Hivi tukio hili tunaweza kuliweka kundi la Uchawi? Niliyoyaona live siku ile

Mkuu chunguza kwa umakini hicho kinachodaiwa kua ni uchawi, mara nyingi ni ujanja ujanja tu

Ingekua mambo yanafanyika kirahisi hivyo kama ambavyo tunasimuliana humu sidhani kama ile dollar Million 1 ingechukua miaka mingi vile bila kupatikana mchawi ambaye angeweza kuthibitisha
Nje ya mada kidogo kwani umekulia mkoa gani mkuu?
 
Nani anayehitaji kuwa open-minded kati yetu? Wewe ambaye ukiambiwa tu unaamini hapo hapo au mimi ambaye na-question everything?

Story zenu zote ni hearsay na nyie mnaziamini kama msaafu ila sisi tunawapa reasoning kabisa na bado hamtaki mnaishia kuamini tu kama nyumbu.
unachokiita wewe reasoning ni kwa sababu ushautia mipaka ufahamu wako, na unachokiita stori ni kwa sababu bado hujakiprove.
 
Bufa na Scars mko sahihi Sana

Me huwa nashangaa mpk wasomi KBS wanaamini tukio la kikemia kuwa Ni uchawi...yaani mambo ya ajabu kwa kweli Ni sawa na mtu Kijijini kafa ghafla kumbe pressure imemuua Sasa kwa kuwa kule hamna kipimo au hospital Basi wakazi inabidi waamini kuwa kalogwa kitu ambacho hakipo.....

Mimi huwa nawaambia watu wanaoamini Kama Kuna uchawi Basi waende sehemu Waite watu wote Kisha wawahoji kwa kuwaambia waandike matatizo mawili makubwa yanayowasumbua....bila shaka wote wataandika MARADHI na PESA...yaani means wanahitaji afya nzuri na wasiwe maskini hutapata mtu atakayesema anasumbuliwa na wachawi usiku kwamba asaidiwe asilogwe....hii inamaanisha hicho kitu hakipo basi tu maarifa na uwezo wa watu wetu Ni mdogo wanawaza utafikiri tupo karne ya 13
 
Hapana tupo level moja, ia utofauti unapokuja ni kila mmoja anavyo define jambo fulani ambalo limeshuhudiwa na wote wawili.

Mwingine anasema ni uchawi kwa kuhusisha supernatural power kwasababu hajui mechanism ya hilo jambo lilivyotokea au kufanyika, ila mwingine analiita ni tukio la ujanja ambapo linaweza kufanywa na mtu yeyote
mkuu tunazunguka bure bt tatizo lipo katka uchaguzi wa ufahamu, unajua nadharia zote tunazoziamini/tusoziamini ziwe za kimwili/kiroho(kidini, kimila na kisayansi) mwanzilishi wake ni mwanadamu hivo kwa kua kifikra tunatofautiana ndio maana suala la uchaguzi wa ufahamu huchukua nafasi.
 
Kwema Wakuu!

Leo nitasimulia tukio lililoniacha mdomo wazi mpaka leo nisielewe nini kilitokea.
Tukio hili ni halisi, sio Stori ya kubuni.

STORI KAMILI!

Mimi ni jamii ya watu ambao usiku tunaona mambo mengi, waotaji WA ndoto, waonaji na wakati mwingine watu tunaolala lakini tunahangaika usiku.

Haiwezekani Kwa watu dizaini yangu usiku upite bila Kuota ndoto yoyote, hiyo haiwezekan, na siku ikiwezekana nahisi itakuwa nimekufa.

Kwa bahati nzuri ndoto nyingi huja na maana zake, zipo ndoto zenye mafumbo magumu, zipo za kawaida na zipo ambazo unazielewa pasipo kuumiza kichwa. Hata hivyo zipo ndoto ambazo nikiumwa hasa malaria zinanisumbua.

Ndoto ngumu kuzitafsiri ni zile ambazo nikiamka Asubuhi nimezisahau, hizi ndio ndoto ambazo Kwa kweli zinaniumizaga kichwa.

Ndoto zinafaida zake, lakini moja ya faida niliyoipata kwenye ndoto ni katika paper ya Kidato cha nne Practical ya Physics, na Chemistry.

Rafiki yangu Hossen Juma ambaye amemaliza Udaktari wake pale KCMC atakuwa ni shahidi pamoja na rafiki zangu wengine wa nyakati hizo nasoma.

