Hivi Rais Magufuli anataka kuigeuza Tanzania kuwa mali yake binafsi?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,477
30,137
Nimekuwa nafuatilia mwenendo wa utawala huu wa awamu ya tano na nimekuja na "conclusion" kuwa Rais Magufuli anataka kuigeuza nchi hii ya Tanzania kuwa Mali yake binafsi na yeye anaamini kuwa atakalosema yeye ndiyo sheria na litatekelezwa!

Tunajua wazi kuwa Rais Magufuli kabla hajaingia madarakani, aliapa kuwa ataitii na kuiheshimu Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya mwaka 1977

Katiba hiyo katika ibara ya 3(1) inaeleza kuwa nchi yetu itafuata misingi ya kidemokrasia na ni nchi ya vyama vingi

Hebu sasa tuangalie kama kweli nchi yetu inafuata misingi ya kidemokrasia na ni ya vyama vingi??

Jibu langu kwa swali hilo ni HAPANA kubwa sana

Hebu kwanza tupate tafsiri ya neno Demokrasia, kama ilivyotafsiriwa kwenye kamusi ya kiswahili kuwa Demokrasia maana yake ni serikali iliyochaguliwa na watu kupitia sanduku la kura, katika uchaguzi ulio huru na wa haki na watu hao wakiwa ndiyo wenye kauli ya mwisho ya namna wanavyotaka serikali yao itakavyoendeshwa

Hilo swala la pili kuwa nchi yetu inaendeshwa kwa mfumo wa vyama vingi, jibu lake liko wazi kabisa, kuwa vyama hivyo ni LAZIMA vipate haki sawa katika uendeshaji wa shughuli zao

Tuje kwenye uhalisia wa mambo yanavyoendeshwa hapa nchini

Tulimuona Rais Magufuli, mara tu alipoingia madarakani mwaka 2015, akivipiga marufuku vyama vyote vya kisiasa vya upinzani kutofanya mikutano yoyote ya kisiasa hadi mwaka 2020, wakati yeye na chama chake cha CCM kila kukicha tukiwaona wakichanja mbuga nchi nzima wakikifanyia kampeni chama chao cha CCM!

Nimuulize Rais wangu Magufuli, hivi hiyo kuvipiga marufuku vyama vya kisiasa vya upinzani, visifanye mikutano yoyote ya kisiasa, alitumia ibara ipi ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya mwaka 1977??

Tunashuhudia pia uchaguzi wa serikali ya mitaa ukivurugwa kwa kiasi kikubwa sana na wasimamizi wa uchaguzi, ambao ni makada wa CCM, wakiwaengua wagombea wa vyama vya upinzani, hivi kwa kufanya hivyo ndiyo wanatekeleza kwa vitendo kuwa uongozi wa nchi hii watachaguliwa na wananchi katika maeneo yao, kwa kutumia sanduku la kura, katika uchaguzi ulio huru na wa haki??

Tunashuhudia pia kuwa pamoja na kuvurugika kwa kiasi cha kutisha uchaguzi huu na pamoja na miito mbalimbali ya vyama vya kisiasa vya upinzani kuwa ufutwe na upangwe upya chini ya Tume huru ya uchaguzi, tunashuhudia viongozi walioko madarakani wakisisitiza kuwa uchaguzi huo utaendelea hivyo hivyo licha ya kilio cha wapinzani kuwa ufutwe

Hivi kwa mifano hiyo michache niliyoitoa, nitakuwa nakosea kweli, nikisema kuwa Rais Magufuli ameamua kwa makusudi kabisa, kuisigina Katiba ya nchi na kulifanya Taifa hili na watu wake kuwa mali yake binafsi??

Nakaribisha hoja zitolewe kwa kuzingatia maslahi mapana na kuangalia mustakabali wa Taifa hili ambalo sisi wananchi wake hatupendi lisambaratike
 
Wananchi huwa tunajiuliza hivi hawa wateule wake ambao huwa wanaisigina waziwazi kwa vitendo vyao na wananchi tumepiga kelele sana, lakini yeye Rais ameamua kuweka pamba masikioni.

Nitatoa mifano michache, akina Bashite, Ole Sabaya, Chalamila na Gambo, just to mention a few, ambao wamekuwa "untouchables" kwa kuwa ni wateule wa Rais na yeye hasikilizi kelele za wapiga debe!

Hivi hiyo ndiyo kutekeleza kweli ile tafsiri ya demokrasia kuwa ni serikali ya watu inayochaguliwa na watu kwa ajili ya kuwatumikia watu??
 
Nimekuwa nafuatilia mwenendo wa utawala huu wa awamu ya tano na nimekuja na "conclusion" kuwa Rais Magufuli anataka kuigeuza nchi hii ya Tanzania kuwa Mali yake binafsi na yeye anaamini kuwa atakalosema yeye ndiyo sheria na litatekelezwa!

Tunajua wazi kuwa Rais Magufuli kabla hajaingia madarakani, aliapa kuwa ataitii na kuiheshimu Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya mwaka 1977

Katiba hiyo katika ibara ya 3(1) inaeleza kuwa nchi yetu itafuata misingi ya kidemokrasia na ni nchi ya vyama vingi

Hebu sasa tuangalie kama kweli nchi yetu inafuata misingi ya kidemokrasia na ni ya vyama vingi??

