Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,484
- 30,160
Nimekuwa nafuatilia mwenendo wa utawala huu wa awamu ya tano na nimekuja na "conclusion" kuwa Rais Magufuli anataka kuigeuza nchi hii ya Tanzania kuwa Mali yake binafsi na yeye anaamini kuwa atakalosema yeye ndiyo sheria na litatekelezwa!
Tunajua wazi kuwa Rais Magufuli kabla hajaingia madarakani, aliapa kuwa ataitii na kuiheshimu Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya mwaka 1977
Katiba hiyo katika ibara ya 3(1) inaeleza kuwa nchi yetu itafuata misingi ya kidemokrasia na ni nchi ya vyama vingi
Hebu sasa tuangalie kama kweli nchi yetu inafuata misingi ya kidemokrasia na ni ya vyama vingi??
Jibu langu kwa swali hilo ni HAPANA kubwa sana
Hebu kwanza tupate tafsiri ya neno Demokrasia, kama ilivyotafsiriwa kwenye kamusi ya kiswahili kuwa Demokrasia maana yake ni serikali iliyochaguliwa na watu kupitia sanduku la kura, katika uchaguzi ulio huru na wa haki na watu hao wakiwa ndiyo wenye kauli ya mwisho ya namna wanavyotaka serikali yao itakavyoendeshwa
Hilo swala la pili kuwa nchi yetu inaendeshwa kwa mfumo wa vyama vingi, jibu lake liko wazi kabisa, kuwa vyama hivyo ni LAZIMA vipate haki sawa katika uendeshaji wa shughuli zao
Tuje kwenye uhalisia wa mambo yanavyoendeshwa hapa nchini
Tulimuona Rais Magufuli, mara tu alipoingia madarakani mwaka 2015, akivipiga marufuku vyama vyote vya kisiasa vya upinzani kutofanya mikutano yoyote ya kisiasa hadi mwaka 2020, wakati yeye na chama chake cha CCM kila kukicha tukiwaona wakichanja mbuga nchi nzima wakikifanyia kampeni chama chao cha CCM!
Nimuulize Rais wangu Magufuli, hivi hiyo kuvipiga marufuku vyama vya kisiasa vya upinzani, visifanye mikutano yoyote ya kisiasa, alitumia ibara ipi ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya mwaka 1977??
Tunashuhudia pia uchaguzi wa serikali ya mitaa ukivurugwa kwa kiasi kikubwa sana na wasimamizi wa uchaguzi, ambao ni makada wa CCM, wakiwaengua wagombea wa vyama vya upinzani, hivi kwa kufanya hivyo ndiyo wanatekeleza kwa vitendo kuwa uongozi wa nchi hii watachaguliwa na wananchi katika maeneo yao, kwa kutumia sanduku la kura, katika uchaguzi ulio huru na wa haki??
Tunashuhudia pia kuwa pamoja na kuvurugika kwa kiasi cha kutisha uchaguzi huu na pamoja na miito mbalimbali ya vyama vya kisiasa vya upinzani kuwa ufutwe na upangwe upya chini ya Tume huru ya uchaguzi, tunashuhudia viongozi walioko madarakani wakisisitiza kuwa uchaguzi huo utaendelea hivyo hivyo licha ya kilio cha wapinzani kuwa ufutwe
Hivi kwa mifano hiyo michache niliyoitoa, nitakuwa nakosea kweli, nikisema kuwa Rais Magufuli ameamua kwa makusudi kabisa, kuisigina Katiba ya nchi na kulifanya Taifa hili na watu wake kuwa mali yake binafsi??
Nakaribisha hoja zitolewe kwa kuzingatia maslahi mapana na kuangalia mustakabali wa Taifa hili ambalo sisi wananchi wake hatupendi lisambaratike