Tukio hili maana yake nini?

Aunty_

Member
Nov 15, 2023
6
8
Habarini wanajf,

Naomba kudiscuss jambo hili nanyi. Kama ulifanyiwa ubaya na mtu ukakuumiza sana moyo, sasa bila kujua ukawa unamlaumu yule mtu kwa kumtamkia maneno mabaya uku unalia.

Baada ya muda yule mtu anakuja kutokewa na tukio kama jinsi ambavyo ulilitamka. Yaani vilevile jinsi ulivyosema tukio linatokea. Kama ni kifo kinamtokea vilevile kama mdomo ulivyosema.

Hiyo ilinitokea kwa ndugu yangu kabisa niliyezaliwa nae. Alikuwa hanipendi sasa kuna tukio baya alilifanya Mimi nikamsemea mabaya Yani nakumbuka niliyasema kwasababu aliniumiza moyo wangu na nilikuwa na hasira lakini Cha kushangaza baada ya miezi kadhaa tukio likatokea kama jinsi ambayo nilitamka.

Mpaka Leo nashindwa kuelewa Nini maana yake. Ndugu yangu alifikwa na umauti kama ambavyo nilitamka.

Najiuliza sipati majibu.
 
Hayo mambo yapo.KUNA ROHO IKO NDANI YAKO(EVIL SPIRIT) UNATAKIWA UFANYIWE MAOMBI ITOKE HYO ROHO.ama sivyo muda c mrefu utaitwa mchawi
 
Binadamu ameumbwa kwa sura na kwa mfano wa Mungu. Kumbuka Mungu aliumba kwa kutamka na hivyo hivyo binadamu atafanya mambo yatokee kwa kutamka pia,lakini binadamu sahihi na mwenye nguvu ni yule mwenye uwezo wa kusamehe.

Tumia mdomo wako kuumba mema na samehe mabaya yote utakayofanyiwa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom