mahema, hadi machine za kuchanganya zege kwenye site za ujenzi.
UbArikiwe!!
 
Back
Top Bottom