Hivi shule ni mtaji?

Balanciaga Jr

Verified Member
Jan 6, 2021
643
1,000
Huwa nakaa nafikiri hivi hii shule tunayosoma na tunaosomesha hivi ina umuhimu saaana? Sipo kuharibu fikra ya mtu ila ngoja niseme yangu na ku-comment chochote ruksa ila sio povu ok.

Kiupande wangu, wasomi ni wengi miaka hii halafu miaka ya kukaa shule ni mirefu mno tofauti na nchi za mbele huku mtu anaanza chuo miaka 20 kuja kuyapambania maisha kashachelewa maskini kagongonyoka kabisa huwa inachosha na kuumiza hasa unamaliza mpaka degree halafu unasugua benchi na mchizi wako wa darasa la saba angalau ana kibanda cha chips.

Kufupisha mada: Elimu ndio ina umuhimu, ila sometimes ni kero kwa kweli. Wasomi ni wengi, ajira chache. Hivi unaonaje mtoto ukamjengea mazingira fulani ya kazi au pa kujishikiza wakati yupo shule na si lazima apate degreee hata akiishia form 4/6 hapo mbona kasonga sana na uwezo wa kujisimamia anao.

Sio lazima kumalizia miaka yako na ujana wako shule kisha kupambana na midaftari halafu unakuta hapati kitu. Shida si kusoma bali kubadili elimu kuwa pesa jaman tusikazanie shule kisa unataka mtotowako awe dokta uwe na focus wangapi wamehitimu u-dokta wangapi wapo wanasugua bech kwenye udokta na kivipi hospital zipo lazima ujiongeze?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom