Tulimumu
JF-Expert Member
- Mar 11, 2013
- 14,378
- 13,130
Tanzania ndiyo nchi pekee duniani inayotawaliwa na marais wawili kwa wakati mmoja, mabunge mawili, nyimbo za taifa mbili, majaji wakuu wawili, katiba mbili, bendera mbili, maspika wawili, makamu wa rais sasa hivi watatu, marais wanaopigiwa mixinga 21 wawili nk
Zamani ilikuwa Rais akitokea Zanzibar, makamu anatokea Tanganyika. Rais akitokea Tanganyika, makamu anatoka Zanzibar. Wakati wa Mwinyi kulikuwa na makamu wa kwanza wa Rais ambaye alikuwa ni jaji Warioba kwakuwa marais wote walikuwa ni wazanzibari na rais wa Zanzibar akawa makamu wa pili wa rais.
Kwa mfumo wa muungano huu haitatokea kamwe kuwa na marais wote kutokea Tanganyika kwakuwa Tanganyika ilikufa hivyo haiwezekani kamwe kwa mtanganyika kuwa rais wa Zanzibar.
Sasa hivi nchi inatawaliwa na wazanzibari watupu. Je wakiungana kupanga lolote kuhusu Tanganyika tutapona? Je hamuoni wanagawa vyeo visivyo vya muungano kwa wazanzibari wakati watanganyika zaidi ya milioni 60 wanaangalia tu? Huku kuna wazanzibari wanashika uDC na uwaziri wakati hazipo chini ya muungano lakini hakuna mtanganyika anaweza kupewa hata usheha huko Zanzibar.
Katiba iandikwe upya kuondoa kasoro kama hizi sema kikwazo kikubwa ni watanganyika wenyewe hawaitaki nchi yao eti jitu zima utalisikia linasema katiba haileti maji, barabara, umeme ... wakati wenzetu wazanzibar hawazidi milioni 2 lakini huwezi kuwaambia lolote kuhusu nchi yao.
PIA SOMA
- Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?