Hivi Rais Magufuli kulihutubia Bunge na kuahidi kuwa katika kipindi kijacho ataimarisha Demokrasia, maneno hayo yanatoka moyoni mwake au ni usanii?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,342
2,000
Nianze mada yangu kwa kutoa tafsiri ya neno Demokrasia, ni serikali ya watu iliyochaguliwa na watu katika uchaguzi ulio huru na wa haki

Hata hivyo Rais Magufuli ametoa tafsiri tofauti katika hotuba aliyotoa Bungeni Jana kwa kudai kuwa Demokrasia ni kuleta maendeleo na kuwataka viongozi Wa upinzani wasihoji chochote na watakapofanya hivyo anawaita kuwa wanaleta fujo na uchochezi!

Tumeshuhudia uchaguzi uliojaa kila aina ya malalimiko toka viongozi wa vyama vya upinzani kuwa ulijaa ulaghai na haukuzingatia kanuni ya kuweza kuuita uchaguzi huo kuwa ulikuwa huru na haki.

Hivi kwa viongozi wa upinzani kulalamikia uchaguzi huu kuwa haukuwa huru na haki yalikuwa ni makosa hadi Jeshi la Polisi liwafungulie mashtaka ya ugaidi?

Tumeshuhudia katika utawala huu wa Serikali ya awamu ya 5 ukiturejesha nyuma sana katika suala la kidemokrasia, tokea mfumo huu urejeshwe tena nchini kwetu, mwaka 1992.

Tumeshuhudia katika utawala huu ukitunga sheria kandamizi nyingi tu za kuirejesha nchi yetu katika mfumo wa chama kimoja.

Naweza nikadiriki kusema kuwa nchi yetu hivi sasa imerejea miaka zaidi ya 50 nyuma katika suala la Demokrasia zaidi ya ilivyokuwa katika utawala wa chama kimoja enzi za utawala wa awamu ya kwanza ya Mwalimu Nyerere.

Nakumbuka wakati Wa awamu ya kwanza ya mfumo wa chama kimoja, waziri Wa mambo ya ndani wa wakati huo Ali Hassan Mwinyi akijiuzulu uwaziri wake kwa kuwajibika kutokana na mauaji ya raia wasio na hatia, yaliyotokea wakati huo huko Shinyanga.

Sio yeye tu aliyejiuzulu, Bali hata RPC wa wakati huo Wa mkoa wa Shinyanga naye aliwajibika kwa kujiuzulu.

Hivi katika utawala huu Wa awamu ya 5 ni mauaji mangapi yametokea na viongozi wakiwa hawataki kabisa kujiuzulu, utadhani hakuna tatizo lolote kubwa lilitokea?

Hivi wewe umeshawahi kuona wapi Afisa mkubwa wa Polisi, mwenye cheo cha OCD wa wilaya, kama alivyofanya yule wa wlilaya ya Hai ambaye alimwambia LIVE, aliyekuwa mbunge Wa jimbo hilo, Freeman Mbowe kuwa atashindwa na mgombea wa CCM katika uchaguzi huo na kweli ikatokea utabiri wake kuwa kweli?

Hivi wewe uliwahi kuona wapi, mbunge anashambuliwa na risasi, tena katika makazi wanayokaa waheshimiwa mawaziri, wakati kikao kikiendelea huko Dodoma, kama alivyofanyiwa Mheshimiwa Lissu, hadi sasa ni zaidi ya miaka 3 hakuna mtu yeyote aliyetiwa mbaroni kuhusika na tukio hilo?

Ndiyo maana ninaposikia Rais Magufuli akilieleza Bunge kuwa utawala wake utadumisha Demokrasia, naona kama haina ukweli wowote na ni usanii mtupu na badala yake kama Taifa tutegemee uminywaji mkubwa zaidi wa Demokrasia, ambao Taifa letu halijawahi kushuhudia huko nyuma katika tawala za awamu zilizopita
 
Luther samwel

Member
May 20, 2020
83
125
Mwaka gani wapinzani hawajawahi kulalamika pili demokrasia ni maendeleo sio kelele tena uchaguzi Mkuu huu ulikuwa ni uchaguzi wa haki kabisa malalamiko kwa wapinzani yalikuwapo hata kabla ya Tanzanian
 
Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,342
2,000
CCM ni chama kinachotegemea vyombo vya dola kuendelea kubaki madarakani, kama alivyonukuliwa hivi karibuni Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dkt Bashiru Ally, akikiri hadharani!
 
Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,342
2,000
Mwaka gani wapinzani hawajawahi kulalamika pili demokrasia ni maendeleo sio kelele tena uchaguzi Mkuu huu ulikuwa ni uchaguzi wa haki kabisa malalamiko kwa wapinzani yalikuwapo hata kabla ya Tanzanian
Hata serikali ya makaburu ya Afrika Kusini, ilikuwa ndiyo serikali iliyojenga miundo bora zaidi barani Afrika katika miaka ile kabla ya miaka ya 90, lakini iling'olewa madarakani kutokana na kuminya Demokrasia.

Hivyo ni lazima uelewe kuwa HAKI, UHURU na MAENDELEO ya watu ni muhimu katika nchi yoyote ile zaidi ya hayo maendeleo ya vitu
 
Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
26,292
2,000
Madikiteita wako hivyo, ndivyo kauli zao. Si rahisi dictator kuacha tabia zake. Just imagie kuwa Jiwe aache haya katika kutawala kwake, IS THIS POSSIBLE? anaweza acha haya mambo kumi chini?

10 Ways to Tell if Your President Is a Dictator

1. Systematic efforts to intimidate the media.

2. Building an official pro-president media network.

3. Politicizing the civil service, military, and the domestic security agencies.

4. Using government surveillance against domestic political opponents.

5. Using state power to reward corporate backers and punish opponents.

6. Stacking the Judiciary.

7. Enforcing the law for only one side.

8. Really rigging the system.

9. Fear mongering.

10. Demonizing the opposition.
 
Stan Mashamba

JF-Expert Member
Apr 22, 2020
1,891
2,000
Nianze mada yangu kwa kutoa tafsiri ya neno Demokrasia, ni serikali ya watu iliyochaguliwa na watu katika uchaguzi ulio huru na wa haki

Hata hivyo Rais Magufuli ametoa tafsiri tofauti katika hotuba aliyotoa Bungeni Jana kwa kudai kuwa Demokrasia ni kuleta maendeleo na kuwataka viongozi Wa upinzani wasihoji chochote na watakapofanya hivyo anawaita kuwa wanaleta fujo!

Tumeshuhudia uchaguzi uliojaa kila aina ya malalimiko toka viongozi wa vyama vya upinzani kuwa ulijaa ulaghai na haukuzingatia kanuni ya kuweza kuuita uchaguzi huo kuwa ulikuwa huru na haki.

Hivi kwa viongozi wa upinzani kulalamikia uchaguzi huu kuwa haukuwa huru na haki yalikuwa ni makosa hadi Jeshi la Polisi liwafungulie mashtaka ya ugaidi?

Tumeshuhudia katika utawala huu wa serikali ya awamu ya 5 ukiturejesha nyuma sana katika suala la kidemokrasia, tokea mfumo huu urejeshwe tena nchini kwetu, mwaka 1992.

Tumeshuhudia katika utawala huu ukitunga sheria kandamizi nyingi tu za kuirejesha nchi yetu katika mfumo wa chama kimoja.

Naweza nikadiriki kusema kuwa nchi yetu hivi sasa imerejea miaka zaidi ya 50 nyuma katika suala la Demokrasia zaidi ya ilivyokuwa katika utawala wa chama kimoja enzi za utawala wa awamu ya kwanza ya Mwalimu Nyerere.

