Hivi tukio hili tunaweza kuliweka kundi la Uchawi? Niliyoyaona live siku ile

Nje ya mada kidogo kwani umekulia mkoa gani mkuu?
 
unachokiita wewe reasoning ni kwa sababu ushautia mipaka ufahamu wako, na unachokiita stori ni kwa sababu bado hujakiprove.
 
Bufa na Scars mko sahihi Sana

Me huwa nashangaa mpk wasomi KBS wanaamini tukio la kikemia kuwa Ni uchawi...yaani mambo ya ajabu kwa kweli Ni sawa na mtu Kijijini kafa ghafla kumbe pressure imemuua Sasa kwa kuwa kule hamna kipimo au hospital Basi wakazi inabidi waamini kuwa kalogwa kitu ambacho hakipo.....







Mimi huwa nawaambia watu wanaoamini Kama Kuna uchawi Basi waende sehemu Waite watu wote Kisha wawahoji kwa kuwaambia waandike matatizo mawili makubwa yanayowasumbua....bila shaka wote wataandika MARADHI na PESA...yaani means wanahitaji afya nzuri na wasiwe maskini hutapata mtu atakayesema anasumbuliwa na wachawi usiku kwamba asaidiwe asilogwe....hii inamaanisha hicho kitu hakipo basi tu maarifa na uwezo wa watu wetu Ni mdogo wanawaza utafikiri tupo karne ya 13
 
mkuu tunazunguka bure bt tatizo lipo katka uchaguzi wa ufahamu, unajua nadharia zote tunazoziamini/tusoziamini ziwe za kimwili/kiroho(kidini, kimila na kisayansi) mwanzilishi wake ni mwanadamu hivo kwa kua kifikra tunatofautiana ndio maana suala la uchaguzi wa ufahamu huchukua nafasi.
 
MHHH bwana kuna manzi nlikuwa namfukuzia ni zamani,nlikuwa nampenda sana yule mtoto ila nlikuja kuwa na mashaka nae sjui ana jini ama vp.

Mimi bwana katika ukuaji wangu hasa kipindi cha balehe hadi mid 20s nlikuwa na kama intuation powers fulani,mfano naweza nkamuwaza mtu ambaye sijaonana nae muda mrefu but ikatokea tu nmemuwaza akatokea muda huohuo,pihizi out of body experience nlikuwa zinanikuta sana,mfn nakumbuka nlikuwa form 2 wakt huo,nkajikuta nmefumbua macho nmesimama ila mwili wangu naona umejifunika gubigubi,nkaenda chumban kwa baba nkakuta nae kalala nlitembea mitaan naona watu wengi sana pamoja na ticha wangu fulani pale secondary wamesimama yaan kila mtu anaangalia upande wakw kama hawaelewi kinachoendelea wengne wanatembea nk...hizi vision nazokuwa naona naona kama kuna ukijani fulani,kama natazama ndani ya maji hv...baadae nkashtukia nipo room pale nimejifunika vile vile nkshtuka nkaamka...hiyo ni moja lkn zipo experience nyingi...

Ila kuna moja nadhani ni wachawi walinichukua.Ilikuwa hv

Kama kawaida nlikuwa nmelala but concious zangu bado hazijapotea nlijihis kama mtu kanipush kwenda chini kwa spidi ambayo haielezeki,nakumbuka hadi macho nlifumbua but it was bad.Nlijihis mtu kanipush kwenda chini ila kiukwel nkajikuta nipo hewani nashuka kuelekea sehem naifaham kbs.Sijawahi iona toka juu but nlijua ni wapi.Nlikuwa nashuka kuelekea makaburini,makabur ambay yalikuwa karib kabs na shule nliyosoma.Bwana we.ile nakaribia yale makaburi kutua chini ikawa kama tumeingia kisimani hv tunashuka spidi kubwa sana.kule chini ni kama ulimwengu mwngne japo ilikuwa ni kiza tiii,sisemi uongo na hakuna sababu kusema uongo,nlisikia watu wanaomboleza wanaliita jina la Yesu,watoto nliwasikia,wanawake wanaume pia,namimi nlijisikia kitu cha ajabu sana UPWEKE NA MFADHAIKO nafsini niliufeel yaan ni kama ndio atmosphere ya kule uliniingia,yaan ndani ya nafsi inakuwa kama hakuna tumaini,hakuna kitu yaan ni hollow,utupu ndani ya nafsi.nakosa maneno sahihi but mimi wakati huo sikuwa nmekaa au safari imekwisha hapana bali kwa spidi ileile nlifeel hayo yote within seconds..basi kupita hilo eneo namimi kusikia watu wanaomboleza vile wanalia namimi nkaanza kukemea kwa jina la Yesu but ile hollow feeling ndio imetawala ni kama Hakuna msaada tena kwny lile eneo...nikashtuka usik ule nkaamaka jasho mgongoni nahema hovyohovyo...Haikuwa habar nliyoanza nayo embu niimalizie habar ynyw

Basi usiku mmoja nmelala nkawa vilevile nko concious lakn nmelala usingz bas najitahid kufumbua macho maana hofu ya jinamizi huwa inanijia but yanajifumba nikifumbua naliona dirisha vzr mwanga nauona wa taa na ukungu na upepo unaopuliza naona.

Basi nkajikuta niko juu ya nyumba yetu kweli upepo unapuliza na mawingu yanakimbia sana ukungu nao umetanda wakat huo wote naelea tu.badi ile kugeuka nyuma ndio namuona yule manzi nlikuwa namfukuzia yuko na mamaake mmoja pamoja na mtu mwingne sikumtambua,wakaanza kunikimbia sasa hapo tupepeluka kama tunaogelea,basi naangalia mtaa wetu ni uko vilevile yaan ni real kabs hakuna tofaut yyt ni kwamba tu sisi tuko juu.Basi nakawa napeperuka kufata barabara za mitaa,baadae nkawapoteza na ndio nkajikuta nipo kitandani.Nkafunua dirishani nakaona upepo unapuliza ukungu mawingu nayo yanakimbia...nkajua tu yule manzi ni mwanga na sijui alikuwa anataka kunifanya nn
Nliamua kuachana nae na mandoto yote yakaisha ila mamaake nlikuwa nikimsalim hanijibu na aniangalia kwa jicho baya sana.Nkabadili hadi njia



Jina la Yesu lina nguvu sana nmepata msaada sana nnapokuwa nmebanishwa kwny mazingira yasioeleweka maana tu nakuta niko kwny astral plane unknowingly
Tunapolala tusali,tuanpoondoka majumbani tusali,tunapokula tusali pia
Jina la Yesu lihimidiwe.Amina


Mr Mshana Jr tia neno chief.
 
Kupooza ni ugonjwa unajulikana mlienda kumpima sababu za kupooza au mmeamua kuhitimisha ni uchawi?
 
Kupooza ni ugonjwa unajulikana mlienda kumpima sababu za kupooza au mmeamua kuhitimisha ni uchawi?


Wewe huamini Uchawi upo Mkuu?

Kama huamini unajaribu Kueleza Uelewa wako finyu kuhusu elimu ya kiroho.

Kama unaamini kuna Mungu basi jua kuna shetani.

Kama unaamini kuna miujiza basi jua kuna Uchawi.


Maisha yanaongozwa na miujiza(Mungu) na Uchawi (shetani)

Karibu kila kitu ukionacho kina kiwango cha mambo hayo mawili
 
Mimi nimekuuliza jambo hapo hujanijibu umekuja na story nyingine. Mimi kama mwanasayansi nipo kutafuta ukweli uchawi unaweza kana ukawepo lakini mpaka sasa hamna evidence kuhusu uchawi mfano kama wewe hujasema chanzo cha ndugu yako kupooza ila umekimbilia kusema uchawi.
mungu pia anawezekana akawepo ila hamna evidence na mungu hana control ya kitu chochote hapa duniani, kama hamna mungu pia hamna shetani
 


πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€

Mkuu unajua ili useme Mungu hayupo inakupasa uwe Mpumbavu wa level ya juu kabisa
 
Mwaka 1964 James randi aliweka dollar 1M kwa yeyote atakayefanikisha kuthibitisha uchawi upo, maelfu ya watu walijitokeza kugombea hiyo challenge lakini mpaka 2015 challenge ikawa terminated ikiwa hakuna aliyeweza kufanikiwa kuthibitisha
Utajiri wetu ni wakiroho unaelewa maana ya huu msamiati fahari ya mchawi ni usiku na si mchana na uchawi pia una ladha ndio maana mtu akiwa mchawi hataki kuacha
 
Jina la Yesu ni kuu sana
 
Mimi mara nyingi sana hua naota "kama ninakimbizwa na mtu/watu hua ninapaa" zaidi hua napaa kutoka mti mmoja kwenda mti mwingine
Sijajigughulisha kujua Ndoto za namna hii zina maana gani au Mimi nina Uwezo gani adi niwe napaa namna ile
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…