Kwangu ndoto ni Jambo nyeti Sana, ninalolizingatia kuliko watu wengi wafanyavyo, pengine hii baadhi ya watu wakaona ni ajabu na kuniona nipo Primitive lakini haiondoi ukweli wa kile nikisemacho. Waliokua na Mimi watakuwa mashahidi WA haya yote.

Nimetanguliza maelezo haya ili kurahisisha Stori iliyopo mbele yetu.

Nilimaliza Chuo nikarudi Morogoro, tulipanga chumba cha bei ya chini Kabisa eneo la Mafisa, nikiwa Mimi, Kaka yangu na mdogo wangu. Hivyo chumba kimoja tulilala watu watatu.

Kila Asubuhi niliamka kwenda kwenye ofisi yangu niliyoianzisha huko Kihonda, Kuota ndoto kwangu sio Jambo la kushtusha, na hata walioishi na Mimi hawatashtuka. Lakini zipo ndoto na ndoto bhana! Zipo ndoto zamoto ambazo huogopesha, hutafakarisha, na kuchanganya akili.

MAUZA UZA YAANZA PALE TULIPOPANGA
Usiku mmoja nikiwa nimelala nikaota ndoto ambayo ilikuwa yamoto. Ndoto Ile mpaka Leo hii naikumbuka lakini ndoto za namna Ile zinanitokeaga Kwa nadra Sana na zinaogopesha Sana.

Yaani ni zile ndoto unaanza kuziota ukiwa umelala fofofo lakini kadiri unavyoota unaamka(yaani unakuwa na akili kabisa), sijui kama kuna watu wanaota ndoto za namna hii.

Yaani ndoto inaenda mpaka inakuwa Kama Njozi;
Ndoto ilikuwa hivi;

Nilikuwa Mimi Taikon, Mama mmoja hivi na binti wa umri wangu(miaka 27). Tulikuwa mahali Kama mgahawa hivi, wenye zile meza za Coca-Cola , Mimi nilikuwa upande huu alafu Yule Mama na Yule Mdada walikuwa wamejaa upande wa pili tukiwa tumetenganishwa na Meza, Ni Kama tulikuwa tunazungumza Jambo Fulani ambalo mpaka sasa silikumbuki, Hali ya hewa ilikuwa tulivu na ilikuwa Kama Majira ya saa kumi na mbili jioni kwenda saa moja, jua lilikuwa limeshazama lakini hapakuwa na Giza kivile.

Mazungumzo yangu yalijikita zaidi na Yule Mama, ambaye nilikuwa simfahamu, na hata Yule binti nilikuwa simjui lakini Nafsi yangu ilimfahamu ingawaje Sura haikuwa ya huyo Nafsi yangu iliyomfahamu. Kwenye ndoto ni kawaida mtu kuweka Code alafu achukue Sura ya mtu mwingine, hilo nalitambua. Hivyo Yule Dada nilimtambua ingawaje sikujishughulisha naye, Mimi niliendelea kuongea na Yule Mama ambaye code zake zilikuwa ngumu kuzikokotoa hivyo mpaka hivi leo simfahamu.

Wakati Yule mama akiongea Yule Dada akawa anani-seduce Kwa kunirembulia na kung'ata ng'ata midomo yake, Mimi bado nikawa simzingatii na macho yangu nikawa nayalazimisha kumtazama Yule Mama na kumpuuza Yule Dada.
Lakini Jambo la kustaajabisha likatokea.

Kweli macho hayana pazia, Yule Dada akawa amepeleka kifua chake mbele na kujinyoosha mikono akiwa kaikunja juu ya kichwa, macho yangu yakatua kwenye kifua chake ambacho alikuwa kavaa blauzi yenye vishikizo vilivyoachana achana Hali iliyofanya nione Kwa ndani maziwa(manyonyo yake) nilihamaki na kujawa na hofu nilipoona Dada Yule anamaziwa ya Mbwa, upande wa kushoto matatu na upande wa kulia matatu jumla maziwa sita.

Nilipomtazama usoni Yule Dada akatabasamu, ni kanakwamba alitaka nione na mpango wake ulikuwa imefanikiwa,

Wakainuka na kabla sijafanya maamuzi wakayeyuka mbelel yangu Kama Moshi, nikiwa najua kinachotaka kuendelea Kwa upesi nikaanza kukimbia, kweli nilikuwa sahihi walijitokeza wakiwa wananikimbiza, nami Kwa upesi nikafanya manuva nikaruka wote tukawa tunapaa hewani tukikimbizana Kwa Kasi isiyo na mfano. Tulipita Maeneo mengi wakiwa wananifuka huku wakipiga makelele yakunichanganya.

