Hivi karibuni japokuwa sikumbuki ni mwaka gani lilifanyika shindano kubwa tu nchini na likiwashindanisha wabunifu wote wa mavazi,LENGO likiwa ni kupata vazi la kitaifa...hilo halijawezekana mpaka sasa na sijui litawezekana lini.....likaja kichwani mwangu swali ambalo si tu huwa najiuliza mie bali watanzania wote,hivi jamani tukiichukua taarabu,bongoflava,takeu,dansi n.k..je,miziki ya namna hii ni YETU??tunapojadilim hebu tuzingatie vigezo hivi,asili,style za uchezaji,mavazi,lugha,mipigo(beats) na pengine zaidi ya yote,utengenezaji wake...........je,hizi na aina zingine ambazo sijataja ni aina za muziki ambao ukipigwa ugenini mtu atajua ni wa kitanzania???