hivi tanzania kuna wanasheria kweli?

adabet

Member
Dec 14, 2010
6
0
ikiwa mtu anaingia tz kwa mara ya kwanza unaweza akasea hakuna wanaojua sheria,tunakuwa fooled ktk mengi.watu wanakuwa charged wrongly ili watoke mfano kesi ya aliyekuwa mkuu wa polisi kanda ..... bwana zo.... eti alichajiwa first degree murder, haya tafsiri yake m2 awe kwenye eneo la tukio sasa zo... alikuwepo? au it was calculated ili atokee hapo?haya sasa kuna ishu ya utakasaji wa pesa je kuna kifungu ktk sheria zetu kinachohusu mambo ya utakasaji fedha na je tafsiri yake ikoje?nadhani labda hawa wanaofanya kazi za kisheria serikalini ni wale walioshindwa shule au incomp? au ndio tunarudi kwenye difinition ya what is law?nchi imefika hapa pabaya ni kwa sababu yenu wanataaluma ya sheria mliolala hamuoni mikataba mibovu,wahalifu wanazurula mitaani,violation ya mambo kibao. i dont know who is fooling who?
 
Bwana/bi Adabet,
Kwa namna ulivyouliza swali lako umewatia kichefuchefu wanasheria waliomo humu jamvini,
ambao bila kujali hasara wanazopata hutoa ushauri na elimu ya bure humu kuhusiana na mambo
mbalimbali ya kisheria.Ndiyo maana umeona wamebaki kimya bila kukujibu kwani mtu mwenye akili kubishana na mwehu ni
vigumu mtu mwingine mwenye busara akatofautisha kati ya mwehu na mzima kiakili.
Kuwa Mwanasheria siyo jambo rahisi ambalo mtu aliyefeli analiweza, mtu aliyefeli
anazo dalili kama zako za kupayuka, tena hatari sana unapopayuka kupitia maandishi. Wanasheria ni watu
wanaoheshimiana sana. Taaluma hii inayo miiko yake kama ilivyo kwa madaktari, ndiyo maana huwezi kusikia
wala kuona tangazo la biashara la mwanasheria kutangaza huduma yake kuwa ni bora kupita ya mwingine.
Endapo ulihitaji kuelimishwa ungeuliza swali kistaarabu ili ujibiwe.
Tanzania haina utaratibu wa ku-classfy murder offence into degrees, ie first degree murder, second...,etc.
kila mtu aliyeshiriki kuua hata kama katika hatua ya kula njama hushitakiwa kama principal offender.
kuhusu kutakasa fedha ipo sheria ya Anti money laundering Act. Endapo unazo habari za watuhumiwa wa aina hii unaweza kuzifikisha PCCB au kwa DCI tena kwa siri bila mtu yeyote kukufahamu, ndipo uone kama hatashughulikiwa. Tafakari uchukue hatua!!
Watu hufikishwa mahakamani lakini ni haki ya mtuhumiwa kupata dhamana, ndiyo maana unawaona mitaani.
Kuhusu kesi uliyoitaja ni jambo la kawaida mtu kutokupatikana na hatia kutokana na mtizamo wa jaji aliyeisikiliza kesi,
lakini ushahidi huohuo ambao jaji wa awali aliukataa waweza kukubaliwa kwenye rufani.
Sheria ni Bahari pana sana kuweza kuogelea hapa.
Karibu tena wakati mwingine ukiwa unalo tatizo...usiwanyime wengine fursa ya kufaidika humu kwa kuwatukana wataalamu wetu.
 
Naona hapa Wanasheria wamelaumiwa kwa kila kitu, hata kwa watoto wanaozurura mitaani nalo ni "kosa la Wanasheria!" Kaaazi kweli kweli! Hata ukiachana na mumeo/mkeo bila shaka "hatuna Wanasheria!"
 
Wanasheria wapo tena mahiri sana tatizo wote wanaugua ugonjwa wa rushwa,yaani wana virusi vya kutumia taaluma yao kuchumia tumboni street,penye rupia wapo tayari hata kuuza utu wao,hawa ndio wanasheria wa TZ,angalia akina mzee wa vikofia vya usinga,funga mchele n.k
 
Lipo jambo moja ambalo Mfianchi hulijui ni kwamba kazi ya uanasheria inategemea sana matakwa ya mteja wako.
Endapo mteja anahitaji ukamtetee mahakamani inakubidi utumie ujuzi wako wote kuweza kumtetea mahakamani
bila kujali ugumu wa kazi hiyo kutokana na mazingira ya kesi yake. Kazi hii labda yaweza kufananishwa na ya tax driver,
abiria yeyote atakayemkodi ni wake lazima amfikishe aendapo. Lakini kama ukitaka ushauri wa kisheria ili kujua kama tatizo lako laweza kufanikiwa mahakamani utapata ushauri usioegemea upande wowote.
Kama ulitaka mteja wa Fungamchele ashindwe maana yake unataka kumuonyesha msomi huyo kuwa ni legelege katika kazi yake. Pale unapowaona waovu wanashinda kesi inatokana na mambo mengi, ikiwa ni pamoja na umahiri wa mawakili wao, mtazamo wa hakimu/jaji, makosa ya kiupelelezi nakadhalika. Kamwe haimaanishi kuwa Mtuhumiwa hakutenda aliyotuhumiwa, labda uelewe pia unaposheherekea kuachiwa kwa Muuuoro mwandishi wa habari, usilaumu kuachiwa kwa Zoumbee au Fedhambili. Maana wakati mwingine sababu za kiufundi husababisha mtuhumiwa kuachiwa na haimaanishi kuwa hakutenda bali ushahidi haukuthibitisha.
Ipo siku, Wanasheria, ambayo mnatakiwa kuweka hapa mbinu za kiufundi zilizopo kwenye sheria ya Ushahidi ili kuondoa fikra potofu dhidi yenu.
 
Sheria zenyewe zimetungwa na mapungufu mengi sana, na hivyo zinaleta mapungufu makubwa sana kuzisimamia. Si kosa la wanasheria bali mfumo mzima wa uandaa wa sheria zetu ni dhaifu, kwa mfano sheria inamtambua mtu mwenye chini ya miaka 18 kuwa ni mtoto na hapohapo kuna sheria ya ndoa inayoruhusu mtu mwenye miaka zaidi ya 14 kuoa au kuolewa (sijui kama ilisharekebishwa). Tumezidi kuwa na sheria holela.
 
Wanasheria wapo tena mahiri sana tatizo wote wanaugua ugonjwa wa rushwa,yaani wana virusi vya kutumia taaluma yao kuchumia tumboni street,penye rupia wapo tayari hata kuuza utu wao,hawa ndio wanasheria wa TZ,angalia akina mzee wa vikofia vya usinga,funga mchele n.k

Hao wanasheria mahiri ni kina nani? Umahiri my ass....kama ni mahiri hebu basi na wa-champion sheria zetu zote ziandikwe katika lugha yetu tuijuayo wengi! Ebo!
 
Kujua Sheria doesnt make one Mwanasheria

I think hawa watu wakubali kujivue magamba kulinda heshima ya taaluma yao
 
Jamaa angeuliza hili swali namna hii, Hivi wanasheria walioajiriwa serikalini, si wale wenye alama za chini (waliokosa pa kwenda) kama jinsi watu wanavyoshuku baadhi ya polisi na kada ya ualimu wa sekondari na shule za msingi?
Labda hii inaweza kuwa kweli kutokana na mikataba ya ovyo ilisosainiwa na wanasheria wa serikali, na au namna wanavyolazimisha mashitaka na kusababisha serikali kubwagwa mara nyingi kwenye mahakama zetu. Hata upande wa Takukuru tunajionea sinema za namna hii mara nyingi. Napenda kuwasilisha hoja.
 
Back
Top Bottom