Hivi Tanzania nini tunachoweza? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi Tanzania nini tunachoweza?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mmzalendo, Mar 3, 2011.

 1. mmzalendo

  mmzalendo Senior Member

  #1
  Mar 3, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 165
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kila kukicha uwa najiuliza shwali vipi Tanzania nini tunachowez kufanya kwa ufanisi?
  maana sasa inakuwa kama tunaishi kwa dripu za wahisani, maana hapo juzi rais katika
  hotuba yake anasema mataifa makubwa yakiyumba na sisi tunayumba lakini hii ina

  ukweli kiasi gani na kama kuna ukweli ina maana uchumi wetu sisi unakuwa controlled kwa
  remote? na kama ni hivyo kuna haja gani ya kuwa na hiyo tume ya mipango maana wanachofanya
  hakisaidii uchumi wetu ila yanayotokea nje?

  Tukipewa mikataba kusaini ndio kabisa madudu hasara kwa taifa, kwa sasa karibu mikataba
  yote ya serikali ina kasoro au inatuumiwa kuzungukwa na rushwa

  tukipewa kuendesha viwanda, vinakufa kesho yeka
  tukipewa mabanki pesa inahamishwa tu kama alivyotufanya balari
  bandani ndio hiyo hakuna kinachofanyika
  reli ndio usisema huduma zake za kubeep
  mahospitalini hakuna hata palacentamo
  migodi tunayo faidi hatuioni labda hayo mashimo tutafuga panya na njoka wa utalii
  mbuga za wanyama kila sehemu lakini ziko hoi hakuna vitu vya kuvuti watalii

  sijui nini tunaweza kwa kweli maana hata siasa naona nazo tumeanza kushindwa kidogo kidogo
  ni bunduki na kutishana tu siku hizi
  umeme ndio tumesha sahau sijui wanasubilia nini kuja kuchukuwa haya manyaya yao mitaani au tuyafanye antena

  hakunatunachoweza mimi sijui nini labda mmmmmm maana ukimwi umezagaa kila kona mpaka
  kwa watoto wa shule, hii nadhani tunaweza lakini sijui kama tunawashinda kwa bibi

  source www.lifeofmshaba.com
   
 2. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #2
  Mar 3, 2011
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mkuu kuna baadhi ya mambo ni lazima tukubaliane na hali halisi. Unaweza kusikia wanasiasa wanaongopea watu, lakini hali halisi ni kwamba tumeshindwa ku-manage nchi yetu. Mfano mzuri tu ni umeme, serikali toka imeingia madarakani miaka mitano iliopita, imeweza ku-strengthern ufisadi, favouritism, udini na ubabashaji, na imeweza kuweaken growth na ku-promote taabu kwa wananchi.

  Tatizo ni kubwa ni kwamba lawama nyingi zinaenda kwa rais wakati rais tunasheria na hatujafanya lolote kubwa kulalamikia hali hiyo.
   
 3. 911

  911 Platinum Member

  #3
  Mar 3, 2011
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 761
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 60
  Tupo vizuri katika kulalamika,kunung'unika na kulaumu bila kuonesha kwa vitendo kuwa ni kipi tunakipinga/tunakichukia.
   
 4. Chamoto

  Chamoto JF-Expert Member

  #4
  Mar 3, 2011
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 2,076
  Likes Received: 1,112
  Trophy Points: 280
  Mi naona nikujibu kwa kutumia majibu ya baba wa taifa ambapo aliongelea kuhusu uongozi

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. Click_and_go

  Click_and_go JF-Expert Member

  #5
  Mar 3, 2011
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 451
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  tunaweza kufanya yote kama tukiamua!!!!
   
 6. T

  TANZANIABORA Member

  #6
  Mar 3, 2011
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa sasa kweli yote yametushida ila ukweli ni kwamba tunaweza kila kitu. Tatizo kubwa ninaloliona ni ubinafsi hasa kwa viongozi wetu japo hata kwa wananchi...ila zaidi kwa serikali ikiwa kama injini ya nchi. Maendeleo hayaji kwa miujiza something should be done. Tukiamua tunaweza na uzuri resources za kutosha tunazo. Ubinafsi ni tatizo kubwa maana unakuta kila mtu anajifikiria mwenyewe na familia yake na zaidi ya hapo kutoridhika na ndo maana hata ufisadi umetawala Tanzania sasa. Uzalendo hakuna. viongozi tunawapa kura hawafanyi chochote zaidi ya kuchukua posho na hiyo mipesa ya mashangingi ambayo ingeweza kutekeleza miradi kibao.....ila tukikumbuka mafungu yote hayo ni madeni kwa asilimia kubwa. Raisi kasema uchumi wa mataifa makubwa ukiyumba nasi chali....ni kweli lakini twajitakia. Hivi ukiwa na uwezo wa kula ugali maharage utaenda kukopa ili ule wali kuku?? Kama Tanzania ndo tutaendelea hivi basi hatuwezi kutoka na vizazi vijavyo vitakuwa kwenye hali mbaya zaidi. Naungana na wadau wengine hapo juu. Kila sekta inasumbua na hakuna mipango ya kueleweka ya kutoa matumaini. Ili tusonge mbele na tuweze kujitegemea lazima kwanza tuamue. Hebu tuoneni kwa mfano wachina wanavyosonga. Siyo miujiza bali sera zinazotekelezeka na zinasimamiwa ipasavyo. then kila mtu anafanya kazi vilivyo. Sisi imebaki blablaa tu. We really need changes. Tukiendelea kuwa na viongozi wababaishazi, wasimamizi wababaishaji n.k. hatuwezi kusonga mbele hata kidogo. Miradi mingi ya pesa nyingi ambazo ni mikopo inaishia hewani kwa kuwa wasimamizi wanataka wawe na vitambi na ndo focus yao kubwa. Tujirekebishe tuendelee. Hakuna asiyeona tunafanya yasiyofaa hata hao viongozi wanajua ila kwa vile wamejawa na ubinafsi ndo hivo. Wana bahati kwanza wametembea nchi za watu wakaona vinavyofanyika. Ni mtizamo!! We need to change our attitude!!:decision:
   
 7. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #7
  Mar 3, 2011
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  TUKIAMUA TUNAWEZA TENA SANA.!!!!!!!!!!!!!!!
  ILA TUNAWEZA KUWA HATUJUI KUWA TUNAWEZA!
  KUTOKANA NA HILO BASI ''' viongozi wetu na watendaji wengi wa serikali iliyo madarakani wanashindwa ku analyse fursa za kuanza nazo.
  Kwa sasa mambo makubwa tunayoweza kusema tunaweza au kujisifia kwayo ni
  1. Kuimarisha UFISADI hili tumefanikiwa sana
  2. Kugawiana Kazi kwa upendeleo Hilo nalo ni sehemu ya maisha
  3. Kueneza mbegu ya udini hilo nalo halipo nyuma
  4.Kula mali ya Umma
  5. KUtofuata katiba
  6. Kuchakachua kila suala!
   
Loading...