Hivi Rais Magufuli kulihutubia Bunge na kuahidi kuwa katika kipindi kijacho ataimarisha Demokrasia, maneno hayo yanatoka moyoni mwake au ni usanii?

Hili zigo ni letu sote.
parts
Dunia nzima imeona namna uchaguzi mkuu ulivyovurugwa...........

Sasa tungojee hao tunawaita mabeberu watakavyoanza kutekeleza hiyo azma yao ya vikwazo vya uchumi, ndipo akili zitaanza kutukaa sawa
 
Nianze mada yangu kwa kutoa tafsiri ya neno Demokrasia, ni serikali ya watu iliyochaguliwa na watu katika uchaguzi ulio huru na wa haki

Hata hivyo Rais Magufuli ametoa tafsiri tofauti katika hotuba aliyotoa Bungeni Jana kwa kudai kuwa Demokrasia ni kuleta maendeleo na kuwataka viongozi Wa upinzani wasihoji chochote na watakapofanya hivyo anawaita kuwa wanaleta fujo na uchochezi!

Tumeshuhudia uchaguzi uliojaa kila aina ya malalimiko toka viongozi wa vyama vya upinzani kuwa ulijaa ulaghai na haukuzingatia kanuni ya kuweza kuuita uchaguzi huo kuwa ulikuwa huru na haki.

Hivi kwa viongozi wa upinzani kulalamikia uchaguzi huu kuwa haukuwa huru na haki yalikuwa ni makosa hadi Jeshi la Polisi liwafungulie mashtaka ya ugaidi?

Tumeshuhudia katika utawala huu wa Serikali ya awamu ya 5 ukiturejesha nyuma sana katika suala la kidemokrasia, tokea mfumo huu urejeshwe tena nchini kwetu, mwaka 1992.

Tumeshuhudia katika utawala huu ukitunga sheria kandamizi nyingi tu za kuirejesha nchi yetu katika mfumo wa chama kimoja.

Naweza nikadiriki kusema kuwa nchi yetu hivi sasa imerejea miaka zaidi ya 50 nyuma katika suala la Demokrasia zaidi ya ilivyokuwa katika utawala wa chama kimoja enzi za utawala wa awamu ya kwanza ya Mwalimu Nyerere.

Nakumbuka wakati Wa awamu ya kwanza ya mfumo wa chama kimoja, waziri Wa mambo ya ndani wa wakati huo Ali Hassan Mwinyi akijiuzulu uwaziri wake kwa kuwajibika kutokana na mauaji ya raia wasio na hatia, yaliyotokea wakati huo huko Shinyanga.

Sio yeye tu aliyejiuzulu, Bali hata RPC wa wakati huo Wa mkoa wa Shinyanga naye aliwajibika kwa kujiuzulu.

Hivi katika utawala huu Wa awamu ya 5 ni mauaji mangapi yametokea na viongozi wakiwa hawataki kabisa kujiuzulu, utadhani hakuna tatizo lolote kubwa lilitokea?

Hivi wewe umeshawahi kuona wapi Afisa mkubwa wa Polisi, mwenye cheo cha OCD wa wilaya, kama alivyofanya yule wa wlilaya ya Hai ambaye alimwambia LIVE, aliyekuwa mbunge Wa jimbo hilo, Freeman Mbowe kuwa atashindwa na mgombea wa CCM katika uchaguzi huo na kweli ikatokea utabiri wake kuwa kweli?

Hivi wewe uliwahi kuona wapi, mbunge anashambuliwa na risasi, tena katika makazi wanayokaa waheshimiwa mawaziri, wakati kikao kikiendelea huko Dodoma, kama alivyofanyiwa Mheshimiwa Lissu, hadi sasa ni zaidi ya miaka 3 hakuna mtu yeyote aliyetiwa mbaroni kuhusika na tukio hilo?

Ndiyo maana ninaposikia Rais Magufuli akilieleza Bunge kuwa utawala wake utadumisha Demokrasia, naona kama haina ukweli wowote na ni usanii mtupu na badala yake kama Taifa tutegemee uminywaji mkubwa zaidi wa Demokrasia, ambao Taifa letu halijawahi kushuhudia huko nyuma katika tawala za awamu zilizopita
Huyo haelewagi kinachotoka mdomoni mwake achana naye, Kilaza wa Karne
 
Baba wa taifa aliwaasa CCM kuvilinda vyama vya upinzani alikuwa na sababu zake za msingi kabisa.