Kila nilipoona wananizidi niliwanyoshea Mkono na kumtaja Yesu na Mungu Mkuu, hapo wakawa wanapunguza Kasi.

Hatimaye tukatokea pale chumbani nilipokuwa nimelala, hapo nikamuona mdogo wangu anacheza Game la Dream League, kila mara alikuwa akinitazama huku akinambia ninaota Mimi nilikuwa nashindwa kumjibu Ila namsikia. Yule Dada mwenye maziwa ya mbwa akakaa karibu na dogo, tukawa tunapigana Kwa kunyoosheana mikono, sasa mdogo wangu akawa anashangaa namnyooshea yeye mikono, ni Kama alikuwa ananiogopa, lakini Mimi nilikuwa namnyooshea mikono Yule Dada ambaye alionekana kunikamia.

Mdogo wangu akawa ananisemesha Kwa nguvu, nikamjibu sioti, huyo Dada hapo wewe humuoni, Kwa vile wameshanizoea hivyo akawa ananicheka. Yule Dada Bado alikuwa anapambana na Mimi, nami sikutaka kumuachia nafasi ingawaje sikujua mwisho wa Yale Kama ningeshindwa ingekuwaje.

Yule Dada akajigawanya mmoja akamuingilia Mdogo wangu, sasa wakaanza kunicheka, happ nikawa nashangaa imekuwaje mdogo wangu kageuka Mdada, nikiwa nimemshika na butwaa hapo nikazidiwa nguvu Kwa kupigwa shambulizi na kabla sijafanya chochote nikapiga kelele Kwa sauti hapo hapo Yule Dada akapotea, na Ile Sura ya Yule Dada iliyokuwa kwenye USO wa mdogo wangu ikawa inanitazama na kuanza kunadilika polepole Mimi nikiwa nimemkazia macho mpaka Sura ya mdogo wangu ilipojitokeza polepole kadiri USO wa Yule Dada ulivyokuwa ukiyeyuka pale usoni.

Sasa mdogo wangu akaniambia umepiga kelele Sana. Sikumjibu nikarudi kwenye kitanda kwani nilikuwa nimesimama nikajilaza nikiwa naitafakari ndoto Ile na maana zake.

Ndani ya Dakika moja hata bado sijatulia, Yule Dada ambaye muda huu alikuja Kwa Sura ya mtu ninayemfahamu tena mtu wa karibu akanitokea Live akiwa na kiwiliwili tuu yaani kichwa mpaka kwenye kiuno. Alikuwa kaning'inia hewani huku akitabasamu Mimi nikamnyooshea Mkono na kuanza kumsemea maneno kimoyo moyo. Sasa mdogo wangu akawa ananitazama hapo kaacha kucheza Game. Ananishangaa ninafanya nini akawa ananiita tuu jina langu.

Mimi kazi ikawa kunyooshea kile kiwiliwili cha Yule mama ambacho kilikuwa kinashuka kikiwa kimetanua mikono yake, nikajua lengo lake anataka kushika kichwa changu na Mimi nikawa SITAKI. Pambano kikaendeleza Kwa kitambo huku kile kiwiliwili kikinifanyia vioja.

Alipogundua haniwezi akaninyoshea kidole alafu akasema wewe, wewe! Wewe mara tatu kisha akasema unabahati Sana. Akakunja USO wake kisha akayeyuka na kuniacha nikibabaikà.

Kesho asubuhi nikaenda kazini kwangu Kama ilivyodesturi, wakwanza kuonana naye ni Yule Dada niliyemuona jana ambaye alikuja akiwa katika Sura ya dada mwingine, nilimfahamu Kwa sababu Code yake ilikuwa nyepesi, tofauti na huyu Mama ambaye yeye alijidhatiti kikamilifu.

Nikamuonya aache michezo yake ya kitoto, nikamtisha ingawaje sikuwa na lakumfanya ni mikwala Mbuzi.

Jioni yake nikarudi nyumbani, hapo nilikuwa Mimi na Kaka yangu.