Nakumbuka wakati Wa awamu ya kwanza ya mfumo wa chama kimoja, waziri Wa mambo ya ndani wa wakati huo Ali Hassan Mwinyi akijiuzulu uwaziri wake kwa kuwajibika kutokana na mauaji ya raia wasio na hatia, yaliyotokea wakati huo huko Shinyanga.

Sio yeye tu aliyejiuzulu, Bali hata RPC wa wakati huo Wa mkoa wa Shinyanga naye aliwajibika kwa kujiuzulu.

Hivi katika utawala huu Wa awamu ya 5 ni mauaji mangapi yametokea na viongozi wakiwa hawataki kabisa kujiuzulu, utadhani hakuna tatizo lolote kubwa lilitokea?

Hivi wewe umeshawahi kuona wapi OCD wa wilaya, kama alivyofanya yule wa wlilaya ya Hai ambaye alimwambia LIVE, aliyekuwa mbunge Wa jimbo hilo, Freeman Mbowe kuwa atashindwa na mgombea wa CCM katika uchaguzi huo?

Hivi wewe uliwahi kuona wapi, mbunge anashambuliwa na risasi, tena katika makazi wanayokaa waheshimiwa mawaziri, wakati kikao kikiendelea huko Dodoma, kama alivyofanyiwa Mheshimiwa Lissu, hadi sasa ni zaidi ya miaka 3 hakuna mtu yeyote aliyetiwa mbaroni kuhusika na tukio hilo?

Ndiyo maana ninaposikia Rais Magufuli akilieleza Bunge kuwa utawala wake utadumisha Demokrasia, naona kama haina ukweli wowote na ni usanii mtupu na badala yake kama Taifa tutegemee uminywaji mkubwa zaidi wa Demokrasia, ambao Taifa letu halijawahi kushuhudia huko nyuma katika tawala za awamu zilizopita
Aliahidi dunia nzima kuwa "uchaguzi utakuwa huru na wa haki". Tumejionea vitu tofauti kabisa. Kwa hiyo haaminiki.
 
chabuso

JF-Expert Member
Feb 18, 2013
6,133
2,000
Usiamiamini chachote anachosema,hukumbuki aliiambia dunia na kutuma barua Kwa raisi wa Marekani kuwa Uchaguzi utakuwa huru na wa haki

Si unakumbuka Nini kilitokea wakati wa Uchaguzi!?
 
Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,342
2,000
Usiamiamini chachote anachosema,hukumbuki aliiambia dunia na kutuma barua Kwa raisi wa Marekani kuwa Uchaguzi utakuwa huru na wa haki

Si unakumbuka Nini kilitokea wakati wa Uchaguzi!?
Hakika Rais wetu, ni mtu mwenye ndimi mbili, anachosema na anachofanya ni vitu viwili tofauti sana
 
Rogojin The Idiot

JF-Expert Member
Jul 25, 2017
1,474
2,000
Watanzania wanataka kula, na kusheherekea maisha. Haya mambo ya siasa sio shida yao kabisa. Ndio maana hawakuandamana. Wakaishia vijiweni kutafuta riziki.
Awamu hii Rais ajitahidi kuhakikisha biashara zetu zinalindwa na sio kufilisiwa na kodi zisizolipika. Ahakikishe kunakuwa na uwekezaji wa ndani na nje pia.
Vyombo vyake vya kodi visione wafanya biashara kama ni watu hatari, wenye malengo ya kukwepa kodi tu. Kuna wakati watu wanakwepa kodi sababu ya dhuluma ambayo wanapata sababu tu ya kuambiwa wanatakiwa kulipa kodi.
Kodi ni wajibu wetu kulipa. Ila lazima ziwe kodi stahiki
 
Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
8,235
2,000
Huyo siyo wa kumuamini, aiutangazia ulimwengu kuwa uchaguzi wa waka huu utakuwa huru na haki, nadhani wewe mwenyewe ulikuja uajionea uchafuzi uliotokea!
Never Trust Jiwe!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom