Hivi unajua unaweza kutumia akili kidogo tu ukapata pesa nyingi?

DocJayGroup,
Hivi unahofia biashara ya jenereta la 1M na kabati la 250,000 au mziki wa 700,000 unaziona hizo ni hela kubwa sana kwenye biashara? Unajua bei ya Boda Boda naongelea Boxer 125 au 150 bei yake unaijua ni Tsh ngapi?

Kama hujui hizo pikipiki bei yake ni 2M and above lakini anapewa mtu aende nayo popote alete hesabu usiku,unafikiri yule anaetoa pikipiki haogopi kuibiwa hiyo pikipiki?

Pikipiki sio kama jenereta wala kabati ni chombo cha mafuta kinatembea ambacho kufumba na kufumbua mtu anaweza kimbia nayo ukamkuta kashatokea Mwanza na ulimkabidhi pikipiki mkiwa Morogoro. (utampatia wapi)

Kama huwezi kukubali kupoteza huwezi Kufanikiwa kuingiza ktk maisha yako yote,The higher the risk the Higher the income.
 
Eti biashara mimi bado sana?? Usinifurahishe. Nina lodge ya wageni. Nina kampuni ya utalii. Na studio ya media production. Na nina mpango wa kuanzisha kampuni ya ujenzi/ construction. Kwa hio usiseme eti sina uzoefu. Nimefanya business tokea 2003. Nimefanikiwa sehemu na sehemu, pia nimefeli sehemu na sehemu. Kufeli au kushindwa ndio kunakupa mafunzo na uzoefu.
Narudia tena kwa herufi kubwa WEWE BADO SANA toka mwaka 2003 (17 yrs) unantajia Biashara mbili

1.Lodge ya wageni
2.Studio media production

3. Kampuni ya ujenzi (Hii hata hujaianzisha ndio iko planned)

Mimi nimeanza Ujasiriamali 2015 with Zero Tsh ila nikikutajia biashara ninazofanya mpaka sasa zimefika biashara zaidi ya 10,naomba nipe hiyo miaka yako wewe 17 yrs then nikirudi hapa uone kama utakua unaweza hata ku quote comment zangu.

wewe ni aina ya watu mlio FELI na mnakuja aminisha wenzenu kuwa na wao watafeli,Biashara/ujasiriamali haupo hivyo.
 
DocJayGroup,
Hatugombani na wala siwezi gombana na wewe kabisa (napenda watu kama wewe)

Kabla sijajibu swali lako napenda tu kukwambia wewe ni mmoja wa watu ambao hamjawahi miliki chombo cha moto kama Gari na PikiPiki (kibiashara),sasa kwa sababu hujawahi miliki au kujua wanaomiliki huwa wanafanyaje vyombo vyao vya moto visiibiwe Naomba tafuta mtu anaefanya hizo biashara kisha muulize.

Eti unafanyaje unapompa pikipiki/gari/bajaji mtu usiemfahamu kabisa kwa makubaliano tu ya maandishi? Je,huogopi akikimbia navyo? kisha sikiliza jibu atakalo kupa.

Gari thamani yake unaijua nadhani wale madereva Uber sio wote magari ni yao wengi wamepewa magari kisha wanapeleka hesabu,PikiPiki/bajaji zipo mikononi mwa watu zaidi ya 20 Muulize anafanyaje kulinda vyombo vyake?

Achilia mbali na wizi wa kuaminiwa huo umemkabidhi dereva chombo kisha akakimbia nacho (achana na huo wizi), Muulize tena huwa anafanyaje Dereva anapomrudia mikono mitupu na kumwambia kuwa "kaibiwa chombo na majambazi"? Anahakikishaje kuwa kweli huyu dereva kaibiwa chombo na sio janja janja?

Akikupa majibu nadhani hautorudi hapa tena najua utaishia huko huko (17yrs kwenye biashara hujui kulinda mali zako),njoo kwangu mimi nakupa leo pikipiki/gari ukafanyie kazi (na sikujui) Ukiweza kuliiiba ukakaa nalo masaaa 24 Nakupa hicho chombo kama zawadi yako. (huna uzoefu narudia tena kukwambia hili)

Ukirudi kwangu niulize maswali magumu magumu kuhusu biashara sio swali ambalo mwanangu nikimuamsha sasa hivi ana uwezo wa kulijibu.
 
Welda nzuri itakayokidhi mahitaji ya mafundi, ni shs milioni moja na kuendelea. Si chini ya hapo.
wewe mtu unajua kukatisha sana watu tamaaa narudia kukwambia kwa mara ya mwisho (acha kukatisha watu tamaa na research zako ziszo na uhakika)

eti welda nzuri sio chini ya sh.ngapi hapo juu umeandika? Nina welding site mbili na mtaji wa kila moja ni 1M hiyo 1m nimeweka 1.Grinder machine 2.Welding machine 3.Cutting Machine (ya kukatia bomba/chuma).

ila wewe Ukipewa 1M unasema haitoshi hata kununua welding machine nzuri (unatia simanzi sana)
 
Tokea jf ianzishwe,mtu ambae ametoa madin ambayo ni tangible na ya ukwel ,wew umevunja rekod mzee,daaaaah

Nakutunuku cheo cha kanali,najua una madin meng ,ukinitumia piemu ya madin mengne itabid nikutunuku cheo cha generali
Kunipamba kote ili tu nije piyemu nikupe madini😂😂

Barrick washachukua migodi yao hapa nina Makinikia tu😂😂

Asante sana kwa kuthamini michango yangu🙏,tupo pamoja sana mkuu

Tuendelee tu kufatiliana,sitosita kuleta kila ninachoona kina faida kwa wengi.
 
CONTROLA, Ninapenda sana positive and constructive dialogue Kama hizi ili kupata vitu vyenye kujenga na kutusaidia;

Mkuu nataka kuuliza , ninavyojua Mimi Uber Kuna mfumo wa kuchukua taarifa za dereva mpaka unapigwa picha, huu mfumo kiukweli ni ngumu Sana kwa dereva kukimbia au kuiba gari maana lazima utakamatwa... Lakini pia hata kuiba gari ni ngumu Sana kutokana na security systems za gari kwenye usajili .. labda uibe na ulikate spares ... Hivyo Basi ukija kuangalia kwa kina utaona gari sio rahisi kuiba kwa dereva .. Sio Uber tu Kuna malori ya mafuta yanaenda Congo na mizigo pia ...


Sasa tukija kwenye hivi vitu alivyooibua mwenzetu kuhusu ulinzi na usalama wake. Ninadhani atakuwa ameangalia kwa Hilo jicho, maana ukimpa mtu kabati Hakuna taarifa unazichukua Kama taarifa zinazochukuliwa na dereva wa Uber mpaka wadhamini wake ..


Hivyo Basi nadhani changamoto atakuwa ameonelea hapo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Forbes1990,
Mkuu Mwizi ni Mwizi halafu haya maisha huweza m'badilisha hata mchungaji/shekhe wa leo ukamkuta kesho ni tapeli/kibaka wa kutupwa hadi ukawa unajiuliza kulikoni.

Hayo magari mkuu wakiiba wanaenda yakata kata kila kitu kinauzwa kivyake,hivi dereva wa uber aliechafukwa apate connection ya kwenda kuuza Unga south,kaambiwa mtaji ni 2M tu ya kibongo (fanya uje mwanangu hela ipo huku)

uunafkiri ataogopa kuiba hilo gari asepe? ataiba vizuri tu kwanza kashapga hesabu kwenda south anaenda kwa njia za panya hatumii airport wala bus official (utamkamatia wpi)

Kule anaenda kufanya biashara haramu ambayo haina tofauti na biashara aloifanya huku kupata mtaji wa biashara ya south,kwa ufupi mwizi ni mwizi tu na akiamua kaamua hata umchukue makalio print,umchukue picha kila kona ya mwili wake,Ukiona Haibi sio kwamba kaogopa ZILE TAARIFA ZAKE alizochukuliwa,ila anakuwa tu kawaza familia yake/ndugu/nk nk.

Ndio mana kuna kampuni kama huna Familia (hupewi ajira) wanajua kabisa wewe anytime unaweza badilika maana huna cha kupoteza,hivyo huyu jamaa yeye anahofia wizi ila hajaamua kuwaza kuna hata matapeli wa LIVE uso kwa uso.

Mtu anakufata anakupanga live mnaangalia uso kwa uso unampa hela kisha analala mbele,hivi huyu tapeli haogopi kuja kudakwa siku 1 kwasababu kashaonekana? Biashara ni Majaribu mkuu.
 
Nunua na Kodisha COMPACTOR MACHINE

Hii mashine huwezi maliza wiki hujapata kazi na kama wiki ikipita si zaidi ya wiki mbili,na kuna wakati mashine inakuwa busy mpaka unatamani ungekua na mashine zaidi ya 5,bei ya hizi mashine zipo tofauti kwa maelezo zaidi kuhusu bei ya manunuzi ndugu yangu Kidatu anajua zaidi kuhusu bei.

Kuhusu kukodisha hii mashine si chini ya 50,000 inategemea na site unayoenda kufanyia kazi pana ukubwa gani (sqm) ila ni kitendea kazi kingine kwa msio taka stress na biashara za kusubiri wateja,kodi za frem,nk nk

Kwa msiojua compactor machine huu ndio muonekano wake

plate-compactor-05.jpg



Hapa chini ikiwa ipo kazini inafanya mambo yake,ambapo unaweza tafuta kijana wako wakwenda kufanya hii kazi au ukatafuta fundi anaejua itumia au siku uko free ukaenda mwenyewe site kula hela

1240328662825_compaction4stone_10414900.jpg
 
CONTROLA,
Mbona unajisifia? Bila hata kujibu maswali yangu. Pikipiki watu wanalizwa sana tu. Mimi mwenyewe na mifano hai mingi tu. Tena achana na kuibiwa, vijana wanaziharibu zinabakia makopo halafu wanatafuta nyingine. Zaidi ya hayo pikipiki au gari unampatia mtu mmoja ambaye umemhakiki.

Na gari linalalaga sehemu ya kueleweka. Sasa huwezi linganisha pikipiki na gari unazompatia mtu mmoja na hayo mavitu unayowapatia watu wengi wa aina mbalimbali usiowajua. Wewe ni mwandishi tu, lakini ukweli HAUNA UJUZI WA BIASHARA HATA. Nitajie biashara yako moja iliyofanikiwa sana, na kwamba iko wapi, na inashughulika na nini. Na mimi nitakutajia ya kwangu moja.

Sikutaka kufikia hapa, lakini naona sasa unaleta kujifanya sana na kudharau mawazo ya wengine. Mimi ya kwangu na website ya kampuni nitaweka kabisa hapa.
 
CONTROLA,
Nimesema, tusiongelee sana mate. Wewe si unajifanya sanaaa. Nitajie biashara yako moja iliyofanikiwa sana, na kwamba iko wapi, na inashughulika na nini. Na mimi nitakutajia ya kwangu moja. Sikutaka kufikia hapa, lakini naona sasa unaleta kujifanya sana na kudharau mawazo ya wengine.

Mimi ya kwangu na website ya kampuni nitaweka kabisa hapa.
Moja tu kwanza. Unaleta kujisifia wakati wafanya biashara vikongwe tunajua wewe ni mwandishi tu. Sikutaka kufikia hapa, nilitaka tufundishane tu kwa kueleweshana, lakini naona sasa UNALETA MADHARAU huku unajisifia sana.
 
DocJayGroup,
Sijisifii na sina muda wa kujisifia kwako ulie ktk biashara 17 yrs na Biashara mbili.

Sito quote comment yako kuanzia sasa hii ni ya mwisho(thank God) nmekupa time

sana halafu sifanyagi huo ujinga nimejikuta tu nakupa vichache ila umeshaanza ona najisifia.
 
CONTROLA,
Nilishakuambia TOA MIFANO HAI. Pikipiki na gari ni tofauti na hivyo vitu umesema eti mtu atafanikiwa pasipo kutumia akili. Niliandika hapo juu kwamba "Pikipiki watu wanalizwa sana tu. Mimi mwenyewe na mifano hai. Pia pikipiki au gari unampatia mtu mmoja ambaye umemhakiki. Na gari linalalaga sehemu ya kueleweka. Sasa huwezi linganisha pikipiki na gari unazompatia mtu mmoja na hayo mavitu unayowapatia watu wengi wa aina mbalimbali usiowajua.

Halafu acha dharau za kusema mtu hajawahi miliki chombo cha moto. Umeona mtu ana kampuni ya tours asiye na magari wewe? Hehehehe. Usinichekeshe.

Wewe unajiona sana, na watu kama wewe huwa NI MANENO MATUPU tu. Mwandishi wa mada lakini vitendo SIFURI. Tutajie biashara zako na majina kabisa sababu UTAKUWA UNAFANYA ADVERTISING HAPA watu waje kwako. Najua hauwezi taja sababu HAUNA BIASHARA ILIYOFANIKIWA.
 
CONTROLA,
Nimeshakuambia toa mifano hai. Mimi najua mambo ya kumpa mtu gari zaidi yako. Tena land cruisers za mamilioni. Hatumpi tu mtu. Kabla dereva hajakabidhiwa gari kwa mara ya kwanza tunafanya hatua nyingi sana ikiwa ni pamoja na kumfuatilia huyo mtu kwa undani kujua historia yake, wazazi wake, lazima awe amejiaminisha katika utalii. Manake anafahamika nk. Sasa UNATOAJE MFANO WA GARI kuelezea jenereta au welda unazowapatia watu wengi na mbalimbali? Unanichekesha kweli kweli. Bado nasubiri ututajie biashara yako, na mimi nitataja ya kwangu na website nitaweka kabisa.
 
CONTROLA,
Ushamba mwingine huo. Bill Gates ambaye ni tajiri sana duniani ana makampuni mangapi? Wewe unaangalia kufanikiwa biashara kwa kuhesabu namba ya biashara mtu alizo nazo? Hehehehehe.

Bill Gates ana kampuni moja tu ya Microsoft na wewe unazo kumi (kama ni kweli sababu najua wewe ni maneno tu), nani amefanikiwa zaidi ya mwingine. Hehehehe. Acha ushamba.
 
Back
Top Bottom