Jibu langu kwa swali hilo ni HAPANA kubwa sana

Hebu kwanza tupate tafsiri ya neno Demokrasia, kama ilivyotafsiriwa kwenye kamusi ya kiswahili kuwa Demokrasia maana yake ni serikali iliyochaguliwa na watu kupitia sanduku la kura, katika uchaguzi ulio huru na wa haki na watu hao wakiwa ndiyo wenye kauli ya mwisho ya namna wanavyotaka serikali yao itakavyoendeshwa

Hilo swala la pili kuwa nchi yetu inaendeshwa kwa mfumo wa vyama vingi, tafsiri yake iko wazi kabisa, kuwa vyama hivyo ni LAZIMA vipate haki sawa katika uendeshaji wa shughuli zao

Tuje kwenye uhalisia wa mambo yanavyoendeshwa hapa nchini

Tulimuona Rais Magufuli, mara tu alipoingia madarakani mwaka 2015, akivipiga marufuku vyama vyote vya kisiasa vya upinzani hadi mwaka 2020, wakati yeye na chama chake cha CCM kila kukicha tukiwaona wakichanja mbuga nchi nzima wakikifanyia kampeni chama chao cha CCM!

Nimuulize Rais wangu Magufuli, hivi hiyo kuvupiga marufuku vyama vya kisiasa vya upinzani, alitumia ibara ipi ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya mwaka 1977??

Tunashuhudia pia uchaguzi wa serikali ya mitaa ukivurugwa kwa kiasi kikubwa sana na wasimamizi wa uchaguzi, ambao ni makada wa CCM, wakiwaengua wagombea wa vyama vya upinzani, hivi kwa kufanya hivyo ndiyo wanatekeleza kwa vitendo kuwa uongozi wa nchi hii watachaguliwa na wananchi katika maeneo yao, kwa kutumia sanduku la kura, katika uchaguzi ulio huru na wa haki??

Tunashuhudia pia kuwa pamoja na kuvurugika kwa kiasi cha kutisha uchaguzi huu na pamoja na miito mbalimbali ya vyama vya kisiasa vya upinzani kuwa ufutwe na upangwe upya chini ya Tume huru ya uchaguzi, tunashuhidia viongozi walioko madarakani wakisisitiza kuwa uchaguzi huo utaendelea hivyo hivyo licha ya kilio cha wapinzani kuwa ufutwe

Hivi kwa mifano hiyo michache niliyoitoa, nitakuwa nakosea kweli, nikisema kuwa Rais Magufuli ameamua kwa makusudi kabisa, kuisigina Katiba ya nchi na kulifanya Taifa hili na watu wake kuwa mali yake binafsi??

Nakaribisha hoja zitolewe kwa kuzingatia maslahi mapana na kuangalia mustakabali wa Taifa hili ambalo sisi wananchi wake hatupendi lisambaratike
Tanzania haiwezi kuwa kama Rwanda abadani
 
Wananchi huwa tunajiuliza hivi hawa wateule wake ambao huwa wanaisigina waziwazi kwa vitendo vyao na wananchi tumepiga kelele sana, lakini yeye Rais ameamua kuweka pamba masikioni.

Nitatoa mifano michache, akina Bashite, Ole Sabaya, Chalamila na Gambo, just to mention a few, ambao wamekuwa "untouchables" kwa kuwa ni wateule wa Rais na yeye hasikilizi kelele za wapiga debe!

Hivi hiyo ndiyo kutekeleza kweli ile tafsiri ya demokrasia kuwa ni serikali ya watu inayochaguliwa na watu kwa ajili ya kuwatumikia watu??
Hao dawa yake unawafanyia ile Kitu Kleluu aliifanya huko Iringa kwa mkuu wa Mkoa miaka hiyooo. Zamani watu walikuwa na Akili sana hawakupenda kudharauliwa na Mabashite.
 
Mbona alishaigeza Mali yake tayari Mkuu. Anaongoza Dead bodies pia!
Nchi hii ni Mali ya Mungu na ndiye aliyetuumba na ni yeye pekee ndiye anayejua siku yetu ya mwisho ya kuishi hapa duniani..........

Kwa binadamu yoyote kwa ulevi tu wa madaraka, kwa kuamini kuwa amezungukwa na majeshi ambayo yanamtiii yeye akaamini kuwa ana uwezo unaofanana na Mungu anajidanganya waziwazi na anafanya kufuru kubwa sana!
 
Tufanyaje Sasa hahaha
FB_IMG_15737054103547969.jpeg
 
Nchi hii ni Mali ya Mungu na ndiye aliyetuumba na ni yeye pekee ndiye anayejua siku yetu ya mwisho ya kuishi hapa duniani..........

Kwa binadamu yoyote kwa ulevi tu wa madaraka, kwa kuamini kuwa amezungukwa na majeshi ambayo yanamtiii yeye akaamini kuwa ana uwezo unaofanana na Mungu anajidanganya waziwazi na anafanya kufuru kubwa sana!
Sahihi, lakini nayeye Kila Pigo atalionja hata kwa watoto wake ama Vitukuu. Malipo hapa hapa Duniani!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom