Opuk Jater
Senior Member
- Dec 25, 2018
- 145
- 130
------------Hizo ni athari za lugha ya nyumbani na sio rahisi kubadilisha kama unavyofikiri.Lugha yoyote inayokuja kwako kama lugha ya pili lazima itaathiriwa na lugha ya kwanza.Nailo ni swala la ulimi sio akili.Hata wazungu kwenye nchi wanazozungumza kingereza wanatofautiana lafudhi kati ya nchi na nchi wakati lugha ni ile ile.kwaiyo hiyo ni kawaida sana kwenye jamii yetu na kamwe hatuwezi kufanana ulimi.
nuruyamnyonge, Haya si makosa ya kisarufi, useme kwa mfano, kusema anakujaga ni makosa, Kiswahili sahihi ni kusema anakuja.
Haya ni makosa ya kuchanganya herufi.
Kwa mfano, Magufuli mtu atamke "Magufuri" au "Mzee wa Kiraracha" mtu atamke "Mzee wa Kilalacha".
Hivyo basi, utaona ni vigumu kuweka kanuni katika makosa ambayo kimsingi si ya kisarufi (grammatical), bali ni ya kimatamshi (phonetical).
utakuta mtu na masters yake anaandika reo badala ya leoNi Mazoea ya watu tu, HALAFU CHA AJABU UTAKUTA MSOMI MZIMA ANACHANGANYA HIZI HERUFI
hakuna cha lugha za mama, kwani wengine hawana lugha za mama, umejuaje kibeberu {zungu} kama si kujifunza?Naomba usinijumuishe kwenye huo upumnavu wa watu wachache ambao lugha mama zimeathiri matamshi yao kwenye lugha hii ya kiswahili.
Watu wanajifunza na kunyoosha lugha. Hajataka tu.Kwenye kutamka ndio ana shida, sina hakika anapoandika. Hilo la kumtaka hana ujanja nalo kutokana na utumiaji mkubwa wa lugha ya mama utotoni, hilo halina mjanja ni kwa yoyote kuathiriwa na mother tongue.
Tatizo lingine kubwa ni hili kama lako. Wengi hawajui wapi h au a inatumika. Mfano wewe ulitakiwa kuandika waandishi. Au mwingine hajui tofauti ya HANA na ANA.Tatizo hili sio hapa jf tuu.yaani Wahandishi na watangazaji karibu wote kwenye tv za mitandaoni .wana tatizo hili R na L