BAKITA fanyeni uchunguzi na mtoe msaada kwa wanaochanganya R na L

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,620
46,264
Kuna wakati nilifikiri hili ni tatizo la baadhi ya kanda au mikoa fulani ila nimegundua sasa kila mkoa wa Tanzania wapo watu wengi wanaongea na kuandika kwa kuchanganya hizi herufi mbili, mfano mtu anasema.

Tofari badala ya Tofali
Karamu badala ya Kalamu
Siraha badala ya Silaha
Mchere badala ya Mchele
Jasili badala ya Jasiri
Lekebisha badala ya Rekebisha n.k

BAKITA fanyeni uchunguzi muone kama ni matatizo katika ubongo, kushindwa kukaza ulimi kwa wazungumzaji au udhaifu katika ufundishaji wa Kiswahili shule za msingi ndio kumepelekea tatizo hilo kushika kasi kila kona ya nchi, ukisikiliza vi online TV ndio kichefuchefu zaidi, ni kama hicho ndio kigezo cha kuwa mtangazaji huko.
 
Kuna wakati nilifikiri hili ni tatizo la baadhi ya kanda au mikoa fulani ila nimegundua sasa kila mkoa wa Tanzania wapo watu wengi wanaongea na kuandika kwa kuchanganya hizi herufi mbili, mfano mtu anasema
Tofari badala ya Tofali
Karamu badala ya Kalamu
Siraha badala ya Silaha
Mchere badala ya Mchele
Jasili badala ya Jasiri
Lekebisha badala ya Rekebisha n.k

BAKITA fanyeni uchunguzi muone kama ni matatizo katika ubongo, kushindwa kukaza ulimi kwa wazungumzaji au udhaifu katika ufundishaji wa Kiswahili shule za msingi ndio kumepelekea tatizo hilo kushika kasi kila kona ya nchi, ukisikiliza vi online TV ndio kichefuchefu zaidi, ni kama hicho ndio kigezo cha kuwa mtangazaji huko.
as long as the concept is home nd dry hayo mengine ni mbwembwe
 
Kama huwezi kuzungumza vizuri lugha yako uliyozaliwa na kukuzwa nayo unakuwa kilaza mkubwa sana. Hata ujengaji wako hoja unakuwa wa hovyo tu.
as long as the concept is home nd dry hayo mengine ni mbwembwe
 
Andiko/uzi/ habari au taarifa yenye makosa hasa palipotakiwa kuwepo R lkn IPO L
Inakera Sana maranyingi naishia kuipita sisomi maana najua Ni uwongo Sijui kwa nini nimekuwa hivi
 
Ni tatizo la kiakili zaidi. Speech center kwenye brain ina shida. R na L matamshi tofauti kabisa. Inakera.
 
Kuna wakati nilifikiri hili ni tatizo la baadhi ya kanda au mikoa fulani ila nimegundua sasa kila mkoa wa Tanzania wapo watu wengi wanaongea na kuandika kwa kuchanganya hizi herufi mbili, mfano mtu anasema.

Tofari badala ya Tofali
Karamu badala ya Kalamu
Siraha badala ya Silaha
Mchere badala ya Mchele
Jasili badala ya Jasiri
Lekebisha badala ya Rekebisha n.k

BAKITA fanyeni uchunguzi muone kama ni matatizo katika ubongo, kushindwa kukaza ulimi kwa wazungumzaji au udhaifu katika ufundishaji wa Kiswahili shule za msingi ndio kumepelekea tatizo hilo kushika kasi kila kona ya nchi, ukisikiliza vi online TV ndio kichefuchefu zaidi, ni kama hicho ndio kigezo cha kuwa mtangazaji huko.
Duh. Waswahili sasa hawawezi hata kuandika Kiswahili vizuri. Wanafunzi wa chuo ni aibu kubwa sana kwa taifa
 
Cha ajabu hata mwalimu anaefundisha kiswahili anaandika "hasubuhi" ndio huwa nachoka kabisa.....
Naona tumefika kwenye "bora elimu"
Bora huyo wa hasubui na asubui, maana kimatamshi ni similar ila R na L haivumiliki, utadhani ni mtoto anajifunza kuongea bana. Takataka kabisa. Mi huwa siendelei kusoma nikishajua mtu ana shida hiyo.
 
Wanatakiwa wachukue hatua kali maana hali ni mbaya sana, lakini ndio hivyo hakuna wanachofanya
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom