Hivi ni sahihi kwa watanzania kununua nyanya za Oman ?

JAMII-ASM

JF-Expert Member
Jul 30, 2015
1,305
524
Nakumbuka bunge lililopita Mh. Lugola ali ilalamikia Wizara ya Biashara na Viwanda kwa kuruhusu uagizaji wa bidhaa ambazo kimsingi zingeweza kuzalishwa hapa nchini.Leo nimekutana na nyanya 'tomato paste' made in oman. Kwa kweli ina ubora wa hali ya juu.
Lakini je, ni halali kwa watanzania kuagiza nyanya Oman.Hivi hatupotezi fedha za kigeni kwa kuagiza vitu ambavyo tunauwezo wa kusindika wenyewe ?Utumwa huu wa akili utaisha lini.
Almudhish Tomato Paste Oman..

tomatto1.png
 
tusikosoe tu na kulaumu hawa wafanyabiashara wakati viwanda vya uhakika hapa hakuna, mfanyabiashara anaangaliA mlaji anataka nini na anapata faida gani kumletea mlaji hiyo bidhaa, walaji wamekosa paste nzuri bongo ndio maana wananunua za nje, ngoja tuone huyu jamaa aliyesema tanzania yake itakua ya viwanda baada ya miaka 3 kama tutakua tunaagiza bidhaa simple kama hizi nje atakua ameshindwa hii ahadi yake
 
Sionyanya za oman tu .hata peanut butter .tomatosuoce ya american garden..paster tambi za italy .zabibu .maziwa kutoka kenya na vingi sana ila wewe umeona oman tu ndio imekushtua
 
Nakumbuka bunge lililopita Mh. Lugola ali ilalamikia Wizara ya Biashara na Viwanda kwa kuruhusu uagizaji wa bidhaa ambazo kimsingi zingeweza kuzalishwa hapa nchini.Leo nimekutana na nyanya 'tomato paste' made in oman. Kwa kweli ina ubora wa hali ya juu.
Lakini je, ni halali kwa watanzania kuagiza nyanya Oman.Hivi hatupotezi fedha za kigeni kwa kuagiza vitu ambavyo tunauwezo wa kusindika wenyewe ?Utumwa huu wa akili utaisha lini.
Almudhish ::
Utumwa huu utaisha pale tutakapoamua kwa hiari yetu kuvipenda vitu vilivyo zalishwa nchini mwetu. Unakuta mhehe naye ana kopo la Tomato sauce ya India wakati nyanya original zipo pale Ilula.

Tatizo, ni kwamba, wengi wetu tunajifanya tumekaa Ulaya na matembele tumesahau kuyala tunataka canned food, na wengine wanadhani wakienda kununua wali pale Shoprite wanaona watakuwa wamewaonyesha majirani zao kwamba nao wamepanda daraja.

La tatu, ni hili, upungufu wa ubora wa bidhaa zetu nao unachangia watu kupenda vya nje. Nadhani hata wewe ni shahidi, habari ya bidhaa za mchina. Hapa serikali ikisimamia suala la Viwango vya bidhaa zetu tunaweza kurudi kwenye msitari.
 
Swala sio kupenda vilivyozalishwa nyumbani. Hizi nyanya za makopo pamoja na vyote vinavyotoka nje tatizo havilipiwi kodi, si mnaona makontena yanapitishwa bila kodi, kwa hiyo bei yake inakuwa ndogo, vikilipiwa kodi kama inavyostahili haviwezi kununulika kirahisi. Wacheni walete lakini walipie kodi stahiki.
 
Sasa wewe kama umeona Fursa hio na unaona uwezo wa kutengeneza unao kwa gharama nafuu si utengeneze mkuu na kuuzia wananchi wenzako ?

"Millions Saw an Apple Fall..., But Newton was the One who Asked Why...."
 
Sionyanya za oman tu .hata peanut butter .tomatosuoce ya american garden..paster tambi za italy .zabibu .maziwa kutoka kenya na vingi sana ila wewe umeona oman tu ndio imekushtua
Imenishtua kwa sababu moja kuu. Oman haina ardhi yenye rutba kama yetu. Oman wamegeuza majangwa yao kwa gharama kubwa na kuwa ardhi inayozalisha bidhaa nyingi..mojawapo ikiwa ni nyanya hizi. na sasa niwakulima wazuri tu.Hivi sisi tunashindwa nini ?
 
Utumwa huu utaisha pale tutakapoamua kwa hiari yetu kuvipenda vitu vilivyo zalishwa nchini mwetu. Unakuta mhehe naye ana kopo la Tomato sauce ya India wakati nyanya original zipo pale Ilula.

Tatizo, ni kwamba, wengi wetu tunajifanya tumekaa Ulaya na matembele tumesahau kuyala tunataka canned food, na wengine wanadhani wakienda kununua wali pale Shoprite wanaona watakuwa wamewaonyesha majirani zao kwamba nao wamepanda daraja.

La tatu, ni hili, upungufu wa ubora wa bidhaa zetu nao unachangia watu kupenda vya nje. Nadhani hata wewe ni shahidi, habari ya bidhaa za mchina. Hapa serikali ikisimamia suala la Viwango vya bidhaa zetu tunaweza kurudi kwenye msitari.

Kila mwenye hela anapenda kutumia kitu kizuri tatizo viwanda vya bongo vingi havijali ubora wa bidhaa zao
 
Na kwanini ununue minyanya ya kopo wakati bongo ziko fresh za shamba?! Mtumwa ni we unaenunua, nunua za gengeni bhana..
 
Back
Top Bottom