Sasa mtu anakuja kuvuruga kazi yote iliyofanywa toka mwaka 1992.. huyu ni adui wa wote wapenda demokrasia.

Mataifa tunaomba msaada wenu..msaada wa haraka sana.
 
Nianze mada yangu kwa kutoa tafsiri ya neno Demokrasia, ni serikali ya watu iliyochaguliwa na watu katika uchaguzi ulio huru na wa haki

Hata hivyo Rais Magufuli ametoa tafsiri tofauti katika hotuba aliyotoa Bungeni Jana kwa kudai kuwa Demokrasia ni kuleta maendeleo na kuwataka viongozi Wa upinzani wasihoji chochote na watakapofanya hivyo anawaita kuwa wanaleta fujo na uchochezi!

Tumeshuhudia uchaguzi uliojaa kila aina ya malalimiko toka viongozi wa vyama vya upinzani kuwa ulijaa ulaghai na haukuzingatia kanuni ya kuweza kuuita uchaguzi huo kuwa ulikuwa huru na haki.

Hivi kwa viongozi wa upinzani kulalamikia uchaguzi huu kuwa haukuwa huru na haki yalikuwa ni makosa hadi Jeshi la Polisi liwafungulie mashtaka ya ugaidi?

Tumeshuhudia katika utawala huu wa Serikali ya awamu ya 5 ukiturejesha nyuma sana katika suala la kidemokrasia, tokea mfumo huu urejeshwe tena nchini kwetu, mwaka 1992.

Tumeshuhudia katika utawala huu ukitunga sheria kandamizi nyingi tu za kuirejesha nchi yetu katika mfumo wa chama kimoja.

Naweza nikadiriki kusema kuwa nchi yetu hivi sasa imerejea miaka zaidi ya 50 nyuma katika suala la Demokrasia zaidi ya ilivyokuwa katika utawala wa chama kimoja enzi za utawala wa awamu ya kwanza ya Mwalimu Nyerere.

Nakumbuka wakati Wa awamu ya kwanza ya mfumo wa chama kimoja, waziri Wa mambo ya ndani wa wakati huo Ali Hassan Mwinyi akijiuzulu uwaziri wake kwa kuwajibika kutokana na mauaji ya raia wasio na hatia, yaliyotokea wakati huo huko Shinyanga.

Sio yeye tu aliyejiuzulu, Bali hata RPC wa wakati huo Wa mkoa wa Shinyanga naye aliwajibika kwa kujiuzulu.

Hivi katika utawala huu Wa awamu ya 5 ni mauaji mangapi yametokea na viongozi wakiwa hawataki kabisa kujiuzulu, utadhani hakuna tatizo lolote kubwa lilitokea?

Hivi wewe umeshawahi kuona wapi Afisa mkubwa wa Polisi, mwenye cheo cha OCD wa wilaya, kama alivyofanya yule wa wlilaya ya Hai ambaye alimwambia LIVE, aliyekuwa mbunge Wa jimbo hilo, Freeman Mbowe kuwa atashindwa na mgombea wa CCM katika uchaguzi huo na kweli ikatokea utabiri wake kuwa kweli?

Hivi wewe uliwahi kuona wapi, mbunge anashambuliwa na risasi, tena katika makazi wanayokaa waheshimiwa mawaziri, wakati kikao kikiendelea huko Dodoma, kama alivyofanyiwa Mheshimiwa Lissu, hadi sasa ni zaidi ya miaka 3 hakuna mtu yeyote aliyetiwa mbaroni kuhusika na tukio hilo?

Ndiyo maana ninaposikia Rais Magufuli akilieleza Bunge kuwa utawala wake utadumisha Demokrasia, naona kama haina ukweli wowote na ni usanii mtupu na badala yake kama Taifa tutegemee uminywaji mkubwa zaidi wa Demokrasia, ambao Taifa letu halijawahi kushuhudia huko nyuma katika tawala za awamu zilizopita
Huo ni usanii toka kwa msanii mzoefu kwenda kwa Bunge dhaifu kuwahi kutokea likiongozwa na yuleyule Spika dhaifu wa Wabunge dhaifu wa ndiyooo toka Chama mfu.
 
Back
Top Bottom