Huko nje alikuwepo kijana mmoja mlevi alikuwa akitukanana na Mama mwenye nyumba, Yule kijana tulishamzoea kila jioni mida ya saa moja huja kumtukana Mama mwenye nyumba kwani anamdai elfu Saba yake.

Huyo kijana alikuwa haishi kwenye nyumba hiyo. Hivyo alikuwa ni mtu wakuja anatukana were! Akichoka anaondoka.

Basi nikatoka kwenda kuoga, kwani bafu na Choo lilikuwa la nje. Kama nilivyosema hapo awali kuwa tulipanga chumba cha Hali ya chini. Basi nilivyotoka nikashtushwa na nguo aliyokuwa kavaa mama mwenye nyumba, Kwa maana baada tuu ya kuiona moja Kwa moja akili yangu ikanirudisha kwenye Ile ndoto ya kutisha ya Jana usiku, ilikuwa nguo ileile.
Nikaficha hofu yangu nikasalimia nikaenda kuoga na ndoo yangu.

Sasa nikawa naoga huku natafakari mambo yote Yale, bado matusi yakiendelea hapo nje kutoka Kwa Yule kijana.

Kutokana na Bafu lilikuwa halina bati juu na lilikuwa Bafu lenye kuta fupi ambalo Kama utachechemea au kuruka juu unaweza ona nje, nikawa mara Kwa mara nachungulia nje hasa pale ninaposikia wameshikana yaani Yule kijana mlevi na Mama mwenye Nyumba.

Yule kijana nikamuona akiwa ameshikamana na Mama mwenye nyumba wakiwa wanavutana vutana, nikachungulia Kule lilipodirisha letu kumbe Kaka yangu naye alikuwa kasogeza Pazia kidogo naye anachungulia.

Katika Hali isiyotarajiwa yenye kutia hofu, Yule kijana baada ya kumsukuma mama mwenye nyumba akaanguka, kijana mlevi akawa anakimbia na kulifuata Geti akiwa kashika mandala yake; Mama mwenye nyumba akasimama Kwa kujikokota kwani ni mtu mzima akiwa amekusudia kumkimbiza Yule kijana mlevi asitoke getini.

Lakini tayari Yule kijana mlevi alikuwa yupo Mbali amelikaribia Geti anataka kulifungua atokomee.

Kilichofuata ndicho kimenifanya niandike Uzi huu.

Nilishangazwa bado nikiwa bafuni kumuona Mama mwenye nyumba akinyanyua Mkono wake akiwa kasimama na kumnyooshea Yule kijana mlevi ambaye tayari alikuwa amelifungua Geti ili atokomee, Mama mwenye nyumba alikuwa ananguruma Kama Simba nafikiri alikuwa kapandisha maruhani.

Yule kijana akawa Kama kanatishwa pale Getini akageuka Kama Roboti wakawa wanatazamana na Mama mwenye nyumba.

Yule kijana akawa anapiga kelele Kama mtu anayesikia maumivu makali huku akiomba Msamaha, akiwa anatembea Kama Roboti kumfuata Mama mwenye nyumba ambaye amesimama akitetemeka akiwa bado amenyosha Mkono wake.

Yule kijana alipofika karibu na Mama mwenye Nyumba akapiga magoti akawa anapiga Sana.

Ni Kama pombe zilikuwa zimakatika, Yule mama akamgusa pajini kisha akaanza kusema wewe si unajifanya mjanja, sasa utanikuta Mimi ni Nani, kijana naye akawa anapiga akiomba asamehewa.

Mama akageuka nyuma akaanza kutembea huku akitetemeka na kuyumba yumba ungedhani ataanguka lakini ndio alikuwa akiondoka hivyo, Yule kijana naye akawa anamfuta mpaka walipofika mlangoni kwake wakaingia ndani na kutunga mlango.

Kilichofuata ni kelele za Yule kijana mlevi akiomba msaada anakufa, wakati mama mwenye nyumba akinguruma na kutamba pigana na Mimi sasa, pesa yako sikupi na huna chakunifanya.

Nikatoka Bafuni mbiombio nikaenda chumbani nikamkuta Bro akiwa analalama kuwa tuhame pale, nikamuuliza Kwa nini ati ananiambia huyu Mama mwanga.

Nikamwambia hawezi tufanya kitu, yeye akakazana tuhame, wiki iliyofuata tulihama.

Yule kijana alipiga ukelele WA mwisho kisha kimya ndicho kilifuatia.
Hatukumuona tena mpaka wiki tunayoondoka pale.

Tukio hili nafikiri ndio kitu kifananacho na Uchawi nilichowahi kukiona katika maisha yangu.

Yote juu ya yote.
Mungu ni Mkuu, huyo ukimtegemea hakuna wakukugusa

Robert Heriel
Dar es salaam
MHHH bwana kuna manzi nlikuwa namfukuzia ni zamani,nlikuwa nampenda sana yule mtoto ila nlikuja kuwa na mashaka nae sjui ana jini ama vp.

Mimi bwana katika ukuaji wangu hasa kipindi cha balehe hadi mid 20s nlikuwa na kama intuation powers fulani,mfano naweza nkamuwaza mtu ambaye sijaonana nae muda mrefu but ikatokea tu nmemuwaza akatokea muda huohuo,pihizi out of body experience nlikuwa zinanikuta sana,mfn nakumbuka nlikuwa form 2 wakt huo,nkajikuta nmefumbua macho nmesimama ila mwili wangu naona umejifunika gubigubi,nkaenda chumban kwa baba nkakuta nae kalala nlitembea mitaan naona watu wengi sana pamoja na ticha wangu fulani pale secondary wamesimama yaan kila mtu anaangalia upande wakw kama hawaelewi kinachoendelea wengne wanatembea nk...hizi vision nazokuwa naona naona kama kuna ukijani fulani,kama natazama ndani ya maji hv...baadae nkashtukia nipo room pale nimejifunika vile vile nkshtuka nkaamka...hiyo ni moja lkn zipo experience nyingi...

Ila kuna moja nadhani ni wachawi walinichukua.Ilikuwa hv

Kama kawaida nlikuwa nmelala but concious zangu bado hazijapotea nlijihis kama mtu kanipush kwenda chini kwa spidi ambayo haielezeki,nakumbuka hadi macho nlifumbua but it was bad.Nlijihis mtu kanipush kwenda chini ila kiukwel nkajikuta nipo hewani nashuka kuelekea sehem naifaham kbs.Sijawahi iona toka juu but nlijua ni wapi.Nlikuwa nashuka kuelekea makaburini,makabur ambay yalikuwa karib kabs na shule nliyosoma.Bwana we.ile nakaribia yale makaburi kutua chini ikawa kama tumeingia kisimani hv tunashuka spidi kubwa sana.kule chini ni kama ulimwengu mwngne japo ilikuwa ni kiza tiii,sisemi uongo na hakuna sababu kusema uongo,nlisikia watu wanaomboleza wanaliita jina la Yesu,watoto nliwasikia,wanawake wanaume pia,namimi nlijisikia kitu cha ajabu sana UPWEKE NA MFADHAIKO nafsini niliufeel yaan ni kama ndio atmosphere ya kule uliniingia,yaan ndani ya nafsi inakuwa kama hakuna tumaini,hakuna kitu yaan ni hollow,utupu ndani ya nafsi.nakosa maneno sahihi but mimi wakati huo sikuwa nmekaa au safari imekwisha hapana bali kwa spidi ileile nlifeel hayo yote within seconds..basi kupita hilo eneo namimi kusikia watu wanaomboleza vile wanalia namimi nkaanza kukemea kwa jina la Yesu but ile hollow feeling ndio imetawala ni kama Hakuna msaada tena kwny lile eneo...nikashtuka usik ule nkaamaka jasho mgongoni nahema hovyohovyo...Haikuwa habar nliyoanza nayo embu niimalizie habar ynyw

Basi usiku mmoja nmelala nkawa vilevile nko concious lakn nmelala usingz bas najitahid kufumbua macho maana hofu ya jinamizi huwa inanijia but yanajifumba nikifumbua naliona dirisha vzr mwanga nauona wa taa na ukungu na upepo unaopuliza naona.

Basi nkajikuta niko juu ya nyumba yetu kweli upepo unapuliza na mawingu yanakimbia sana ukungu nao umetanda wakat huo wote naelea tu.badi ile kugeuka nyuma ndio namuona yule manzi nlikuwa namfukuzia yuko na mamaake mmoja pamoja na mtu mwingne sikumtambua,wakaanza kunikimbia sasa hapo tupepeluka kama tunaogelea,basi naangalia mtaa wetu ni uko vilevile yaan ni real kabs hakuna tofaut yyt ni kwamba tu sisi tuko juu.Basi nakawa napeperuka kufata barabara za mitaa,baadae nkawapoteza na ndio nkajikuta nipo kitandani.Nkafunua dirishani nakaona upepo unapuliza ukungu mawingu nayo yanakimbia...nkajua tu yule manzi ni mwanga na sijui alikuwa anataka kunifanya nn
Nliamua kuachana nae na mandoto yote yakaisha ila mamaake nlikuwa nikimsalim hanijibu na aniangalia kwa jicho baya sana.Nkabadili hadi njia

Jina la Yesu lina nguvu sana nmepata msaada sana nnapokuwa nmebanishwa kwny mazingira yasioeleweka maana tu nakuta niko kwny astral plane unknowingly
Tunapolala tusali,tuanpoondoka majumbani tusali,tunapokula tusali pia
Jina la Yesu lihimidiwe.Amina

Mr Mshana Jr tia neno chief.
 
Mkuu haya mambo yapo, haijalishi unaamini au la, mimi nimewahi kushuhudia mjomba wangu akipooza mwili mzima ajili ya kudai mirathi, iliposhindikana kudai kwa njia ya kawaida alifungua kesi, baada ya kufungua kesi aliambiwa na mke wa babu mdogo "we si unajifanya unajua haya tutaona" usiku wa kuamkia siku kesi inaanza kusikilizwa alipooza na hakuwahi hudhuria kesi mpaka ikafutwa, mama, ancle mdogo na wadogo zao waliogopa kuhudhuria wakijua nao yatawafika, baada ya kupona alitokomea mazima hadi leo hatujawahi kumuona.
Kupooza ni ugonjwa unajulikana mlienda kumpima sababu za kupooza au mmeamua kuhitimisha ni uchawi?
 
Kupooza ni ugonjwa unajulikana mlienda kumpima sababu za kupooza au mmeamua kuhitimisha ni uchawi?

Wewe huamini Uchawi upo Mkuu?

Kama huamini unajaribu Kueleza Uelewa wako finyu kuhusu elimu ya kiroho.

Kama unaamini kuna Mungu basi jua kuna shetani.

Kama unaamini kuna miujiza basi jua kuna Uchawi.

Maisha yanaongozwa na miujiza(Mungu) na Uchawi (shetani)

Karibu kila kitu ukionacho kina kiwango cha mambo hayo mawili
 
Mimi nimekuuliza jambo hapo hujanijibu umekuja na story nyingine. Mimi kama mwanasayansi nipo kutafuta ukweli uchawi unaweza kana ukawepo lakini mpaka sasa hamna evidence kuhusu uchawi mfano kama wewe hujasema chanzo cha ndugu yako kupooza ila umekimbilia kusema uchawi.
mungu pia anawezekana akawepo ila hamna evidence na mungu hana control ya kitu chochote hapa duniani, kama hamna mungu pia hamna shetani
 
😀😀😀😀

Mkuu unajua ili useme Mungu hayupo inakupasa uwe Mpumbavu wa level ya juu kabisa
 
Mwaka 1964 James randi aliweka dollar 1M kwa yeyote atakayefanikisha kuthibitisha uchawi upo, maelfu ya watu walijitokeza kugombea hiyo challenge lakini mpaka 2015 challenge ikawa terminated ikiwa hakuna aliyeweza kufanikiwa kuthibitisha
Utajiri wetu ni wakiroho unaelewa maana ya huu msamiati fahari ya mchawi ni usiku na si mchana na uchawi pia una ladha ndio maana mtu akiwa mchawi hataki kuacha
 
MHHH bwana kuna manzi nlikuwa namfukuzia ni zamani,nlikuwa nampenda sana yule mtoto ila nlikuja kuwa na mashaka nae sjui ana jini ama vp.

Mimi bwana katika ukuaji wangu hasa kipindi cha balehe hadi mid 20s nlikuwa na kama intuation powers fulani,mfano naweza nkamuwaza mtu ambaye sijaonana nae muda mrefu but ikatokea tu nmemuwaza akatokea muda huohuo,pihizi out of body experience nlikuwa zinanikuta sana,mfn nakumbuka nlikuwa form 2 wakt huo,nkajikuta nmefumbua macho nmesimama ila mwili wangu naona umejifunika gubigubi,nkaenda chumban kwa baba nkakuta nae kalala nlitembea mitaan naona watu wengi sana pamoja na ticha wangu fulani pale secondary wamesimama yaan kila mtu anaangalia upande wakw kama hawaelewi kinachoendelea wengne wanatembea nk...hizi vision nazokuwa naona naona kama kuna ukijani fulani,kama natazama ndani ya maji hv...baadae nkashtukia nipo room pale nimejifunika vile vile nkshtuka nkaamka...hiyo ni moja lkn zipo experience nyingi...

Ila kuna moja nadhani ni wachawi walinichukua.Ilikuwa hv

Kama kawaida nlikuwa nmelala but concious zangu bado hazijapotea nlijihis kama mtu kanipush kwenda chini kwa spidi ambayo haielezeki,nakumbuka hadi macho nlifumbua but it was bad.Nlijihis mtu kanipush kwenda chini ila kiukwel nkajikuta nipo hewani nashuka kuelekea sehem naifaham kbs.Sijawahi iona toka juu but nlijua ni wapi.Nlikuwa nashuka kuelekea makaburini,makabur ambay yalikuwa karib kabs na shule nliyosoma.Bwana we.ile nakaribia yale makaburi kutua chini ikawa kama tumeingia kisimani hv tunashuka spidi kubwa sana.kule chini ni kama ulimwengu mwngne japo ilikuwa ni kiza tiii,sisemi uongo na hakuna sababu kusema uongo,nlisikia watu wanaomboleza wanaliita jina la Yesu,watoto nliwasikia,wanawake wanaume pia,namimi nlijisikia kitu cha ajabu sana UPWEKE NA MFADHAIKO nafsini niliufeel yaan ni kama ndio atmosphere ya kule uliniingia,yaan ndani ya nafsi inakuwa kama hakuna tumaini,hakuna kitu yaan ni hollow,utupu ndani ya nafsi.nakosa maneno sahihi but mimi wakati huo sikuwa nmekaa au safari imekwisha hapana bali kwa spidi ileile nlifeel hayo yote within seconds..basi kupita hilo eneo namimi kusikia watu wanaomboleza vile wanalia namimi nkaanza kukemea kwa jina la Yesu but ile hollow feeling ndio imetawala ni kama Hakuna msaada tena kwny lile eneo...nikashtuka usik ule nkaamaka jasho mgongoni nahema hovyohovyo...Haikuwa habar nliyoanza nayo embu niimalizie habar ynyw

Basi usiku mmoja nmelala nkawa vilevile nko concious lakn nmelala usingz bas najitahid kufumbua macho maana hofu ya jinamizi huwa inanijia but yanajifumba nikifumbua naliona dirisha vzr mwanga nauona wa taa na ukungu na upepo unaopuliza naona.

Basi nkajikuta niko juu ya nyumba yetu kweli upepo unapuliza na mawingu yanakimbia sana ukungu nao umetanda wakat huo wote naelea tu.badi ile kugeuka nyuma ndio namuona yule manzi nlikuwa namfukuzia yuko na mamaake mmoja pamoja na mtu mwingne sikumtambua,wakaanza kunikimbia sasa hapo tupepeluka kama tunaogelea,basi naangalia mtaa wetu ni uko vilevile yaan ni real kabs hakuna tofaut yyt ni kwamba tu sisi tuko juu.Basi nakawa napeperuka kufata barabara za mitaa,baadae nkawapoteza na ndio nkajikuta nipo kitandani.Nkafunua dirishani nakaona upepo unapuliza ukungu mawingu nayo yanakimbia...nkajua tu yule manzi ni mwanga na sijui alikuwa anataka kunifanya nn
Nliamua kuachana nae na mandoto yote yakaisha ila mamaake nlikuwa nikimsalim hanijibu na aniangalia kwa jicho baya sana.Nkabadili hadi njia

Jina la Yesu lina nguvu sana nmepata msaada sana nnapokuwa nmebanishwa kwny mazingira yasioeleweka maana tu nakuta niko kwny astral plane unknowingly
Tunapolala tusali,tuanpoondoka majumbani tusali,tunapokula tusali pia
Jina la Yesu lihimidiwe.Amina

Mr Mshana Jr tia neno chief.
Jina la Yesu ni kuu sana
 
Mimi mara nyingi sana hua naota "kama ninakimbizwa na mtu/watu hua ninapaa" zaidi hua napaa kutoka mti mmoja kwenda mti mwingine
Sijajigughulisha kujua Ndoto za namna hii zina maana gani au Mimi nina Uwezo gani adi niwe napaa namna ile
 
22 Reactions
Reply
Back
Top Bottom